Andrew Chenge Ateuliwa Kuwania Uenyekiti wa Bunge

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Kamati ya Uongozi ya Bunge imepitisha majina matatu ya wabunge watakaowania nafasi ya uenyekiti wa Bunge.

Majina hayo yamepitishwa na kamati hiyo iliyoketi jana kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 7.00 mchana ikiongozwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Taarifa za ndani kutoka katika kikao hicho, zilisema kikao kilikuwa na ajenda mbili ambazo ni uteuzi wa majina ya wenyeviti wa Bunge na kujadili ratiba ya Bunge.

Chanzo hicho cha kuaminika kimesema kuwa waliopitishwa ni Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge, Mbunge wa Viti Maalumu, Dk. Mary Mwanjelwa na Mbunge mwingine wa Viti Maalumu, Najima Murtaza Giga wote kutoka CCM.

Chanzo hicho kilisema wabunge hao wanakidhi matakwa ya kanuni inayoelekeza kuwa mwenyekiti wa Bunge ni lazima awe aidha mwenyekiti wa kamati au makamu mwenyekiti.

Katika uteuzi wa kamati uliofanyika mwishoni mwa wiki, Chenge ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo, wakati Mwanjelwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Najima ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria.

Kwa mujibu chanzo hicho, majina hayo ambayo ni kati ya majina sita yanayotakiwa katika kanuni, yatawasilishwa katika kikao cha kwanza cha mkutano wa pili wa Bunge utakaoanza kesho.

“Kanuni zinasema Spika atawasilisha bungeni majina sita yapigiwe kura na baadaye yapatikane matatu, hawa ndiyo walioomba wamesimama wamejieleza na kamati imewapitisha.

“Hadi tunafanya uamuzi huu Ukawa walikuwa hawajaleta majina, sisi hatujui kama wataleta au hawaleti, lakini majina yaliyopitishwa leo (jana) ndiyo hayo,” kilisema chanzo hicho.

Bunge lililopita wenyeviti wa Bunge walikuwa ni Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu, aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu, Lediyana Mng’ong’o na aliyekuwa Mbunge wa Uzini, Muhammed Seif Khatib.

Zungu amekosa fursa ya kutetea nafasi yake kutokana na kukosa sifa na hivi sasa yeye ni mjumbe wa kawaida wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba. Khatib na Mng’ong’o hawakufanikiwa kurejea bungeni.

Kamati ya Uongozi inaundwa na wenyeviti wote wa Kamati za Kudumu za Bunge, akiwamo Spika wa Bunge, Job Ndugai, Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai (Chadema).

Majina hayo yameteuliwa huku kukiwa na sintofahamu katika kambi ya upinzani bungeni kuhusu uteuzi na mpangilio wa wajumbe katika kamati mbalimbali za Bunge.

Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), havijaridhidhwa na uteuzi wa kamati hizo, hasa katika Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na ile ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zinazopaswa kuongozwa na wapinzani.

Kutoridhishwa huko kumewafanya wabunge wa kambi hiyo kususa shughuli za kamati ikiwa ni pamoja na kutoshiriki uchaguzi wa wenyeviti wa kamati, jambo linaloleta taswira isiyoeleweka.
 
Kila la heri mzee Chenge. Ukiachia vile vifursa vya hapa na pale vilivyompatia vile vijisenti, Chenge ni lesser evil. There are real mamonsters out there ila sio huyu mpendwa wangu!
 
Kwani mwenyekiti wa kamati ya PAC ni nani ?,

Mbowe kakataa PAC isiongozwe na Zitto.
Zitto nae kakataa pendekezo la Mbowe Mh.Kubenea matokeo yake Spika kaleta
watu tofauti kabisa Mbowe na Zitto wameungana kumpinga Ndugai.
Mbowe and Zitto wamekisaidia Chama cha Mapinduzi kuruka kiunzi cha kuteua Heavy duty wa Upinzani kuongoza PAC na LAAC huku POAC ikibadilishwa jina na kuitwa kamati ya Vitega uchumi hivyo Ccm Inatumia inaongoza kamati hii.
Mbowe na Zitto wanaweza wakamaliza tofauti zao wakafanya kazi nzuri kama Chadema walivyomaliza tofauti zao na CUF wakafanya vizuri DSM.
Naipenda sana CCM inayokimbizwa mchakamchaka na ukawa + Zitto. Refer bunge la Mama senkyuu vere macheee!
 
Najihisi mwenye mkosi kuzaliwa nchii ya TANZANIA bora hata ningezaliwa swala tu mbugani mida hii najilia tu zangu majani tu huku nikimcheki samba au chui watatokea wapi....kuliko kuishi mwanadamu ndani ya TANZANIA.....ni taifa ambalo maamuzi ya viongozi wake yatakufanya ukae ujiulize mara mbili mbili kuwa aliyefanya maamuzi haya anatumia kiungo gani kufikiria maana hata mwendawazimu mwenye kichwa kibovu hawezi kufanya maamuzi ya kipuuzi kama yanayofanywa na hawa viongozi wetu......aaaaaaaaaaaaarrgggg..............
 
ACT - Mbunge mmoja, Zitto

CDM+CUF - Wabunge zaidi ya 100; Sidhani kwa idadi hii kama bado tu wanamhitaji Zitto, yeye Zitto ndo anawahitaji wao.
 
Kamati ya Uongozi ya Bunge imepitisha majina matatu ya wabunge watakaowania nafasi ya uenyekiti wa Bunge.

Majina hayo yamepitishwa na kamati hiyo iliyoketi jana kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 7.00 mchana ikiongozwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Taarifa za ndani kutoka katika kikao hicho, zilisema kikao kilikuwa na ajenda mbili ambazo ni uteuzi wa majina ya wenyeviti wa Bunge na kujadili ratiba ya Bunge.

Chanzo hicho cha kuaminika kimesema kuwa waliopitishwa ni Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge, Mbunge wa Viti Maalumu, Dk. Mary Mwanjelwa na Mbunge mwingine wa Viti Maalumu, Najima Murtaza Giga wote kutoka CCM.

Chanzo hicho kilisema wabunge hao wanakidhi matakwa ya kanuni inayoelekeza kuwa mwenyekiti wa Bunge ni lazima awe aidha mwenyekiti wa kamati au makamu mwenyekiti.

Katika uteuzi wa kamati uliofanyika mwishoni mwa wiki, Chenge ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo, wakati Mwanjelwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Najima ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria.

Kwa mujibu chanzo hicho, majina hayo ambayo ni kati ya majina sita yanayotakiwa katika kanuni, yatawasilishwa katika kikao cha kwanza cha mkutano wa pili wa Bunge utakaoanza kesho.

“Kanuni zinasema Spika atawasilisha bungeni majina sita yapigiwe kura na baadaye yapatikane matatu, hawa ndiyo walioomba wamesimama wamejieleza na kamati imewapitisha.

“Hadi tunafanya uamuzi huu Ukawa walikuwa hawajaleta majina, sisi hatujui kama wataleta au hawaleti, lakini majina yaliyopitishwa leo (jana) ndiyo hayo,” kilisema chanzo hicho.

Bunge lililopita wenyeviti wa Bunge walikuwa ni Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu, aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu, Lediyana Mng’ong’o na aliyekuwa Mbunge wa Uzini, Muhammed Seif Khatib.

Zungu amekosa fursa ya kutetea nafasi yake kutokana na kukosa sifa na hivi sasa yeye ni mjumbe wa kawaida wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba. Khatib na Mng’ong’o hawakufanikiwa kurejea bungeni.

Kamati ya Uongozi inaundwa na wenyeviti wote wa Kamati za Kudumu za Bunge, akiwamo Spika wa Bunge, Job Ndugai, Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai (Chadema).

Majina hayo yameteuliwa huku kukiwa na sintofahamu katika kambi ya upinzani bungeni kuhusu uteuzi na mpangilio wa wajumbe katika kamati mbalimbali za Bunge.

Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), havijaridhidhwa na uteuzi wa kamati hizo, hasa katika Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na ile ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zinazopaswa kuongozwa na wapinzani.

Kutoridhishwa huko kumewafanya wabunge wa kambi hiyo kususa shughuli za kamati ikiwa ni pamoja na kutoshiriki uchaguzi wa wenyeviti wa kamati, jambo linaloleta taswira isiyoeleweka.

Kama CHADEMA tuliokuwa tunawaamini wamempa utukufu Lowassa...., Chenge nae ana haki jama!!
 
Najihisi mwenye mkosi kuzaliwa nchii ya TANZANIA bora hata ningezaliwa swala tu mbugani mida hii najilia tu zangu majani tu huku nikimcheki samba au chui watatokea wapi....kuliko kuishi mwanadamu ndani ya TANZANIA.....ni taifa ambalo maamuzi ya viongozi wake yatakufanya ukae ujiulize mara mbili mbili kuwa aliyefanya maamuzi haya anatumia kiungo gani kufikiria maana hata mwendawazimu mwenye kichwa kibovu hawezi kufanya maamuzi ya kipuuzi kama yanayofanywa na hawa viongozi wetu......aaaaaaaaaaaaarrgggg..............
Mkuu umeongea pointi sana viongozi badala ya kufanya mambo tusonge mbele wao wanafanya vitu vya kuturudisha nyuma sasa unapomchagua mtu kama Chenge mwenye kashfa kibao unamkomoa nani ??? maana kwa wenzetu ukishakuwa na kashfa basi wewe umeshakosa sifa za kuwa kiongozi.
 
Hapo ndio nampenda joka la makengeza haaaa haaaa wana muogopa wooooote ataendelea kutufundisha maana ya upigaji na nyie watumbuaji jaribuni kumgusa joka kama mna ubavu.
 
Huyu chenge kawafanya nini ccm yani hakuna mtu mwingine mpaka huyo tunayemjua fisadi
 
CCM NI CHAMA KILICHOSHINDWA KWA KILA HALI....NI KAMA VILE KIMESHAISHIWA PUMZI....KINAENDESHA NCHI KWA MTINDO WA BORA LIENDE....KUENDELEA KULALAMIKA NA KUWASHANGAA VIONGOZI WA CCM NI SAWA NA KUMSHANGAA MBUZI AKILA MAJANI KWANI NDIO STYLE YA MAISHA YAO......

Hatutakiwi kuanza kuyalalamikia maaamuzi mabovu na yakipumbavu ya CCM bali sisi wananchi ambao ndio tunaoumia tunachukua hatua gani dhidi ya haya maamuzi mabovu dhidi ya hawa tuliowapa ridhaa za kutuongoza( kama kweli tuliwapa ridhaa)......???

Pengine Tanzania inaingia kwenye maajabu ya dunia kwa kiongozi mwenye kashfa za ufisadi kuendelea kushika nyadhifa serikalini......huu ni zaidi ya upuuzi kama sio upumbavu....
 
ACT - Mbunge mmoja, Zitto

CDM+CUF - Wabunge zaidi ya 100; Sidhani kwa idadi hii kama bado tu wanamhitaji Zitto, yeye Zitto ndo anawahitaji wao.

Unashindanisha idadi ya wabunge mimi najadili umuhimu wa kushirikiana wote kwa pamoja kama idadi ingekuwa kigezo kama unavyowaza basi NCCR mageuzi ina mbunge mmoja isingekuwa sehemu ya Ukawa.
Muda wa kujadili nani kapata nini kwny uchaguzi uliopita umekwisha sasa tunajadili namna ya kufanya kazi Bungeni.
Punguza siasa za kizamani na mihemko.
 
Mkuu umeongea pointi sana viongozi badala ya kufanya mambo tusonge mbele wao wanafanya vitu vya kuturudisha nyuma sasa unapomchagua mtu kama Chenge mwenye kashfa kibao unamkomoa nani ??? maana kwa wenzetu ukishakuwa na kashfa basi wewe umeshakosa sifa za kuwa kiongozi.

Kama Lowassa mliona ana sifa ya kuwa Rais iweje muone Chenge hana Sifa ya kuwa Mwenykiti wa Bunge. Au kwa kuwa tu anagombea kupitia CCM kama ambavyo mngejifanya kushangaa ingetokea Lowassa agombee urais kupitia CCM!
Chenge angegombea kupitia Chadema mngekumbuka ufisadi wake?
Siasa za kinafiki ni mbaya kuliko za kifisadi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom