Angalia mfano wa jinsi rada za Syria zimekua zikizimwa na jeshi la Israel

ze kokuyo

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
7,414
9,556
Tumeshuhudia jeshi la Israel likifanya mashambulizi kadhaa ndani ya nchi ya Syria katika operation tofauti tofauti kama vile kuharibu silaha za zinazohofiwa kusafirishwa kwa Hezbollah, kuharibu kinu cha nyuklia cha Syria mwaka 2007(operation Orchard), nk.

Katika operesheni hizo tumeshuhudia mara nyingi jeshi la Syria likitoa taarifa kwamba limefanikiwa kudungua ndege za Israel na baadae taarifa hizo kukanushwa na jeshi la Israel (IDF) kwamba hakuna ndege yao hata moja iliyopata matatizo.

Pia tumeshuhudia jeshi la anga la Syria kurushia makombora mengi ndege za Israel bila mafanikio ya kuzitungua, huku ndege hizo zikiwa kwenye operation zake kadhaa.

Video hii inaelezea jinsi mifumo ya Israel inavyoweza kuJam rada za adui au kuzipa signal za uongo na kuona kwamba wamefanikiwa kutungua ndege zao kumbe ni kinyume chake.
Pia inaelezea namna ambavyo mifumo hiyo imekua ikielekeza makombora hayo mahali pengine kabisa na zilipo ndege zao kama tulivyoshudia miezi kadhaa iliyopita makombora ya kutungulia ndege ya Syria yakirushwa kwa wingi bila mafanikio yoyote ya kutungua ndege za jeshi la Israel.

Hela wanayotumia Israel na USA kujikinga na sijuwi Syria, Lebanon, Iran na wengine ingetosha kuanzisha na kuboresha maisha ya raia wa taifa la Palestine, kuboresha maisha ya wa Israel na kutosha kufanya Dunia iwe na amani zaidi..Binadamu tunapenda sana vita, yawezekana kuna wanaofaidi sana sana na haya mambo ya silaha, si bure..
 
Mkuu biashara ya silaha ni biashara yenye faida ya mabilioni ya dola. Sasa bila vita hizo silaha zitauzika vipi?!
Nadhani mkuu izzo anaweza kulielezea hili kiundani zaidi
 
Tanzania MTU akisema fake news bad idea usimshangae tumezoea kutumia manati kuwinda ndege na makombeo kurusha makombora ya kufukuzia ndege kwenye mpunga

Mtoa mada makala yako itakuwa ngumu kumeza
MTU mweusi yuko behind tecknohama siku nyingne ukiandika ngosha bashite kaanza kilimo cha mpunga pale jangwani utaeleweka sana maana utakuwa umeangukia kwenye mazingira na utamaduni wa mtanzania
 
Mkuu biashara ya silaha ni biashara yenye faida ya mabilioni ya dola. Sasa bila vita hizo silaha zitauzika vipi?!
Nadhani mkuu izzo anaweza kulielezea hili kiundani zaidi
Hela wanayotumia Israel na USA kujikinga na sijuwi Syria, Lebanon, Iran na wengine ingetosha kuanzisha na kuboresha maisha ya raia wa taifa la Palestine, kuboresha maisha ya wa Israel na kutosha kufanya Dunia iwe na amani zaidi..Binadamu tunapenda sana vita, yawezekana kuna wanaofaidi sana sana na haya mambo ya silaha, si bure..
GDP ya Dunia ni $74.15 trillion USD mpaka 78.28 trillion kwa mwaka lakini fedha yote unayoiona hapo 45% inakwenda kwenye Ulinzi na Usalama pekee zinazobaki 55% ndio zinagawanywa kwenye vitu vingine
 
Fakes news ama ni uwongo mtupu... Why Israel are they using Lebanon airspace to attack Syria.. Kama wanaume kweli waingie bac Syria airspace...kajipange upya uje na uzi wa maana sio ushabiki maandazi kama wa profesa lipumba
Air strike on Damascus military complex shows Syrian Air Defense can do nothing against Israeli Electronic Warfare
The Silent Strike
The Aviationist » Operation Orchard
https://www.google.com/amp/s/amp.cn...dleeast/israel-jets-syria-strikes/index. html
 
Fakes news ama ni uwongo mtupu... Why Israel are they using Lebanon airspace to attack Syria.. Kama wanaume kweli waingie bac Syria airspace...kajipange upya uje na uzi wa maana sio ushabiki maandazi kama wa profesa lipumba

Nilitegemea majib haya! Uelewa wetu mdogo sana kwenye tekinolojia. Ni sawa ndo kiwango chetu cha kutathmini mambo
 
Tanzania MTU akisema fake news bad idea usimshangae tumezoea kutumia manati kuwinda ndege na makombeo kurusha makombora ya kufukuzia ndege kwenye mpunga. Mtoa mada makala yako itakuwa ngumu kumeza. MTU mweusi yuko behind tecknohama siku nyingne ukiandika ngosha bashite kaanza kilimo cha mpunga pale jangwani utaeleweka sana maana utakuwa umeangukia kwenye mazingira na utamaduni wa mtanzania.

Umesema vema sana sina cha kuongeza
 
Tumeshuhudia jeshi la Israel likifanya mashambulizi kadhaa ndani ya nchi ya Syria katika operation tofauti tofauti kama vile kuharibu silaha za zinazohofiwa kusafirishwa kwa Hezbollah, kuharibu kinu cha nyuklia cha Syria mwaka 2007(operation Orchard), nk.

Katika operesheni hizo tumeshuhudia mara nyingi jeshi la Syria likitoa taarifa kwamba limefanikiwa kudungua ndege za Israel na baadae taarifa hizo kukanushwa na jeshi la Israel (IDF) kwamba hakuna ndege yao hata moja iliyopata matatizo.

Pia tumeshuhudia jeshi la anga la Syria kurushia makombora mengi ndege za Israel bila mafanikio ya kuzitungua, huku ndege hizo zikiwa kwenye operation zake kadhaa.

Video hii inaelezea jinsi mifumo ya Israel inavyoweza kuJam rada za adui au kuzipa signal za uongo na kuona kwamba wamefanikiwa kutungua ndege zao kumbe ni kinyume chake.
Pia inaelezea namna ambavyo mifumo hiyo imekua ikielekeza makombora hayo mahali pengine kabisa na zilipo ndege zao kama tulivyoshudia miezi kadhaa iliyopita makombora ya kutungulia ndege ya Syria yakirushwa kwa wingi bila mafanikio yoyote ya kutungua ndege za jeshi la Israel.

hizi mambo nazipenda sana daah
 
Back
Top Bottom