Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,671
- 149,843
Nawashauri msikubali kufa na tai shingono na badala yake wakiwafikisha mahakamani wekeni kila kitu wazi vikiwemo vimemo(kama mlipewa) vya kuwaagiza mfanye mliyoyafanya.
Na kwa mawaziri watakaoshitakiwa (kama kweli kuna atakaeshitakiwa) ombeni ruhusu ya mahakama ili ikiwezekana mtoe maelezo/nyaraka za vikao vya baraza la mawaziri in case mlitekeleza maamuzi ya baraza na si yenu binafsi.
Wabunge wa upinzani ikibidi muwasilishe hoja binafsi kutaka kinga ya raisi iondolewe na hoja nyingine za kutaka kashifa kubwa zote za nyuma kama vile RICHMOND, EPA, KAGODA, MEREMETA, KIVUKO KIBOVU,n.k zote zichunguzwe.
Ukitaka kusafisha nyumba husafishi sebuleni tu bali lazima usafishe nyumba nzima pamoja na vyumbani/chumbani tena mpaka kwenye uvungu wa kitanda.
Wanataka tumuunge mkono Raisi basi tumuunge kwa style hii pia na si kwa kusubiri kila kitu aanzishe yeye ndio tumuunge mkono.