Angalia jinsi polisi wanavyozidi kuididimiza CCM mbele ya Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Angalia jinsi polisi wanavyozidi kuididimiza CCM mbele ya Watanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zak Malang, Jul 12, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi:

  Kufikishwa mahakamani kwa Mbunge huyu wa upinzani kunaifanya idadi ya wabunge wa upinzani kufikishwa mahakamani na serikali ya CCM tangu uchaguzi mkuu mwaka jana (chama hichi kilipoporomoka vibaya) kufikia wabunge kama 11 hivi.

  Kitu ninachokiona hapa ni jinsi mamlaka hizi za usalama na sheria za serikali ya CCM zinavyozidi kuididimiza CCM mbele ya macho ya jamii. Mamlka hizi zimeshindwa kuwakamata mafisadi waliotuibia hel;a zetu na kutuingiza katika mikataba ya kiwizi ambayo baadhi yao inatututesa hadi sasa – umeme.

  Halafu polisi wanashindwa kuwakamata wabunge wa CCM kama vile yule wa zamani wa Busega.


  __________________________
  Mbunge wa Chadema kizimbani Mbeya

  MBUNGE wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chadema, Joseph Mbilinyi na wezanke wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Mbeya kwa tuhuma za kuandaa mkutano wa hadhara kinyume cha sheria.

  Mbilinyi ni mbunge wa saba wa Chadema kupanda kizimbani akitanguliwa na wabunge wenzake, Freeman Mbowe (Hai), Godbless Lema (Arusha), Joseph Selasini (Rombo), Philemon Ndesamburo (Moshi Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki) na Esther Matiko (Viti Maalum), ambao wanashtakiwa kwa tuhuma tofauti katika mahakama mbalimbali nchini.

  Mbilinyi maarufu kwa jina la ‘Mr II au Sugu' alifikishwa mahakamani jana pamoja na wenzake ambao ni Mwenyekiti wa Chadema, Wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija, maarufu kwa jina la Mzee wa Upako na Katibu Mwenezi wa chama hicho wilaya ya Mbeya Mjini, Job Zebedayo Mwanyerere.

  Akiwasomea mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Mbeya, Michael Mtaite, Wakili wa Serikali, Apimaki Mabrouk, alisema Julai 8, mwaka huu watuhumiwa hao wakiwa katika eneo la Nzovwe, jijini Mbeya waliitisha na kufanya mkutano wa hadhara bila kutoa taarifa kwa Ofisa wa Polisi wa eneo husika.

  Mabrouk alifafanua kwamba, kitendo hicho ni kinyume cha kifungu cha 43 (i) na kifungu cha 46(iia) cha Sheria ya Polisi, kama ilivyorekebishwa mwaka 2002.Baada ya kusomewa shtaka hilo, watuhumiwa wote walikana kufanya kosa hilo. Hakimu Mteite aliuuliza upande wa mashtaka kama ulikuwa na pingamizi lolote kuhusu dhamana ya watuhumiwa hao.

  Wakili Mabrouk aliweka bayana kwamba, kwa kuwa shauri linalowakabili watuhumiwa linadhaminika kisheria, upande wa mashtaka hauna pingamizi lolote kuhusiana na dhamana ya watuhumiwa hao.Aliongeza kwamba, upande wa mashtaka tayari umekamilisha upelelezi wa shauri hilo, hivyo akamuomba hakimu kutaja tarehe ya kuanza kusikilizwa kwake.

  Hakimu Mfawidhi Mteite baada ya kupitia nyaraka za maelezo ya watuhumiwa wote, alibaini kuwa mshitakiwa namba moja kwenye shauri hilo ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo akampa ruhusa mbunge huyo kwenda kuendelea na vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini Dodoma.

  Aliongeza kwamba, watuhumiwa wote kabla ya kuondoka mahakamani hapo walitakiwa kujidhamini wenyewe kwa Sh100,000 kila mmoja ambapo, wote waliweza kujidhamini wenyewe na kuachiwa huru hadi Septemba 6, mwaka huu kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa.


  Mbilinyi na wenzake walikamatwa Julai 8, mwaka huu na polisi kabla ya kufanya mkutano na kisha kuhamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi Mbeya, ambako walihojiwa huku ulinzi ukiwa umeimarishwa na baadaye kuachiwa huru.

  Kupandishwa kizimbani kwa mbunge huyo, kuongeza kesi zinazowakabili wabunge wa Chadema, zilizopo mahakamani hadi sasa.Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema pamoja na Ndesamburo, Lema na Selasini, wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama ya kutenda tuhuma kufanya mkutano wa hadhara bila kibali, kukaidi amri ya Jeshi la Polisi na kufanya vurugu baada ya kutolewa amri ya Polisi.

  Mashitaka mengine ni kufanya mkusanyiko usio halali na kusababisha taharuki kwa jamii.
  Viongozi hao wa Chadema walifanya maandamano Januari 5, mwaka huu licha ya Jeshi la Polisi kukataza kwa misingi ya kiusalama, pia wafuasi wao wanadaiwa kutaka kuvamia Kituo Kikuu cha Polisi Arusha kuwatoa viongozi waliokuwa wanashikiliwa. Katika ghasia hizo, watu watatu walipoteza maisha kwa kupigwa risasi na polisi, akiwamo raia mmoja wa Kenya.

  Siku chache zilizopita, Mbowe aliwekwa mahabusu kwa siku mbili katika Kituo Kikuu cha Polisi Dares Salaam kutokana na kukiuka masharti ya dhamana.Lissu na Matiko wao wanatuhumiwa kuchochea vurugu katika wilaya ya Tarime, mkoani Mara na kesi yao bado inaendelea.

  Chanzo: Mwananchi
   
 2. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Counterpunch, unaongea kama vile huyo sugu anaonewa. Una maana wabunge wa upinzani watapotumia karata ya fujo uvunjifu wa amani waachiwe tu? Eti kwa nini? Kwa kuwa ni wapinzani. Licha ya hayo, rekodi ya Sugu kabla hajawa Mbunge umesha isahau? Jee, hii ni mara yake ya kwanza kupandishwa mahakamani? Si anajulikana kuwa ni mtu wa fujo? Au wewe umesahau visa vyake?
   
 3. emmanuel1976

  emmanuel1976 JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 301
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani anachosema huyu jamaa ni kwa nini CCM inatumia dola vibaya katika kupambana na upinzani nchini! Kwa maneno mengine , kwa nini makosa ya wapinzani ndiyo yanaonekana machoni pa jeshi la polisi? Paliwahi kuwekwa mada hapa juu ya aliye kuwa mbunge wa Musoma mjini Mr Mathayo ambaye majuzi alifanya mkutano wa hadhara huko Musoma akilindwa na FFU hadi saa 12:30 wakati sheria inasema wisho ni saa 12:00, je tuamini kuwa CCM wako juu ya sheria? ( Zitto amewahi kukamatwa kwa kuzidisha dakika 20) je hii ni uvunjifu wa sheria am utii wa sheria? Ama sheria huwa zinavunjwa na wapinzani tu?
   
 4. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Watawapiga, watawaweka chini ya ulinzi, watawaweka selo, Watawapandisha wote kizimbani na mwisho watawapeleka magereza. Ila hawataweza kuzibadili fikra za kimageuzi tulizonazo hivi sasa. Hakuna kulala hadi kieleweke!
   
Loading...