Andiko hili la kada wa CCM, Thadei Mushi ukakasi juu ya yaliyompata Dr. Ulimboka

simba jike

Senior Member
Mar 23, 2017
182
535
Jukwaa la Wahariri ndio kalamu ya watanzania, hiki ndio chombo kinachochuja, kuchunguza na kuthibitisha wananchi wawalishe nini kwa maandishi.

Huyu moja kwa moja kaonyesha Itikadi yake na imekuwa ikijionyesha mara nyingi. Pamoja na Itikadi yake bado waandishi wameamua kumchagua na kuendelea kuwa kiongozi wao.

TLS ni chombo cha Kisheria ambacho ni mtetezi wa wanyonge wa Tanzania ambao haawana msaada kisheria. Ndio chombo ambacho ambacho kinatusemea Kisheria vs Watafsiri wa sheria (Mahakama). Kiongozi wake ni Tundu Lisu, huyu alioitishwa kwa Kura nyingi japokuwa anajulikana ni mwanaharakati wa chadema.

LHRS ni kituo cha kutetea haki za binadamu, kiongozi wake mama Kijo Bi Simba tumekuwa tukimlaani Kila siku kuwa ni mwanachadema. Hata mm nimekuwa nikifanya hivyo kutokana na kauli zake na vutendo vyake.

NINI NAMAANISHA?

Ili tufanye siasa kwa kiwango cha juu lazma ukamate asasi na Taasisi Muhimu katika nchi. Eneo hili Chadema wanafanya vizuri sana. Kila asasi na Taasisi hizi zinapokuwa zinafanya Uchaguzi vyama vyetu kwa namna moja au nyingine wamekuwa wakitumbukiza huko mikono yao. Ila cha ajabu hawa wapinzani wanafanikiwa kutugaragaza. Lazma tujitazame katika hili na tuandae mipingo ya kuzirudisha kwenye mikono yetu.

Hili halina ubishi watu mpaka wanashindwa kuficha hisia zao wanazitoa hadharani. Na halina ubishi kuwa viongozi wa Asasi hizi ni wanasiasa wa upinzani kwa asilimia zote. Kuna kipindi pia walifanikiwa kutusimamishia Pandikizi Ulimboka alitusumbua sana tukasema Liwalo na Liwe. Msaidizi wake Ulimboka alikuwa Dr Mashinji huyu katibu mkuu wa Chadema kwa sasa.

Kuna kipindi niliwahi kusema kuwa tuna haja ya kuangalia watu wenye ushawishi mkubwa kwenye Jamii na kuwaomba kukaa kimya au kuisema Serikali.

Nikashauri na kutahadharisha kuwa mtu Kama Edo Kumwembe ana viashiria vyote vya kugombea 2020. Fuatilieni nyendo zake huyu anaongea Lugha ya Upinzani najua Upinzani unaweza kumuwahi na kumpa jimbo la Kugombea. Mara nyingi watu kama hawa kuwashinda inakuwa ngumu sana. Huyu hata kama hagombei Kauli zake zinawanufaisha zaidi wapinzani.

Ni watu wanaojua kuongea Lugha zote za kihuni na kistaarabu, nchi hii Maisha yamewageuza watu wengi wamekuwa wahuni hivyo kushinda ni jambo jepesi sana kwake.

Huyu ni mtu aliyekaribu sana na kina Prof Jay nadhani tutakuja kuona haya mbeleni. Hawa wakina Sugu, Lema, Prof Jay wanawashinda maprofesa wetu na Madr wetu kwenye majukwaa ya kisiasa.

Hata tukipeleka msomi wa aina gani mbele ya wagombea hawa wanaojua kuongea na Masela tutapigwa tu. Kuna Kina Roma, Ney Wa Mitego na wengineo wanatumbukia kundi hili.

Chadema wala hawahangaiki na watu wasomi sana ndio maana kina Baregu na Safari wala hawaruhusiwi kushika form za ubunge wao kazi yao ni kukaa nyuma ya wabunge wao kutengeneza vitu vya kuongea.

NINI TUKIFANYE SASA.

Kwanza ni kukusanya watu wote wenye influence wawe upande wetu.

Mbili kila anayeonyesha kiashiria cha kugombea Upinzani tumuwahi na kutafuta strenghts zake.

Tatu: Mwisho tuangalie Upya namna ya kutumbukiza watu wetu kwenye hizi asasi Muhimu.

Ole Mushi.
 
Poleni sana maana mmepigwa upofu hadi hamuoni pa kutokea. Kifupi kwa hoja hii ina maanisha wapiga kura ni wahuni kwa kuwasikiliza wahuni na kuwapigua kura wahuni.

Kweli kabisa mwandishi na chama chake wamedhihirisha walivyo wahuni.
 
Duuuuh!!haya yote unamshauri nani kwa mfano,hivi unaelewa nini maana ya neno sipangiwi wala sijaribiwi?
 
Back
Top Bottom