Angalia wanaojua maana ya PhD za heshima hawazitumii kama vile walisomea

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
[h=3][/h]

raila.jpg
Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga alirejea nchini mwake akitokea Marekani alikopewa shahada ya heshima ya Udaktari na chuo kikuu cha Florida Agricultural and Mechanical University huko Tallahase. Kutokana na ukio hilo, gazeti la The Daily Nation la Kenya lilipambwa na kichwa cha habari hiki "Applause as 'Dr Odinga' returns. Au shangwe ujio wa 'daktari Odinga'. Wametumia neno daktari kwa uangalifu kwa kuliwekea alama za kufunga na kufungua usemi wakijua kuwa udaktari wa kupewa hata kama ni wa heshima si heshima kuutumia kama baadhi ya viongozi wa Tanzania wanavyofanya hasa rais Jakaya Kikwete. Wanaojua maana ya shahada za heshima wanashangaa sana hasa ikizingatiwa kuwa marehemu baba wa Taifa alikuwa miongoni mwa viongozi waliotunukiwa shahada nyingi za heshima kutoka na mchango wake katika kufikiri kidunia. Hivyo ingekuwa vizuri wanaomshauri rais Kikwete kumwambia aachane na kutambia udaktari wa heshima. Maana hata marais wenzake kama vile Mwai Kibaki, Yoweri Museveni na Paul Kagame wanazo shahada hizi tena nyingi lakini hawajinasibishi nazo.
 
inwezekana hata ukanali wa jeshi alipewa kama anavyopewa phd za heshima, kumbukeni maneno ya NYERERE aliposema bado hajaiva kisiasa asubiri kwanza akue watu hawakumwelewa
 
Kikwete alipewa udaktari baada ya kugundulika kuwa CDM wangempa ugombea u-rais Dk Slaa back in 2010.

Ishu ikawa, CDM wana Dk Slaa, CUF wana Prof Lipumba je CCM wana nani...Mh JK Kikwete??? hapana.....Dk Kikwete.

it was political move basiiiiiiiiiiiiiii....hakuna heshima wala nini, pure politiki kama kawaida ya bongo!!!!!!!!!!!!!
 
JK inferiority complex inamsumbua, ukijumlisha na funga* waliopo kichwani, mambo yanakuwa ziii...
 
te te teh, tanzania si hivyo, ukipewa unaanza kuutumia, weni ni wavivu wa kuutafuta wanataka wa kupewa
 
Kikwete alipewa udaktari baada ya kugundulika kuwa CDM wangempa ugombea u-rais Dk Slaa back in 2010.

Ishu ikawa, CDM wana Dk Slaa, CUF wana Prof Lipumba je CCM wana nani...Mh JK Kikwete??? hapana.....Dk Kikwete.

it was political move basiiiiiiiiiiiiiii....hakuna heshima wala nini, pure politiki kama kawaida ya bongo!!!!!!!!!!!!!

Yaani Likikwete lijinga sana nalo linachekelea tu kuitwa Dr. Ningekuwa mimi nisingekubali kuitwa Dr kwa sababu ya PhD ya heshima. Tuna raisi ZUMBUKUKU MLANGO HUKO HUKU!!!
 
inwezekana hata ukanali wa jeshi alipewa kama anavyopewa phd za heshima, kumbukeni maneno ya NYERERE aliposema bado hajaiva kisiasa asubiri kwanza akue watu hawakumwelewa
Kwani sas hivi haja kua,mbona ana wake wengi na watoto?
 
low minded people always seek for prestige even if it stutpid one. Huyu ni narrow minded ana akili za KIKWERE hamnazo, alikwepa tu kucheza ngoma akawahi shule, lakini alifaa sana kuwa celebrity wa nchi na si rais wa nchi.
 
Hivi JK ameandika vitabu vingapi? Au basi ata academic/ research papers au articles ngapi? Nyerere aliandika vya kutosha, sina uhakika na Mwinyi na Mkapa.

Mwinyi hawezi kuandika article, not that am being disrespectful to the old man lakini anajua anachoweza ndio maana hajawahi kujiita "Dr" japo nae keshatunukiwa PhD za heshima pia.

Nyerere alishapewa doctorate kadhaa - ikiwemo ya kusomea- na uprofessor pia, lakini hakutaka kuitwa kwa title hizo.
 
Hivi JK ameandika vitabu vingapi? Au basi ata academic/ research papers au articles ngapi? Nyerere aliandika vya kutosha, sina uhakika na Mwinyi na Mkapa.
kwani uandishi wa vitabu ni kipimo cha udokta?
 
raila.jpg
Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga alirejea nchini mwake akitokea Marekani alikopewa shahada ya heshima ya Udaktari na chuo kikuu cha Florida Agricultural and Mechanical University huko Tallahase. Kutokana na ukio hilo, gazeti la The Daily Nation la Kenya lilipambwa na kichwa cha habari hiki "Applause as 'Dr Odinga' returns. Au shangwe ujio wa 'daktari Odinga'. Wametumia neno daktari kwa uangalifu kwa kuliwekea alama za kufunga na kufungua usemi wakijua kuwa udaktari wa kupewa hata kama ni wa heshima si heshima kuutumia kama baadhi ya viongozi wa Tanzania wanavyofanya hasa rais Jakaya Kikwete. Wanaojua maana ya shahada za heshima wanashangaa sana hasa ikizingatiwa kuwa marehemu baba wa Taifa alikuwa miongoni mwa viongozi waliotunukiwa shahada nyingi za heshima kutoka na mchango wake katika kufikiri kidunia. Hivyo ingekuwa vizuri wanaomshauri rais Kikwete kumwambia aachane na kutambia udaktari wa heshima. Maana hata marais wenzake kama vile Mwai Kibaki, Yoweri Museveni na Paul Kagame wanazo shahada hizi tena nyingi lakini hawajinasibishi nazo.
Na Dr. Mengi aelezwe!
 
Anna Mkapa pia alipewa doctorate ya heshima na chuo kimoja huko marekani na aliporudi magazeti yakaanza kumwita " DR " hapo nadhani mumewe alimuelimisha kuhusu hizo honoraly degrees na hakuitwa kwa title hiyo tena!! Mkweree yeye kwa vile ni mtu wa misifa basi anaona poa tu kuitwa "DR"!!!!!
 
U-Dr huo ni jamii kutambua mchango wako lkn kwa Wabongo ni title kuliko ubatizo! Wengine hata majina yao halisi wameshaanza kuyasahau? Hata waliokuwa wanafikiria kusoma hawaendi tena maana title wameshazipata! Hapo ndio uone wabongo wanavyozitafuta title hata kwa shule fake...loh!
 
Ni Kweli Mh. Hata jana nilisikia Dr. Reginald Mengi. Dr. Augustine mrema , just shame.

Yani nilishangaa siku moja kumbe mrema naye ni dr khaa juzi juzi si alichukua degree online? Elimu ya tz kweli mufilisi ngojaa nichange hela namie niwe professor king kong watatu.
 
Nchi zetu maskini tabu tupu, huko marekani kuna maprofesa na madokta lakini kwenye utumishi wa kisiasa huitwa kwa majina yao tu, mf. Condoleza Rice hatumii title za kitaaluma japo anazo.
 
U-Dr huo ni jamii kutambua mchango wako lkn kwa Wabongo ni title kuliko ubatizo! Wengine hata majina yao halisi wameshaanza kuyasahau? Hata waliokuwa wanafikiria kusoma hawaendi tena maana title wameshazipata! Hapo ndio uone wabongo wanavyozitafuta title hata kwa shule fake...loh!

Wanitakiani. Suala la title bongo limekuwa kero sasa. Mara utasikia Advocate Nyombi,mara Engineer Manyanya,mara Accountant Gama n.k.

Yaani imekuwa ni fujo na kero tu. Sasa kila mtu atataka kujitambulisha kwa kuanza na "title" zao. Tutaona, Mchorakatuni Masoud,Fundisaa Masawe,Muuzaduka Tarimo,Kondakta Masangu,Dereva Luhanga n.k.
 
Last edited by a moderator:
Hivi ni J.K ndo anataka kuitwa ama vyombo vya habari ndo vinavyomuita hivyo? Ninavyofikiri mimi ni waandishi wa habari ama kwa nidhamu ya uoga, kujipendekeza, ama kutokujua ndo wamezusha hiyo title kutumika hivyo kwa J.K
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom