Angalia watu wanavyo mkufuru mungu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Angalia watu wanavyo mkufuru mungu

Discussion in 'Jamii Photos' started by Lawkeys, Jun 16, 2010.

 1. Lawkeys

  Lawkeys JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 1,110
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  LUCIFER IS GOD.png JUPETER.png KENNETH QT3.png KENNET C QUT2.png CHUNG QUORT3.png View attachment 11132 View attachment 11131
  VIDOLE PAPA.png Hivi umewahi kutafakari? hivi unadhani hii ni sahii? wahubiri wengi wanaibuka kila kukicha, wanafanya miujiza mikubwa sana. Wengi wanadhani kwa kufanya miujiza tu wanadhihirisha kwamba wana Roho wa Mungu. Isaya 8:20 inatoa kipimo cha roho. Lakini Yohana anatwambia, "zijaribuni hizo roho.....", kwani sio roho zote zinatoka kwa Mungu. Kumbuka maandiko yansema siku za mwisho shetani atafanya miujiza mingi hata ikiwezekana kufanya moto ushuke kutoka juu, hata kuwafanya hata watakatifu kuanguka, kwani anajua wakati wake uliobaki ni mfupi sana.

  Hawa wachungaji, ujumbe wao mkuu ni miujiza,miujiza tuu! hawahubiri watu wafwate sheria za Mungu na wengine wanasema, wahubiri wanahubiri kuhusu sheria za Mungu (10 commandments) wanazuia roho wa Mungu kutenda kazi, na wengine wanasema, "sheria ziligongomelewa msalabani". Soma Mathayo 5:17-18 na Ufunuo 12:14. Mahubiri yao ni ya kujiinua nafsi zao kama vile nao ni Mungu, nafasi ya Yesu haionekani KABISA, utasikia mini na fufua wafu, mimi ndio ninaponya magonjwa yote, MIMI, MIMI, MIMI (Yesu yukawapi). Kuna kiongozi wa DINI MMOJA anavaa kofia yenye ngazi tatu, zinazoonesha mamlaka tatu za kiongozi huyo. Yani, yeye ni mfalme wa Mbinguni, Duniani na Kuzimu. Yaani, inatisha binadamu anapojiinua kujifanya Mungu, onyo;

  I Wathesalonike 2: 3-4<?xml:namespace prefix = o ns = "urn:schemas-microsoft-com:eek:ffice:eek:ffice" /><o:p></o:p>
  Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yoyote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa, yule mtu wa kuasi; mwana wa uhalibifu; yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akajionesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.

  Viongozi hawa wa Dini, wana pesa nyingi na kutembelea Magari ya kifahari, sina hakika kama inatokana na sadaka au la! lakini kuna mitandao ya siri kama FREEMASON wanaofund hizi institutions ili kujenga mazingira ya kumuinua LUCIFER. Nasema, hivi kwasababu nimeona katika video ya muhubiri mmoja mashuhuri (Mmarekani) anahubiri kwa mtindo wa upako na kwa kunena kwa lugha, baadae anonesha HE GOT SYMBOL (alama ya FREEMASON inayo mwakilisha Lucifer) kisha anasema kwa maneno ya kubanabana, "I am together with Lucifer". Wengine wanamtukana hata Mungu.

  Kama wachungaji ndio hivyo, je wengine wamepona? Music industry ndo usiseme, alama nyingi wanazo onesha ni za Kimizimu, wanajitoa kumtumikia lucifer, hebu angalia link hii: Lady Gaga's Bad Romance - The Occult Meaning | The Vigilant Citizen . Tafuta link katika Jamii Forums, LADY GAGA, Beyonce na SASHA FIERCE, occult nk. utaona jinsi wanamuziki wanavyo fanya kazi ya yule mwovu. Kazi kuhamasisha vitendo vya zinaa, ulevi na mara nyingine hata ushoga. Maskini watanzania tunaiga iga tu.Wanamyeleka, utashuhudia alama hizo pia. Makanisa makubwa kuna alama hizo pia, angalia mchoro huo ndani ya Cathedral moja;


  NDANI CATHE3.png

  Lengo sio kumkwaza mtu, ila ni nia yangu ya dhati kwamba tuone jinsi ambavyo shetani anafanya kazi kwa nguvu, dalili kwamba Yesu anarudi. Tujiandae
   
 2. N

  NJEMBA Member

  #2
  Jun 19, 2010
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani ndiyo nafasi ya Miungu watu kuonekana sasa kwani hata wewe ukiamua kuanzisha kanisa utafanikiwa ili mradi utangaze kuwa unamiujiza ya kuponya. Aiu unaombea watu kupata kazi nk. utapata waumini wengi na kuanza kuzichanga kwa sadaka.
  Nilikuwa safarini Mwenzi jana akaja jamaa anahubiri kwenye gari na kusema kanisa lao liko Sanawari na akawa anawakaribisha abiria kuhudhuria ibada zao za maombezi. Cha kushangaza alimalizia kwa kusema ukija kuombewa usisahau mchango wa kiti cha kanisa Sh. 15,000/=, Je hii ni biashara au ni Maombi?
   
 3. M

  Malunde JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 311
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Msingi wa Ukristo ni Kristo mwenyewe. Biblia na tafsiri sahihi ya biblia inatuongoza namna ya kuuishi ukristo, hapo ndipo penye matata.
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Wakristo wenyewe tumekuwa wa miujiza tuu.Huoni jinsi ambavyo watumishi wanajikweza na kujitwalia utukufu(hadi kutumia ving'ora......) na wafuasi walivyo wakali kuwalinda!Miujiza ya kanisani inakuwa advertised kuliko ya waganga wa kienyeji!Watu wanaponywa kwa jina la bwana mkubwa (na sio kwa jina la Yesu kama alivyoagiza)
  Hivi Yesu angaliweka matangazo ya redio na TV kama ilivyo sasa ingekuwaje!
   
 5. T

  Tall JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  1.ndio hivyo tena akili kichwani mwako
  2.shetani mjanja kuliko maelezo,kama alimjaribu yesu,atamshindwaje askofu?
  3.anajua hana muda kabisa.
   
Loading...