Ancelotti: Chelsea ni lazima ibadilike kwa Man United | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ancelotti: Chelsea ni lazima ibadilike kwa Man United

Discussion in 'Sports' started by kilimasera, Apr 11, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  LONDON, England
  KOCHA Carlo Ancelotti amekiri kuwa Chelsea inatakiwa kubadilika haraka kama wanataka kuendelea kubadi kwenye Ligi ya Mabingwa hapo kesho watapocheza dhidi ya Manchester United.

  Vijana hao wa Ancelotti watakuwa ugenini Old Trafford kwenye mchezo wa pili wa robo fainali wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 baada ya Wayne Rooney kufunga goli la kwanza kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

  Chelsea ilipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Wigan hapo Jumamosi, lakini Blues kwa mara nyingine walikuwa chini ya kiwango.Kocha wa Chelsea, Ancelotti amekuwa na mashaka na kiwango hicho kidogo kabla ya kuwavaa vijana wa Sir Alex Ferguson.

  "Ni jambo zuri kushinda. Si kitu rahisi," alisema Ancelotti."Hatukuwa vizuri kwenye kipindi cha kwanza, cha pili tulikuwa vizuri na kitu kizuri kujenga moyo wa kujituma, lakini mwisho wa siku tumeshinda ndio jambo muhimu.

  "Tunatakiwa kucheza vizuri zaidi Jumanne. Kushinda mchezo huo tunahitaji kucheza kwa asilimia 100."

  Ancelotti na vijana wake wanajua kuwa ushindi Old Trafford ni kitu muhimu katika kuamua mbio zao za ubingwa dhidi ya United.Kasi ya kufunga wa Chelsea iliyokuwa nayo mwaka jana imepungua na Ancelotti amekubali kuwa kikosi chake kimekuwa kwenye hali mbaya zaidi kwa sasa.

  "Ni wazi tupo kwenye hali mbaya kulinganisha na msimu uliopita," alisema. "Msimu uliopita tulifunga mabao mengi lakini sasa mambo ni tofauti kabisa.
   
 2. F

  FUSO JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,811
  Likes Received: 2,294
  Trophy Points: 280
  Play fit again Yossi at midfield, Essien to be a holding mid, Ramires and Lampard - Up front play Drogba.

  CECH

  IVANOVIC ALEX TERRY COLE

  ESSIEN LAMPARD RAMIRES

  YOSSI DROGBA ZHIRKOV

  Formation is 4 - 5 - 1 when we dont have a ball and can change to 4 - 3- 3 when attacking with Yossi to the right and Zhrkov to the left.


  Zhirkov and Yossi can create chances from the wings. Try this for 60minutes if wont work Please Sub Ramires with Kalou, Drogba with Torres, drop Zhrkov at the middle.

  Kalou is faster, Torres is fasta, Yossi is fasta - Torres can play at the center waiting for those killer balls from left & right.

  JOB DONE!!!!
   
Loading...