Angalia mwongozo wa kanuni uliyowachinja Wapinzani

Frey Cosseny

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
1,984
1,405
WALE WANAOLALAMIKA WAMEONEWA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA WAMEZINGATIA HAYA?
1 . Kama majina yake yatatofautiana kati ya majina aliyojaza kwenye fomu na majina aliyojiandikisha kwenye daftari. Angalia kanuni ya 13 (e) Uk. 152

2. Endapo mdhamini hataandika majina matatu na cheo ktk vyama. Angalia mwongozo wa uchaguzi kipengele cha 14.2 (d) Uk. 10-11

3. Jina alilojaza wakati anachukua fomu lifanane na lililopo kwenye fomu ( dispatch book vs forms). Angalia kanuni ya 17 (1) Uk. 153

4. Mgombea arejeshe fomu mwenyewe na kusaini. Angalia kanuni ya 17 (2) Uk. 153

5. Majina ya mdhaminiwa yafanane na ya mgombea yaliyojazwa kwenye fomu. Angalia mwongozo wa uchaguzi kipengele cha 14.2 (a-d) Uk. 10-11

6. Fomu ya kiapo iwe halisi iliyotolewa na msimamizi msaidizi na ishuhudiwe na msimamizi msaidizi ngaz husuka. Angalia kanuni ya 16 (e) Uk. 152

7. Fomu zijazwe na mhusika lazima ziwe zimesainiwa. Angalia mwongozo wa uchaguzi kipengele cha 14.2 (e&f) Uk. 10-11

8. Fomu zishuhudiwe na ngazi ya chini ya chama itakayobainishwa na chama. Angalia mwongozo wa uchaguzi kipengele cha 14.1 & 14.2 (a) Uk. 10-11

9. Ambaye hajajiandikisha hana sifa ya kuwa mgombea. Angalia kanuni ya 13 (e)Uk. 152, ilinganishe na Kanuni ya 16 (d) Uk. 152 na Kanuni ya 14 (a) Uk. 152

10. Aliyejiandikisha mara mbili atakuwa amepoteza sifa ya kugombea au kupiga kura. Angalia kanuni ya 14 (b)Uk. 152

11. Lazima aeleze shughuli halali inayomwingizia kipato na endapo atabainika kudanganya atakuwa amepoteza sifa. Angalia kanuni ya 15 (d)Uk. 152

12. Atakayeomba nafasi zaidi ya moja kwenye fomu moja atakuwa amepoteza sifa. Angalia kanuni ya 17 (1) & (5) Uk. 152-153

13. Nafasi anayoomba ionekane mpaka kwenye fomu ya kiapo. Angalia kanuni ya 17 (1)Uk. 153 isome sambamba na Kanuni ya 16 (e) Uk. 153

14. Fomu zijazwe kwa ukamilifu. Angalia kanuni ya 17 (2) Uk. 153

15. Eneo la uraia ajaze uraia siyo nchi mfano: Mtanzania na siyo Tanzania. Angalia kanuni ya 17 (1-5) Uk. 153-154

16. Usahihi wa maeneo kwa mujibu wa GN mfano chankobe akiandika chakobe atakuwa amepoteza sifa maana eneo hilo litakuwa halipo ktk GN. Angalia kanuni ya 15 (e) Uk. 152 & Kanuni ya 17 (1-5) Uk. 153-154.

17. Mwombaji aeleze anaomba nafasi ipi na wapi mfano nafasi anayoomba mwenyekiti wa Kijiji cha Kagera vinginevyo atakuwa amepoteza sifa. Angalia kanuni ya 15 (e) Uk. 152

18. Fomu ijazwe taarifa inayohitajika tu, kuwepo kwa maandishi au michoro isiyohitajika hilo ni kosa. Angalia kanuni ya 17 (5) Uk. 154

19. Mgombea arejeshe fomu zote mbili kinyume na hapo hana sifa. Angalia kanuni ya 17 (2), (3) na (4) Uk. 153-154

20. Kama mgombea ameomba nafasi mbili unaweza kumteua nafasi moja. Angalia kanuni ya 17 (1)& (5) Uk. 153-154

21. Mgombea akiwa na ajira, wadhifa au uteuzi wowote katika mihimili ya Serikali atakuwa amepoteza sifa za kuchaguliwa. Anagalia kanuni ya 16 (f)Uk. 153

22. Ikiwa Mgombea alichukua fomu na hakurejesha atakuwa amepoteza sifa za kuchaguliwa. Angalia Kanuni ya 17 (2), (3) na (4)

23. Mgombea ambaye hatadhaminiwa na ngazi ya chini ya Chama chakeatakuwa amepoteza sifa za kuchaguliwa. Angalia mwongozo wa uchaguzi sehemu 14.1 na 14.2 (a)

Kabla ya kulalamika kukatwa majina,Jiridhisheni kwa kila hatua kama mmekidhi vigezo na masharti sio kulalama....
 
Kwa hiyo ni wapinzani tu ndiyo wamekosea wale wa CCM wao walielewa vyema??
CCM waliwapa wagombea wao semina elekezi jinsi ya kujaza wapinzani wakabaki mitandaoni kulalama sasa wamejaza vidole juu wamekosea wanalia .

Panueni akili sio vidole

State agent
Ukiacha Semina Elekezi, Ccm walikua na wanasheria kabisa kuratibu zoezi kwa wagombea wasikosee kujaza
 
Ujinga wa ccm na viongozi wao bana unatia aibu!! Hivi inawezakanaje wagombea wote wa vyama pinzani kukosea fomu?? Kwamba ccm wao wako Safi wote Nchi nzima??. Kweli Nape alikuwa kichwa Sana na aliyetumia akili nyingi kuudhoofisha upinzan kwa akili nyingi kuliko nguvu za haya matahira😎
 
Ukiacha Semina Elekezi, Ccm walikua na wanasheria kabisa kuratibu zoezi kwa wagombea wasikosee kujaza

...sawa, inamaana hawa wapinzani hawakuwa na uratibu kwenye zoezi hili!?

Wagombea wao waliachwa kama watoto wa kuku? Kwamba hawawezi kujaza majina yao kiukamilifu!? Miaka yote hizi kasoro zilikuwepo lakini si za awamu hii ambayo haina mawaa

Wasimamizi (watendaji kata) ni wa kutiliwa sana shaka kwenye huu mtanziko.
 
Watu wote hawa wawe wajinga kiasi hiko? Kama ww umeweza kugundua basi hata wao waligundua mapema sana,
I think ni time ya kufuta vyama vingi kibaki kimoja tu,
 
Yote 9, kumi mwisho wa ubaya ni aibu,ccm hampishani na yule jambazi msalabani alie mwambia Yesu kama wewe ni mwana wa Mungu jiokoe mwenyewe akasahau kuwa yeye ndo alipaswa aokolewe kupitia Yeye mwisho wa siku aibu ilibaki kwake.
 
KWA HIYO MIAKA YOOTE UCHAGUZI WA SEREKALI ZA MITAA WAPINZANI WASIKOSEE KUJAZA FOMU ILA UTAWALA HUU TU NDIO WAPINZANI WAKOSEE WOTE KUJAZA FOMU.
HII HAIINGII AKILINI HATA KIDOGO
Vipengele vimebadilika Mimi na usomi Wangu tu yanipasa kutulia kuelewa vifungo hivyo vipi layman.Pia mbona Wa ccm figisu hamna.
Ilikuwa ni jukumu la wasimamizi kutoa semina elekezi kwa wagombea wote ili wananchi wapate chaguo lao
 
Watu wote hawa wawe wajinga kiasi hiko? Kama ww umeweza kugundua basi hata wao waligundua mapema sana,
I think ni time ya kufuta vyama vingi kibaki kimoja tu,
Hakutokuwwepo na maendeleo pia wanaogopa kunyimwa misaada kama wakivifuta
 
WALE WANAOLALAMIKA WAMEONEWA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA WAMEZINGATIA HAYA?
1 . Kama majina yake yatatofautiana kati ya majina aliyojaza kwenye fomu na majina aliyojiandikisha kwenye daftari. Angalia kanuni ya 13 (e) Uk. 152

2. Endapo mdhamini hataandika majina matatu na cheo ktk vyama. Angalia mwongozo wa uchaguzi kipengele cha 14.2 (d) Uk. 10-11

3. Jina alilojaza wakati anachukua fomu lifanane na lililopo kwenye fomu ( dispatch book vs forms). Angalia kanuni ya 17 (1) Uk. 153

4. Mgombea arejeshe fomu mwenyewe na kusaini. Angalia kanuni ya 17 (2) Uk. 153

5. Majina ya mdhaminiwa yafanane na ya mgombea yaliyojazwa kwenye fomu. Angalia mwongozo wa uchaguzi kipengele cha 14.2 (a-d) Uk. 10-11

6. Fomu ya kiapo iwe halisi iliyotolewa na msimamizi msaidizi na ishuhudiwe na msimamizi msaidizi ngaz husuka. Angalia kanuni ya 16 (e) Uk. 152

7. Fomu zijazwe na mhusika lazima ziwe zimesainiwa. Angalia mwongozo wa uchaguzi kipengele cha 14.2 (e&f) Uk. 10-11

8. Fomu zishuhudiwe na ngazi ya chini ya chama itakayobainishwa na chama. Angalia mwongozo wa uchaguzi kipengele cha 14.1 & 14.2 (a) Uk. 10-11

9. Ambaye hajajiandikisha hana sifa ya kuwa mgombea. Angalia kanuni ya 13 (e)Uk. 152, ilinganishe na Kanuni ya 16 (d) Uk. 152 na Kanuni ya 14 (a) Uk. 152

10. Aliyejiandikisha mara mbili atakuwa amepoteza sifa ya kugombea au kupiga kura. Angalia kanuni ya 14 (b)Uk. 152

11. Lazima aeleze shughuli halali inayomwingizia kipato na endapo atabainika kudanganya atakuwa amepoteza sifa. Angalia kanuni ya 15 (d)Uk. 152

12. Atakayeomba nafasi zaidi ya moja kwenye fomu moja atakuwa amepoteza sifa. Angalia kanuni ya 17 (1) & (5) Uk. 152-153

13. Nafasi anayoomba ionekane mpaka kwenye fomu ya kiapo. Angalia kanuni ya 17 (1)Uk. 153 isome sambamba na Kanuni ya 16 (e) Uk. 153

14. Fomu zijazwe kwa ukamilifu. Angalia kanuni ya 17 (2) Uk. 153

15. Eneo la uraia ajaze uraia siyo nchi mfano: Mtanzania na siyo Tanzania. Angalia kanuni ya 17 (1-5) Uk. 153-154

16. Usahihi wa maeneo kwa mujibu wa GN mfano chankobe akiandika chakobe atakuwa amepoteza sifa maana eneo hilo litakuwa halipo ktk GN. Angalia kanuni ya 15 (e) Uk. 152 & Kanuni ya 17 (1-5) Uk. 153-154.

17. Mwombaji aeleze anaomba nafasi ipi na wapi mfano nafasi anayoomba mwenyekiti wa Kijiji cha Kagera vinginevyo atakuwa amepoteza sifa. Angalia kanuni ya 15 (e) Uk. 152

18. Fomu ijazwe taarifa inayohitajika tu, kuwepo kwa maandishi au michoro isiyohitajika hilo ni kosa. Angalia kanuni ya 17 (5) Uk. 154

19. Mgombea arejeshe fomu zote mbili kinyume na hapo hana sifa. Angalia kanuni ya 17 (2), (3) na (4) Uk. 153-154

20. Kama mgombea ameomba nafasi mbili unaweza kumteua nafasi moja. Angalia kanuni ya 17 (1)& (5) Uk. 153-154

21. Mgombea akiwa na ajira, wadhifa au uteuzi wowote katika mihimili ya Serikali atakuwa amepoteza sifa za kuchaguliwa. Anagalia kanuni ya 16 (f)Uk. 153

22. Ikiwa Mgombea alichukua fomu na hakurejesha atakuwa amepoteza sifa za kuchaguliwa. Angalia Kanuni ya 17 (2), (3) na (4)

23. Mgombea ambaye hatadhaminiwa na ngazi ya chini ya Chama chakeatakuwa amepoteza sifa za kuchaguliwa. Angalia mwongozo wa uchaguzi sehemu 14.1 na 14.2 (a)

Kabla ya kulalamika kukatwa majina,Jiridhisheni kwa kila hatua kama mmekidhi vigezo na masharti sio kulalama....
Badala usikitike wewe unafurahia inaonyesha ni jinsi gani watanzania bado hatujaijua maana ya democracy
Kama mnadhani kuwa sauti za wapinzani hazina mchango wowote katika maendeleo ya nchi mnajidanganya
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom