Angalia akili kubwa inavyotawala akili ndogo

Morning_star

JF-Expert Member
Apr 21, 2018
4,155
11,465
Ukweli ni kwamba mtandao wa mawasiliano ya kompyuta ulimwenguni "Internet" hakuna mtu anayeumiliki. Waasisi wa mawasiliano ya internet ni jeshi la marekani katika mawasiliano ya vita ya pili ya dunia. Baadaye akatokea jamaa mmoja namkumbuka jina lake la mwisho "Lee" akauboresha kwa ajili ya matumizi ya kiraia. Baada ya hapo ikawa ni fursa kwa kila mtu yeyote duniani kuiona hiyo fursa ataitumiaje kujikomboa?

Kwa wale wenzangu na mimi lugha inayotumika kwenye internet inafundishika na mtu yeyote anaweza kujifunza na kuiandika na kuanza mawasiliano bila kuzuiwa au kuingiliwa na yeyote.

Nawapa mifano kadhaa jinsi watu walivyoona hiyo fursa jinsi walivyoibuka na kuwa matajiri wa kupindukia na kuzitajirisha pia nchi zao.

Moja:
Jamaa anayemiliki tovuti ya kuuza na kununua vitu mtandaoni (www.amazon.com). Alichukulia fursa ya internet akaandika lugha ya kuwezesha kurahisisha watu kuuza na kununua mtandaoni na kufikia mamillioni ya wateja nchini kwake baadaye duniani na sasa ni trillionia. Tena aliacha shule (school dropout) ila baadaye baada ya kufanikiwa alirudi shule kumalizia masomo.

Mbili:
Mmiliki wa mtandao wa kijamii wa Facebook.com. Huu mtandao ulianzishwa kwa lengo la kutunza kumbukumbu za wanafunzi baada ya kumaliza chuo waendelee kuwasiliana. Huyu tena alikuwa kijana chuoni (japo hakuwa mwanzilishi haswaa kivilee) ila alichukulia udhaifu wa wenzake akauboresha na sasa ni billionaire na anaiingizia pia nchi yake hela.

Tatu:
Anayemiliki youtube.com. Hapa huyu jamaa alikaa akazipa akili kazi baada ya kujua watu wanatengeneza picha_mwendo (movies) na ikiwa atarahisisha watu kuzipakia na kuzipakuwa (upload/download) basi atakuwa na watu wengi wa kutembelea tovuti yake na anaweza kuingia mkataba na makampuni ya simu kwa kila bundle la Internet linalotumika kuwasiliana na mtandao wake awe analipwa. Sasa ona anavyopiga hela ndefu mpaka wabongo wanatengeneza TV channel kibao na wasanii utasikia napatikana YouTube nisubscribe utanipata na jinsi anavyopata watembeleaji wengi kwa bundle la Internet unalotumia anapewa commission (hela/mgao) na mwenye mtandao (YouTube).

Mfano wa mwisho kwa leo ni huyu jamaa wa kubeti (Betting). Huyu jamaa aliona watu wanakaa kwenye vijiwe wanabisha kuhusu timu gani bora itashinda au itashindwa, mchezaji gani atafunga bao lipi au mangapi dakika ya ngapi na blahblah nyingi. Jamaa akaona isiwe shida. Kaingia mtandaoni katengeneza website (interactive website) wenzangu mtakuwa mmenielewa ili ubishi uhamie kutengeneza pesa. Kwanza huyu kwenye website anakula hela mara mbili. Kwanza washiriki lazima uingize pesa kwa njia ya mobile pesa (mpesa/tigopesa n.k.), pili kutokana na wingi wa watu wanaoitembelea kupitia application za simu (mitandao ya simu) inamlipa kwa kila bundle la Internet.

Mifano ni mingi nikianza kuangusha nondo hapa tutakesha.

Nini chakufanya;
Jamani wabongo kama fursa za kutengeneza hela bongo hamzioni basi jiulize hiyo shilling miambili unayoitumia kwa chochote unachokinunua jua kwamba kuna mtu kama wewe kaweka mtego umpelekee hela! Nawewe waza mtego wako ili kila kukicha watu wakuletee hela.

LEO ASUBUHI WAKATI BADO NIMELALA NIKASIKIA MTU ANAGONGA HODI NYUMBANI KWANGU. NIKAMPOTEZEA LAKINI KAENDELEA KUGONGA. NIKAONA ISIWE TABU HEBU NIKAMCHEKI KULIKONI. HILE NAFUNGUA GATE NAKUTANA NA MMAMA ANAUZA MAANDAZI. DAAAAH!

Unajua nini? amenisaidia sana kunipa wazo la kuandika uzi huu! Huyu mama ukimchulia poa unaweza kumdharau lakini anaakili kama hao niliowatolea mifano, ila tofauti yake anafanya kikawaida saaana mambo yaleyale ambayo yanaweza kufanywa na mtu yeyote na mwisho wa siku kutoboa ni ngumu au changamoto si cha mtoto. Hila cha muhimu huyu mama kaweka mtego wa kunasa pesa za watu kila asubuhi.

Kwa kweli niliingia ndani nikamuungisha maandazi ya buku jero (1,500) nikayafunga vizuri kwenye mfuko wa nailoni natoa moja nakula kiaina wakati naenda kwenye mishe zangu ila tatizo yanalowanisha midomo na cha kupangushia sina zaidi ya viganja na hapa mikono imelowa mafuta ya uto ya maandazi utadhani nimeyaiba!!
 
Akili kubwa ni kuona fursa na kuzitumia, Nadiriki kusema jeff, zuckerberg , jamaa wa Tick tok, likeee, ni akili tena mnooo bila kumsahau jamaa wa badoo Huyo katisha , 😂😂😂😂😂

Nipo nawaza deal la miaka 7 mbele ambapo nitaweza kufikia Wahitaji huduma Milioni 2 kwa siku na nipate faida Tsh 300 kwa kila kichwa ....bado kichwa kinawasha kutafuta hiyo deal/biashara

Tupo pamoja mkuu
 
Ni mawazo mazuri sana.

Usiziamini sana hizo stori za makampuni ya teknolojia. Kuna siri nyingi sana hazisemwi ili kuwaontario watu katika soko la hisa la huko USA.
Pia internet inamilikiwa na USA kwa 100%. Yapuuze maneno ya kwamba internet haimilikiwi na mtu.
 
Ni mawazo mazuri sana.

Usiziamini sana hizo stori za makampuni ya teknolojia. Kuna siri nyingi sana hazisemwi ili kuwaontario watu katika soko la hisa la huko USA.
Pia internet inamilikiwa na USA kwa 100%. Yapuuze maneno ya kwamba internet haimilikiwi na mtu.
USA Kuimiliki kivipi? Labda kumiliki wingi wa miundombinu na mitambo ya kurushia na kupokelea data nikiwa na maana (host servers, global cabling, satellite, n.k.). Hapa naongelea lugha ambayo inatumika kuandika kwenye internet na kutengeneza cha kwako jinsi unavyotaka alafu ukahifadhi kwenye computer yako nyumbani kwako (kama unaweza) au kupangisha kwa wenye computer hizo (host servers) ili kwamba ukitaka iingie mtandaoni ionekane au isionekana hayo yoote ni juu yako na hakuna kiingilio. Ndo maana tunasema "Internet is free, no one owns it"
 
Back
Top Bottom