Angalieni kuchanganyikiwa kwa CCM, eti chama na Serekali nivitu viwili tafauti!

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
Jee Serekali si inaongozwa na chama tawala na chama kinacho shinda si kinacho fuata sera zake za chama na itikadi za chama? Sasa Nappy unataka kutwambia hivi sasa kua chama na serekali viko mbali katika mipango yakuendesha nchi?.

Sera za ccm nikulinda mafisadi na ndio ukaona nikulindana lindana tu ccm kwakua kila moja sio msafi na wako wengi tu katika mazambi hayo ya ufisani na wengine wamo kwenye vinyaganyiro vya kugombea uraisi.

Kuna ufisadi wakutisha kama Richmon na ule wa Tageta Escrow watu walotafuna mabilionea na hivi sasa wako kwenye kinyaganyiro cha uchaguzi na chama bado kimeshindwa kuwa fungulia kesi za kula mabilion ya Umma na kutaifisha mali zao.

Jee tuseme hawa viongozi wa ccm na makada wao hawayaoni haya? kama wanayaona kwa nini wameshindwakuwafikisha kwenye vyombo vya sheria kuwa wizi wa mamillion ya Dollas ambazo zingetusaidia wanyonge kwa madawa na elimu .

tukiashana na hilo katiba ya Jaji Warioba ilisema Mbunge yoyote anaweza kuhukumiwa na wananchi waliomchagua katika jimbo lake kabla hata yakumaliza kipindi chake cha miaka 5?,sasa unapo twambia Neppy Nawiye kua mara hii tuwawajibishe? kwa sheria gani haliyakua nyiyi ndio muliopinga sheria ya kuwajibishwa?.

Au ndio msimu wa uchaguzi umeingia munataka kura tuwape halafu muendelee kubakia madakani na kuendeleza ufisadi.Mara hii ccm hamuwadanganyi tena wananchi kwa ulahai na kuwaona Watanzania ni Matasira, ma-foolish ili mchezo uendelee kuwa ule ule wa Ufisadi huku walala hoi wa tukihangaika kwa mlo wa siku.

Mukitaka kura munakuja na maneno matamu lakini baado mumekumbatia ilani ya kulindana na kuwalinda mafisadi wenye kujilimbikizia mabilioni ya Dollar na rasilimali zakutisha, mara hii tunataka kuangalia ahadi za upinzani nyiyi punzikeni kidogo miaka 50 inatosha ni nusu karne bado Watanzania tumekua maskini wakutupwa na viongozi wakiwa na utajiri wakutisha.

Tanzania ni nchi yenye rasilimali nyingi lakini haziwanufaishi Watanzania wenyewe ,bali ni vigogo na wawekezaji wa kigeni kwa mikataba mibovu yaufisadi.


https://www.youtube.com/watch?t=143&v=41UCnZxDuBQ
https://www.youtube.com/watch?t=50&v=QQppjgDgaik
 
Jee huku si kutafuta Mchawi hali yakua wachawi ni wao? sheria za kuwajibiswa viongozi wasio wadilifu wamezipinga kwenye katiba kwa lengo tu lakulindana na kulinda mafisadi, walio pinga kwenye Bunge la katiba ni nani kama siowao ccm kwa wingi wao wa kura?

Sasa Mh Kinana na Mh Neppy munazani kua Watanzania ni Danganya toto(Ma-Foolish)ili muendelee kulindana na kulitia umaskini taifa la Watanzania kwa kuwa na wizi wakutisha wa mabillionea.

Nusu karne miaka 50 inatosha kwa ccm kupunzika na tukaangalia upande mwengine wa shillingi,


 
Kama chama na serikali ni kitu kimoja basi CCM waruhusiwe kufanya kampeni kwa kutumia magari ya serikali, na pia magari yote ya serikali yawekwe bendera za CCM.
 
Kama chama na serikali ni kitu kimoja basi CCM waruhusiwe kufanya kampeni kwa kutumia magari ya serikali, na pia magari yote ya serikali yawekwe bendera za CCM.

Nitakufundisha Kwa kutumia mfano wa tajiri mwenye basi la abiria. Mtu awe ni Wananchi na basi ni serikali. Serikali ni mali ya wananchi. Tajiri awe kila baada ya miaka 5 awe anatangaza timu ya kuendesha basi hilo (serikali). Timu ya kuendesha (chama cha siasa) awe ni dereva, kondakta na utingo (rais, mawaziri na watendaji wote). Zijitokeze timu mbalimbali zishindanishwe na timu inayoshinda (chama) inapewa basi kuliendesha. Sasa kutana na basis hilo singida likienda Mwanza. Naulikute limechafuka sana. Itoke lawama kuwa hilo basi linasafirisha abiria likiwa chafu. Ni nani anabebeshwa uzembe huo?
 
Serikali inatakiwa kutekeleza ilani au inatakiwa kujibunia mambo yake? Kama kazi ya serikali ni kutekeleza ilani ya chama tawala, kwa nini vitengwe kama sio kujitetea kwa kuficha ukweli?
 
Kama chama na serikali ni kitu kimoja basi CCM waruhusiwe kufanya kampeni kwa kutumia magari ya serikali, na pia magari yote ya serikali yawekwe bendera za CCM.
Mkuu kwa sasa hivi tunafanyaje?si tunabadirisha plate number tu ila gari na mafuta nivya serikali.
 
Kama chama na serikali ni kitu kimoja basi CCM waruhusiwe kufanya kampeni kwa kutumia magari ya serikali, na pia magari yote ya serikali yawekwe bendera za CCM.
Namuona kinana akiwa mkoani kagera kuzindua miradi iliyo tekelezwa na chama cha mapinduzi kupitia kodi za wadanganyika
 
unajua ccm CHAMA KIKONGWE ( au chama kilichokongoroka ) kinaamini watanzania wa enzi ya uhuru ndio hawahawa wa leo !
 
Back
Top Bottom