Angalia umri wako upo sahihi? Umekosea? Unahitaji kujirekebisha?

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,900
6,657
20 - 25 = Kama ni kielimu hujafikia malengo yako, sitisha mara moja tafuta kazi/biashara ya kufanya, pigana kufa na kupona ili kama vipi urudi shule kwa pesa yako.

25 - 30 = Hakikisha uwe na angalau KAZI RASMI kama umeajiriwa au umejiajiri au una shughuli yeyote ya kukuingizia kipato.

30 - 35 = Uwe na angalau kama sio nyumba basi kiwanja, tena ujitahidi uwe umeoa/umeolewa. Ni vema ukiwa na familia, kwa maana ya kuwa na watoto kama Mungu kakuwezesha.

35 - 40 = Ni wakati kiwanja kiwe kimejengwa na kama ni tayari basi nenda step nyingine ya kumiliki kama ni Gari au kuongeza nyumba na hakikisha vinaenda sambamba na ongezeko la familia. Hapa inabidi upambane sana kuweka misingi.

40 - 45 = Ni umri wa masahihisho, kama hukuwahi kununua kiwanja, kama hukujenga basi hapa pambana afe kipa afe beki, ni umri wa masahihisho. Ila kwa wale ambao wameenda vizuri huko nyuma basi hapa watoto wapo kwenye level tofauti za elimu, kwahiyo ni muda wa kuwawekea malengo ya kimasomo watoto wao.

45 - 50 = Kwa yule ambae hakukosea huko nyuma basi umri huu ni wa kuanza kuwatengenezea mazingira watoto wako, kama ni shughuli zako ni kuanza kuwahusisha, huku wewe ukijiweka pembeni taratibu na kuangalia fursa za umri wako. Lakini kwa wale waliokosea hapa ni kupitia zile hatua za 35 - 40.

50 - 60 = Ni kujiandaa na maisha mapya ya kustaafu au kujiweka mbali na kazi zinazotumia nguvu au akili nyingi

60 - 70 = Kula matunda yako huku ukiangalia misingi ya wanao inaendaje.

70 - 80 = Kula matunda

80 - nk = Umri wa kusubiria geti lifunguke uingie ndani
 
vitisho vyote vya nn wakati sisi ni wapita njia hapa duniani jamani
1619691106096.png
 
Na ukiona umetusua mapene ya uhakika toka 20s na ukayalinda mpaka 35 jua ww tajiri
 
Hizi nyuzi za ku compare age vs achievements ndo zinafanya wadogo zetu wafikirie kunywa sumu kutokana na msongo wa mawazo..maisha hayana constant formula kwa kila mtu,ila tuu tupambane tunavyoweza bila kuwa limited na umri
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom