Angalia kiungo wa Everton alivyovunja mguu, aliyemvunja aangua kilio.

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,145
13,216





Kiungo James McCarthy wa Everton sasa atakaa nje na kuukosa msimu wote huh baada ya kuvunjika mifupa miwili ya mguu wake.

McCarthy amevunjika wakati timu yake ikiivaa Wes Brom na Solomon Rondon ndiye aliyemvunja mguu.

Rondon alikuwa akijaribu kupiga mpira lakini akaukuta mguu wa McCarthy.

Baada ya kugundua alikuwa amevunjika mguu McCarthy, Rondon aliangua kilio muda wote hali iliyofanya wachezaji wenzake na hata kocha na madaktari kuanza kumbembeleza.

Mechi hiyo ambayo Everton ilikuwa nyumbani iliisha kwa sare ya bao 1-1, wenyeji wakisawazisha.










ANGALIA KIUNGO WA EVERTON ALIVYOVUNJWA MGUU, ALIYEMVUNJA AANGUA KILIO - SALEH JEMBE
 
Mkuu kosa lake nini hapo?
Sioni kosa, ni mchezo wapo wengine wanatwangana vichwa na mtu anazima mazima.

Huyu analia ni kuwa hakupenda, hakutegemea

Au tuseme alimpania, yametimia. Wengine furaha ikizidi wanalia.

Yote mawili yawezekana. Moyo wa mtu ni kichaka.
 
Sioni kosa, ni mchezo wapo wengine wanatwangana vichwa na mtu anazima mazima.

Huyu analia ni kuwa hakupenda, hakutegemea

Au tuseme alimpania, yametimia. Wengine furaha ikizidi wanalia.

Yote mawili yawezekana. Moyo wa mtu ni kichaka.
We jamaa bwana
 
Hugo Rondon anaonekana ana miguu nuksi!:D:D
Ila huu ndio utu aisee
 
James mcCarthy alimchomekea mwenzio.. ni faulo, ila kwa moyo wa kibinadamu lazima ujisikie vibaya kama rondon alivyojiskia.
 
Hakutegemea, amejutia kosa lake.
Angekuwa wa huku kwetu angejinyonga.

Kiti siyo changu.

Hapa Kwetu upo wakati Ahmed Amasha (Yanga) alimvunja mguu Yusuf Ambwene (CDA au Waziri Mkuu ya Dodoma ???)...dah...
 
Hakutegemea, amejutia kosa lake.
Angekuwa wa huku kwetu angejinyonga.

Kiti siyo changu.
dah kiongozi unarahisisha mambo yani mtu ajinyonge kwa ajali ya michezoni. hapo hakuna mwenye kosa kila mtu alikuwa anatumia nafasi yake.
 
Mbona aliwahi kutoka nje kabla ajapewa kadi ya moto.

Ndio ligi zenu za mchangani mnavyocheza hivyo?
hapo baada ya kujiingiza jamaa akaanza kumuita refa huyu kajiingiza mwenyewe ,ila baadae akaenda kumuona jamaa akaona kavunjika akaenda nje ya uwanja akawa analiaa
 
Back
Top Bottom