Angalia picha za Sherehe ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Angalia picha za Sherehe ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fatal5, Apr 27, 2012.

 1. Fatal5

  Fatal5 Senior Member

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kwa nini wa Tanganyika tumefanya sherehe za miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar bila ya wa Zanzibari kushiriki pale uwanja wa Taifa na Ikulu

  Rais wa Zanzibar hakuwepo katika sherehe hizo wala makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar hakuja

  Ni Wa Zanzibari 10 tu peke yao kutoka CCM ndio walikuwepo pale uwanja wa Taifa na ikulu.

  RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA WANANCHI MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 48 YA MUUNGANO  [​IMG]
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akipunga mkono kusalimia wananchi wakati akiingia Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
  WAZANZIBARI 10 TU NDIO WAPO HAPO KATIKA PICHA YA CHINI HIYO

  [​IMG]
  Baadhi ya Viongozi wa Kiserikali wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria sherehe hizo katika Uwanja wa Uhuru, wakisimama wakati wa kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  [​IMG]
  Amir Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akikagua gwaride wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar, zilizofanyika leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo katika sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
  [​IMG]
  Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWT, kikipita mbele ya Jukwaa Kuu kwa mwendo wa haraka na kutoa heshima kwa mgeni rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete.
  [​IMG]
  Kikosi cha Wanamaji kikitoa heshima mbele ya Jukwaa Kuu.
  [​IMG]
  Kikosi cha FFU kikionyesha uwezo wa kulichapa gwaride kwa mwendo wa haraka.
  [​IMG]
  Kikosi cha JWT katika mwendo wa haraka.
  [​IMG]
  Kikosi cha Magereza katika mwendo wa haraka.
  [​IMG]
  Watoto wa shule mbalimbali za msingi wanaounda kikundi cha alaiki, wakionyesha manjonjo ya michezo na maumbo mbalimbali wakati wa sherehe hizo leo.
  [​IMG]
  Watoto wa shule mbalimbali za msingi wanaounda kikundi cha alaiki, wakionyesha manjonjo ya mchezo wa Sarakasi.
  [​IMG]
  Watoto wa shule mbalimbali za msingi wanaounda kikundi cha Halaiki wakionyesha manjonjo ya na kupandisha Bendera ya Taifa.
  [​IMG]
  Kikundi cha Sanaa cha JKT Oljoro, kikionyesha umahiri wake wa kuimba na kucheza 'Kiduku' wakati wa sherehe hizo.
  [​IMG]
  Baadhi wa wananchi waliofika kushuhudia sherehe hizo IKULU
  [​IMG]

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanasanii kutoka katika Chuo Cha mafunzo ya Polisi, Moshi wakati wa hafla ya sherehe za miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyofanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.
  [​IMG]
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanasanii kutoka katika kikundi cha JKT Oljoro, Arusha wakati wa hafla ya sherehe za miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyofanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.
  [​IMG]
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsalimia Katibu mkuu kiongozi mstaafu Mzee Timothy Apiyo wakati wa hafla ya sherehe za miaka 48 ya Muungano iliyofanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.
  [​IMG]
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Monsinyori Julian Kangalawe wakati wa halfa ya muungano ikulu jana jioni
  [​IMG]
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mmoja wa Wazee waliohudhuria hafla ya sherehe za Muungano iliyofanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni(picha na Freddy Maro).

  SASA HUU NI MUUNGANO GANI UNAOSHEREHEKEWA NA UPANDE MMOJA TU WAKATI NCHI ZILIZOUNGANA NI 2 ?? NAOMBA JIBU WATANGANYIKA WENZANGU??


   
 2. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,988
  Likes Received: 3,737
  Trophy Points: 280
  na mimi na-echo swali lako zuri.
  linahitaji majibu kutoka kwa wale protagonists wa muungano kwa structure yake ya sasa..
   
 3. S

  Silent Burner Member

  #3
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Gwaride lilifana saana. Inaonekana vijana wetu ni wakakamavu kiukweli.
   
 4. Skp2ole

  Skp2ole Senior Member

  #4
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  utata mtupu huo na mm nadhani nibora kila mtu ale hamsini zake
   
Loading...