Andrew chenge: Mnashangaa hivi vijisenti tu, ipo siku ukweli utajulikana

Mimi ni Goddess Isis, iliniuma sana sana ile issue aisee, alafu akaamriwa na mahakamani alipe visenti kwa ajili ya roho za kina dada wale, jamani! Inasikitisha sana!
RIP wadada may the highest powers AVENGE you!

aliambiwa alipe laki 7 hahahhahaha
 
Wakati alipokuwa akisakamwa sana juu ya kuripotiwa kuwa anamiliki zaidi ya USD 1,000,000 nje ya nchi, Mh Chenge huku akiwa na hasira mbele ya waandishi wa habari aling'aka ni vp waandishi na watanzania kwa ujumla washangae hivyo vijisenti kiasi cha zaidi ya shs bilioni moja anavyomiliki? Na aliongeza kuwa iko siku ukweli utabainika.

Kama mwanasheria mahiri na kiongozi mkubwa tu wa taifa hili, Mheshimiwa Chenge hakuteleza na kwa kweli anayo siri na ufahamu mkubwa tu moyoni.

Toka kauli yake hiyo tumeshuhudia kugundulika kwa uchafu mwingi tu ndani ya Serikali kuanzia MEREMETA, EPA, UBADHIRIFU WA FEDHA ZA SERIKALI na mengine mengi.

Wiki hii nayo imefahamika kuhusu umilikaji wa fedha zaidi ya bilioni 300 zilizoibwa Serikalini na kutoroshewa mabenki ya nje!!

Hoja yangu:- Ni vipi Serikali hii inajipambanua kama inayojali watu wake inashindwa kuwakamata wahalifu hawa? Tatizo ni lipi? Tunao makachero wetu, Tunao watu wanaojua KILICHOTENDEKA kama Chenge n.k

Sasa niwapi tuna kwama viongozi wetu wa Serikali hii.
Aisee, alikuwa na haki ya kusema vyake vilikuwa vijicent, kupiga Fuso karibu mia nne zilizojaa dhahabu safi si mchezo.
 
Mzee na Mtaalamu wa sheria anaetumia utaalamu wake wa Harvard kutuibia
 
Ni nani aliye msafi ndani ya moyo wake?
Binadamu wote tumejaa roho mchafu wa kupenda mali, hata Chadema wakipata upenyo wataiba.
Mimi nikiwa ni mpenzi wa Chadema, nashauri kwenye kutoa maoni yetu kwenye katiba tuitakayo, katiba itamke kabisa kuwa wizi wa mali ya umma ni uhaini, na kifo ndio adhabu stahili

Mkuu Bujibuji hao Chadema wenyewe ndo hawa hawa wamekuja kukumbatia madubwana ya ufisadi, nani atapitisha hii sheria?

Back then, leo mambo yanaibuka upya.
 
niliishaamua kuachana na siasa kitambo baada ya kupinga mifumo ya design hii na kujikuta nashughulikiwa severely....
 
Back
Top Bottom