MGOGOHALISI
JF-Expert Member
- Apr 16, 2011
- 1,984
- 2,586
Wale wahenga wenzangu mtakua mnakumbuka jinsi mwl Nyerere alivyokua anaita waandishi wa habari na kuongekea mambo mbalimbali yanayohusu nchi. Hili alilifanya hasa alipoona mamba yanaenda ndivyo sivyo.
Ninakumbuka alipokemea kuhusu kupuuzwa kwa katiba ya nchi kipindi cha uongozi wa mzee Mwinyi. Hii ilionyesha uwajibikaji kwa kiongozi mstaafu na iliwakumbusha walioko madarakani majukumu yao.
Kwa miaka ya karibuni hali hii imekua tofauti. Huwezi kusikia wastaafu waliopo kuzungumzia mambo au kukemea maovu yanapofanywa na walioko madarakani. Je ni woga, kupuuza au ni sehemu ya wale wanaofanya kinyume?