Angalia jinsi Tanesco inavyojimaliza kimapato! Inasikitisha! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Angalia jinsi Tanesco inavyojimaliza kimapato! Inasikitisha!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Zak Malang, Jan 3, 2012.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Le0 hii mchana kutwa network ya LUKU Tanesco ilikuwa haipatikani, maelfu ya wateja walikuwa wanahaha kutafuta kununua umeme.

  Hii ndiyo njia mojawapo Tanesco inavyojimaliza kimapato kwani itokeapo hitilafu katika network ya kuuza LUKU, kwa saa moja Tanesco hupoteza mamia ya mamilioni, nchini kote.

  Piga hesabu kwa mwaka mzima, Tanesco hupoteza mapato kiasi gani kutokana na hitiliafu katika network yake ya mauzo? Yumkini ni mabilioni!

  Halafu hapo hap[o Tanesco wanakuja na hoja ya kutaka kuongeza viwango vya umeme!!

  Hali hii inasikitisha sana. Tanesco ilikuwa inapoteza mabilioni kila mwaka kutokana kushindwa kukusanya madeni yake. Ikaamua kuiingia mfumo wa LUKU na mambo ni kama vile vile tu -- kupoteza mapato kutokana na kushindwa kusimamia network!

  Hivi hawa Tanesco ni kitu gani hasa wanaweza?
   
 2. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #2
  Jan 3, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Uzembe wa Tanesco kwangu faida. Walisahau kufunga mita nyumbani kwangu na kwa majirani kadhaa. ni zaidi ya miaka sita sasa tunatumia umeme bure. nimeamua kufungua karakana ya welding home ili nifaidi vizuri.
   
 3. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,157
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Si unambiwa shirika la TANDSCO (Tanzania Darkness Supply Company) linaongozwa na wanasiasa badala ya wataalamu, Kwa huu uzembe wao ndio maana wanaona njia rahisi ni kuongeza gharama za umeme
   
 4. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sina haja ya kuilaumu TANESCO binafsi, nafikiri (nafikiri) ni matokeo ya serilikali ya kishkaji ambayo haina uwajibikaji wala kushikishana adabu. Ndiyo maana rais anaweza kutofautina na watendaji wake halafu bado mambo yakaendelea.
  TANESCO ni shirika la umma, linategemea kila kitu kutoka kwa serikali kama ililvyokuwa TRC kabla haijakuwa TRL. Kama serikali inawekeza kidogo kwenye Nishati, hasa ya Umeme, unategemea TANESCO na bodi yao wafanye nini? Rejea yale ambayo amekuwa akiyarudia mara kwa mara RENATUS MKINGA kwenye midahalo na vipindi vya Masako ITV. Serikali ndiyo ya kulaumiwa kwa kila ambalo limetokea katika nchi hii kuhusu umeme. Juzi kati nikamsika Kikwete anasema sasa ruksa kwa wawekezaji wengine kuwekeza kwenye umeme, siyo tu kuzalisha, hadi kusambaza na kuuza. Kwa akili zake anafikiri kuwa anapunguza tatizo kumbe analiongeza. Wawekezaji wa kigeni unafikiri wataisaidia nchi hii kuondokana na tatizo sugu la nishati kwa bei ambayo hata mkulima kijijini ataimudu? Upupu tu!
  Katika kauli zake ambazo nilizisikia na wala sikuhisi kama aliyekuwa anaongea alikuwa rais mwenye mamlaka kikatiba na kama anavyojiita mwenyewe "MKUU WA NCHI" (Rejea kikao chake na wazee wa Dar), alisema kuwa ndani ya mwaka huu wenye siku tatu tangu uanze, serikali inajipanga kuongeza UWEKEZAJI WA WAGENI KUTOKA NJE NA NDANI. Hili neno "wa ndani" analitamka huku ulimi wake ukiwa mzito kabisa hadi msikilizaji unahisi kuwa hakupenda kulitaja basi, afanye nini!!
  Kwa mtazamo wangu, UWEKEZAJI WA WAGENI KUTOKA UGHAIBUNI HAUWEZI KUTUTOA HAPA TULIPO. SISI SOTE NI MASHAHIDI WA YANAYOTOKEA KWENYE MAENEO AMBAYO HAWA JAMAA WAMEWEKEZA. KARIBU KILA MGODI MKUBWA WA MADINI HAPA NCHINI UNA KIWANJA KIKUBWA CHA NDEGE NA NDEGE AMBAZO ZINAINGIA NA KUTOKA HUKO HAZIJAWAHI KUTUA HATA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JK NYERERE. LINI WAWEKEZAJI WATAUOKOA UCHUMI WETU? NJOZI HIZO ZA MCHANA, ANAFIKIRI KUWA ANATUDANGAYA, WANAOMUANDALIA HIZO HOTUBA NAO VILAZA KAMA ALIVYO YEYE.
   
 5. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Yule mama aliyesifiwa na DR slaa(mama Wandiba)wakati wa Sakata la Richmond,aliyegoma kusaini Mikataba yenye utata nae alishatimuliwa wakati ndo alikuwa Kichwa cha Shirika.....siasa Nyingi Tanesco
   
 6. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,024
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Michosho tu TANESCO.
   
Loading...