Andrew chenge: Mnashangaa hivi vijisenti tu, ipo siku ukweli utajulikana

DATAZ

JF-Expert Member
May 25, 2012
2,449
5,974
Wakati alipokuwa akisakamwa sana juu ya kuripotiwa kuwa anamiliki zaidi ya USD 1,000,000 nje ya nchi, Mh Chenge huku akiwa na hasira mbele ya waandishi wa habari aling'aka ni vp waandishi na watanzania kwa ujumla washangae hivyo vijisenti kiasi cha zaidi ya shs bilioni moja anavyomiliki? Na aliongeza kuwa iko siku ukweli utabainika.

Kama mwanasheria mahiri na kiongozi mkubwa tu wa taifa hili, Mheshimiwa Chenge hakuteleza na kwa kweli anayo siri na ufahamu mkubwa tu moyoni.

Toka kauli yake hiyo tumeshuhudia kugundulika kwa uchafu mwingi tu ndani ya Serikali kuanzia MEREMETA, EPA, UBADHIRIFU WA FEDHA ZA SERIKALI na mengine mengi.

Wiki hii nayo imefahamika kuhusu umilikaji wa fedha zaidi ya bilioni 300 zilizoibwa Serikalini na kutoroshewa mabenki ya nje!!

Hoja yangu:- Ni vipi Serikali hii inajipambanua kama inayojali watu wake inashindwa kuwakamata wahalifu hawa? Tatizo ni lipi? Tunao makachero wetu, Tunao watu wanaojua KILICHOTENDEKA kama Chenge n.k

Sasa niwapi tuna kwama viongozi wetu wa Serikali hii.
 
Sasa mkuu ukweli wenyewe si ndio huu wa bilioni zaid ya 300 na ndio maana alisema hivyo ni vijisenti akilinganisha na wengine wenye mabilioni kama haya yalioibuliwa na polisi wa kimataifa yaani interpol.
Tatizo hakuna alie msafi wa kumunyooshea mwenzake kidole na hivyo wao silaha yao pekee ni kulindana tu.
 
Ni nani aliye msafi ndani ya moyo wake?
Binadamu wote tumejaa roho mchafu wa kupenda mali, hata Chadema wakipata upenyo wataiba.
Mimi nikiwa ni mpenzi wa Chadema, nashauri kwenye kutoa maoni yetu kwenye katiba tuitakayo, katiba itamke kabisa kuwa wizi wa mali ya umma ni uhaini, na kifo ndio adhabu stahili
 
ANDREW CHENGE . ..MAMA TANZANIA SHUGHULIKA NAYE . ..DAH! AFANALEK . ..TUMECHOKA NAE KABISA . ..EHH RHABUKA MWENYE ENZI MUNGU TUSAIDIE . ...KATIKA JINA LA YAHUSHUA HA MASHAIC . .AMEN RA
 
IMG_4ut8uz.jpg
IMG_-rftgdn.jpg
 
Kwishney hili babu! Roho za mabinti za watu zitakumaliza wewe na kizazi chako afanalek walahi!
RIP wadada wawili waliokuwa kwenye bajaji!MAMA TANZANIA AMEAMKA!
Mzee upo vizur kwenye kumbukumbu
 
Mzee upo vizur kwenye kumbukumbu
Mimi ni Goddess Isis, iliniuma sana sana ile issue aisee, alafu akaamriwa na mahakamani alipe visenti kwa ajili ya roho za kina dada wale, jamani! Inasikitisha sana!
RIP wadada may the highest powers AVENGE you!
 
Back
Top Bottom