Angalia uzushi wa DailyNnews. Wameanza tena... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Angalia uzushi wa DailyNnews. Wameanza tena...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Profesy, Oct 7, 2010.

 1. Profesy

  Profesy Verified User

  #1
  Oct 7, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wakuu hivi hawa daily news wanashida gani na slaa? Someni hii story.

  2010_10_06Daily News_2.JPG
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,711
  Trophy Points: 280
  Kwanza kabisa mwandishi wa hiyo makala haielewi sheria ya ndoa ya nchi hii na anajikandia mwenyewe kwa kuonyesha jinsi ambavyo alivyo mbumbumbu wa sheria tajwa.

  Chini ya sheria ya ndoa ya nchi hii, Ndoa yahesabika kuwa ni ndoa au kutokuwa ndoa kutokana na matendo ya wanandoa hao katika miaka miwili ya mfululizo ya wakati wowote ule. Huwezi kusema huyu ni mke wangu au mume wangu hata kama mlifunga ndoa kanisani kama hamuishi kama mume na mke katika miaka miwili mfululizo. Taarifa nilizonazo, mtaliki wa Josephine sasa hivi amewekwa kimada na lijimama moja linalogombea jimbo moja hapo Dar kupitia CCM. Sasa huyu jamaa atasemaje ana mke wakati yeye mwenyewe alikwisha kuivunja ndoa hiyo kutokana na matendo yake ya uzinifu?

  Kuhusu ushiriki wa CCM kwenye sakata hili haukwepeki hata kidogo. Mwaka 1995, CCM hiyo hiyo ilimzulia Mrema kashfa inayofanana na hiyo ulipokwisha uchaguzi na CCM kufanikisha upuuzi wake suala hilo likafa kimyakimya. Magazeti ya Uhuru na Daily News ambayo CCM inasimamia yameona kwenye suala hili wamepata kivuno wakati wanatuthibitishia ya kuwa Dr. Slaa atakapokuwa Rais basi aanze na hilo Daily News kusafisha wapambe wa CCM ambao hawana maadili. JK ana watoto wangapi wa nje na familia ngapi amezivunja na hakuna anayekereketwa humo CCM, Uhuru au Daily News. Hivi mbona hamtaki kuongelea ni umeme upi ambao mara kwa mara unamporomosha JK toka jukwaani? Msifikiri tukikaa kimya basi sisi ni wajinga ila tunaona hayo ni masuala binafsi tu na ya kuwa atajijua yeye na Muumba wake.

  Kuhusu suala la "integrity" ambalo mwishoni mwandishi ameliongelea hivi maadili ni kwenye ndoa tu? JK anavyoongoza kwa wimbi la wizi wa mali ya umma hiyo siyo hoja ya kumkataa ya "integrity"? Hivi mwandishi huyu mbona anatudharau watanzania hivyo na kutona hatuna akili?

  Lakini tarehe 31 Oktoba tutamwonyesha ya kuwa sisi nasi zimo ingawaje hatuvumi....................
   
 3. Profesy

  Profesy Verified User

  #3
  Oct 7, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  very good.
   
 4. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Watawala wako hoi na wanatapatapa, bahati nzuri Watanzania hatudanganyiki tena na upuuzi wao. Mbona nasikia Mama Mkapa alikuwa mke wa Basil Mramba?
   
 5. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #5
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  kabla ya kulalamika sana au kumchambua mwandishi kama huyo inabidi umchunguze kwanza maisha yake, hakuna sababu ya kupoteza mda kumjadili mwehu, inawezeka ameshawahi kuugua au kwenye ukoo wao kuna hako kagonjwa, tafuta historia yake ya maisha.
   
 6. Profesy

  Profesy Verified User

  #6
  Oct 7, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  alafu sijui kama umegundua lakini siku hizi DAILY NEWS wanaweka only bad stories kuhusu chadema. Campaigns kabla ya juzi sijaona waki cover.
   
 7. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  .....mwandishi alipokuwa high school aliwahi kupora girfriend wa classmate wake kwa kumlaghai wakati wa likizo. watu wote pale shuleni walikuwa wakijua boyfriend wa yule demu ni best friend wa sadiki so sijui ni njaa na ujinga wa aina gani leo anauongelea. wanafunzi wengi wakamtenga kutokana na ushenzi huo.
   
 8. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  hawa daily news si ndo walewale wafa maji hawaachi kutapatapa
   
 9. mdoe

  mdoe JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 436
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wacha waandike hizo mambo coz its the only weapon they have against dr. Slaa. Mbona hatusemi ya kikwete? tuwaache watapetape. ndo dalili za wafa maji.
   
 10. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Hivi ikatokea CHADEMA/Slaa akaingia ikulu jamaa naona watawahi wenyewe ubungo asubuuhi na familia zao kurudi makwao, hawatangoja.....
   
 11. LeopoldByongje

  LeopoldByongje JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2010
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 373
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Suala hili ilipaswa liwe la kibinafsi na si la kitaifa. Inabidi tuangalie masuala yanayohusu taifa na ndiyo tuyajadili. Lakini kwa vile Mheshimiwa Silaa anataka kuongoza nchi ni budi awe mwangalifu katika nyendo zake binafsi asije kujichanganya na kulichanganya taifa.

  Mwalimu Nyerere alitutahadhalisha kuwa IKULU ni mahala patakatifu. Si pahala pa kuficha wahuni au pango la walanguzi.Hapo ndipo hoja ya uwajibikaji inaibuliwa. Hapa hoja ni je mtu huyu huwa hafanyi utafiti au uchunguzi kabla ya kufanya maamuzi? Je hana washauri wazuri?

  Maisha yake binafsi iwapo yatajaa utata na akawa haeleweki au atabiriki si ajabu watu wakakosa imani naye. Kumbuka kulikuwa na mjadala hapa janvini watu wakichambua maisha ya Dr Silaa hususan kutokuwa na makazi yanayoeleweka. Ziliibuliwa taarifa kuwa huyu Mheshimiwa anaishi Guest house ukipenda Hotel. Hivi ni viashiria kuhusu aiba na tasiwira ya maisha ya kiongozi wetu mtarajiwa.

  Hapa inabidi watu waanze kuhoji kulikoni Mtu ambaye anatushawishi tumkabidhi nchi je anaaminika na ni mkweli? Je anaweza kulinda kwa dhati masilahi ya wengi? Je anaweza kusimamia haki? Je anachukizwa na dhuluma? Na mambo kama hayo.

  Katika Biblia kuna hadithi ya Mfalme aliyemtamani na hatimaye kutembea na mke wa jemadari wake. Jemadari huyo akiwa vitani huku nyuma mfalme anajinafasi na mkewe hadi yule mama kapata uja uzito.

  Baada ya kugunda hilo Mfalme akamuita haraka jemadari arejee nyumbani. Alipofika akamwambia apumzike japo kwa siku chache. Jemadari alitii lakini hakukubali kulala ndani nyumbani kwake kwa vile aliamini haikuwa vyema yeye astarehe wakati wapiganaji wenzake wanakufa huko vitani. Hivyo hakukutana kimwili na mkewe. Mfalme alipobaini kuwa mtego aliouweka haukunasa alimrejesha mstari wa mbele na akafanya kila liwezekanalo jemadari huyo akauawa.

  Hapa tunaoneshwa dhuluma kwa kutumia madaraka. Iwapo mgombea huyo ana ugonjwa huo si ajabu akiingia ikulu akaendeleza tabia hiyo. Kwanza hakuhojiwa wakati wa Kampeini kuhusu tabia hiyo ili aiache. Pili pale ambapo wanaotaka kuhoji iwe kwa nia njeam au mbaya wanibuka watu kumtetea asisemwe au asihojiwe kwa sababu chungu nzima.

  Lakini tukumbuke kuwa Mheshimiwa Silaa pia ana rekodi ya kutokuwa makini na masuala ya Unyumba na Nyumba. Zipo taarifa kuwa alizaa na mwanamke mwingine watoto wawili lakini huyo Mzazi mwenzie eti hawakuwa wachumba!!! Nasema taarifa kama hizi zinatuonesha kuwa pamoja na uzuri na mvuto nk. mambo haya yanaweza kutia doa machoni mwa wapiga kura. Wanasema mchelea mwana kulia ulia mwenyewe. Tusilee ugonjwa. Kwa wapenzi wa Dr. Silaa mpeni ushauri ajirekebishe Muda bado anao.

  Kazi kwenu

  :mad::smow:
   
 12. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwanza gazeti lao la kiingereza, na serikali ya chichiemu iliwanyima fursa watanzania ya shule hivyo wasomaji wake ni kiduchuuuuuuuuu! tena zaid labda watu wa tenda, watafutaji wa kazi, ,,,.............., n.k
   
 13. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  CCM walikuja na iyo hoja ili tuwe na divided attention vs Slaa.
  Imekula kwao bse hii scenario ni kama ya Mkapa tuu.
   
 14. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ukiona mtu anauma sikio kama Tyson au anarusha ngumi chini ya mkanda basi wenye hikma wanajua tu tayari..khalas.
   
 15. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #15
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa inabidi kabla ya kujibu hoja za hawa jamaa inabidi kwanza tujiulize kama wapo sawasawa!
   
 16. Profesy

  Profesy Verified User

  #16
  Oct 7, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wewe umeona Sarkozy akichemsha na mambo yake ya kizinzi? Kwani JK hana wanawake wa kando ambayo sio wa kwake? Au hana watoto (bastards)? Kwanza nasikia Vicky Kamata ambaye anagombania Vitii Maalum Geita alikuaga ana tembea naye. Tuone kama hata shinda.

  Swala kubwa hapa ni kwamba Daily News inatakiwa iwe inatuelezea sera za wagombea na sio story hadharani na za udaku. Yani ghafla siku hizi watu wanajifanya malaika ambayo hawajawahi kutenda dhambi. Kwani ukienda kuomba kazi wanakuomba utangaze unamabinti au wanaume wangapi umelala nao kwenye CV? THINK BEFORE YOU TALK!!!:hand:
   
 17. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  yAAANI KWISHA HABARI YAKEEEEEE
   
 18. I

  ICHONDI JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Hivi si hawa hawa Daily News walisema Slaa hatakuwa raisi, tena wakasema kwa kujiamini. Sasa wana wasiwasi gani kuwa ataingia ikulu akiwa mchafu na Josephine kama fist lady akiwa na pete mbili moja ya mahimbo na nyingine ya Slaa.

  Kweli kama huu ndio uandishi wa habari, nchi imekwisha, hivi mtu utaandikaje utumbo kama huo na kuitetea CCM sasa sijui makala inahusu nini as such, mara Pope, mara ccm mara sijui uchafu gani jeee. Na je si kesi iko mahakamani? kuanza kumhukumu Slaa kwa kesi iliyopo mahakamani kuwa ni mwizi, si kuingilia uhuru wa mahakama? Jaji mkuu uko wapi
   
 19. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Tafadhari tueleze na upande wa pili wa shilimgi ukoje??
   
 20. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #20
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280

  Watasema ya kikwete uchaguzi ukiisha atakapo kuwa anaongoza kambi ya upinzani.
   
Loading...