Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 55,881
- 29,255
'Anelka alichomoa penalti'
LONDON, Uingereza
MSHAMBULIAJI Nicolas Anelka alikataa kupiga penalti ya tano katika mechi ya fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Mshambuliaji huyo wa Chelsea alikosa penalti ya saba mjini Moscow na kuifanya Manchester United kutwaa kombe la Ulaya kwa kushinda penalti 6-5.
Lakini Anelka amesema aligoma kupiga penalti ya tano ya ushindi ambayo ilikoswa na John Terry na kuwafanya wapinzani wao kupata uhai, kwa kuwa alikuwa amechanganikiwa kwa kuingizwa mwishoni kama machazaji wa akiba.
Mfaransa huyo alisema: " Nilitakiwa kupiga penalti moja kati ya tano, lakini nilisema hawezekani nimeingia kama beki wa kulia na mnanitaka mimi kupiga penalti.
" Kwa hiyo nilienda kupiga penalti ya saba lakini Edwin van der Sar aliokoa. Alikuwa na bahati. Sikufikiri kama ningeweza kuingizwa.
"Nilikuwa kwenye benchi hadi dakika ya 110 mara nikaambiwa kuingia kucheza sikufanya mazoezi ya kutosha kupasha," alisema.