angalieni umakini wa waandishi wetu!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

angalieni umakini wa waandishi wetu!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ms Judith, Apr 21, 2011.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  wadau, linganisheni kichwa cha habari na hizo aya nilizowekea rangi ya blue halafu muone aina ya waandishi tulionao

  nawasilisha
  ........................


  CHADEMA: Tutahoji utajiri wa Ridhiwan

  Thursday, 21 April 2011 08:17 0digg

  Geofrey Nyang'oro, Singida
  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk Willbroad Slaa amesema chama chake kinajipanga kuhoji kile alichodai utajiri mkubwa wa ghafla wa Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji na pia Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).

  Dk Slaa alisema hayo jana katika Kijiji cha Ikungi, mkoani Singida alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara.

  Alisema anajua kuwa mjumbe huyo (jina tunalihifadhi kwa kuwa jitihada za kumpata kujibu tuhuma hizo hazikufanikiwa), licha ya umri wake mdogo hivi sasa ana fedha nyingi.

  Katika mkutano huo Dk Slaa alimtuhumu kuwa na utajiri uliopindukia ambao alisema haulingani na umri wake.

  Dk Slaa alisema chama chake kina shaka na wingi wa fedha alizonazo kijana huyo na kwamba atahakikisha kwamba kigogo huyo anaiambia Chadema na Watanzania alipozipata.

  Alisema kijana huyo alimaliza masomo yake muda mfupi uliopita, lakini tayari amekuwa bilionea akisisitiza kuwa chama chake kitahoji alipopata mabilioni hayo.

  "Ninajua kwamba ana fedha nyingi, lakini huyu alikuwa mtoto wa shule juzi tu. Leo amekuwa bilionea! Atatuambia amepata wapi hizo fedha, Chadema tutahoji ni wapi amezipata," alisema Dk Slaa.

  Dk Slaa pia alizungumzia kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuwa kelele za wapinzani hazimnyimi usingizi na kusema watahakikisha halali.

  Mgombea huyo wa urais kwa tiketi ya Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana alitoa kauli hiyo alipozungumzia ushindi wa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu akisema umeimarisha ngome ya upinzani bungeni.

  "Rais Kikwete alisema kelele za upinzani hazimnyimi usingizi, lakini kwa kumchagua Lissu mmeongeza nguvu ya upinzani na sasa hatalala," alisema na kuongeza:

  "Ujumbe wangu kwenu ni kwamba sasa mmemchagua mbunge jasiri anayeweza kumwambia Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mbele ya Waziri Mkuu kuwa amekuwa mvivu kusoma."

  Alisema kutokana na ujasiri huo wa Lissu sasa miswada mibovu haitapelekwa bungeni.

  Awali, akizungumza katika mkutano huo, Lissu alisema Halmashauri ya Wilaya ya Singida imetenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo akisema kuwa ni mara ya kwanza fedha hizo kutengwa huku akijigamba kwamba ni kutokana na wapinzani kubana mianya ya wizi.

  source: http://www.mwananchi.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/11222-chadema-tutahoji-utajiri-wa-ridhiwan.html
   
 2. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu unayoyasema yana ukweli; kwani kama kichwa cha habari kinamtaja mhusika hapakuwepo sababu yeyote kusema kwenye habari yenyewe, ya kuwa jina la mhusika halitatajwa. Sasa sijui ni nani alaumiwa kwaajili ya mapungufu hayo, kati ya mhandishi wa habari hiyo na mhariri wake?
   
 3. s.fm

  s.fm JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 669
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hizo ndio kazi za waandishi wengi tulio nao, ukisoma story utajua tu kama hapa kuna visa, interest ama kitu fulani hasa katika hizi habari za siasa..sasa tatizo unakuja kujikuta unaandika madudu kama usipokua makini kwa sababu lengo lako linakua halieleweki.
   
Loading...