Anayopitia mdogo wangu wa kike siyo sawa na umri wake, inaniumiza sana...

Maisha haya una watoto wawili na baba zao kawakupi hata 100 ya kununua japo chakula na wewe mwanamke huna chochote hata mtaji bhasi usipochukua uamuzi mgumu wa kwenda kuwapeleka kwa baba zao kwa heri ama kwa shari kuna siku unaweza wapa sumu na wew ukajiua ukidhani ndio njia pekee na jibu.
 
Kama huwezi kumsaidia mdogo wako pole sana lakni msaidie awapate wanaume aliozaa nao yani japo atakuja onekana mama katili watoto wakikua ila hana jinsi.. Akishdwa kuwapata bhasi msaidie japo mtaji kama huna mwambie aweke njia ya uzazi wa mpango ajiongeze. Pole sana!
 
aise acha nami nikulalamikie kidg...! Unakumbuka nilikuunganishia kazi Mwanza mwaka juzi eh? Nikampa jamaa namba zako tunakupgia hupokei..! Binafsi nilishangaa na jamaa mie nilikua namjua ana roho ya huruma mno mno...kwanza suala la mshahara hata ungeshangaa hela anayokupa ungemsaidia sana sister ako..! Kwanza hakua na kazi alikua anTaka kijana tu wa kulinda jumba lake akiwa kazini..so ww ungepata fursa tena na tena za kufanya chichote as side hustle..anywys tuyaache haya

Namba 2 pole sana son....! Wewe ndo baba kwa hao wajomba! Mpe moyo dada kila uwezapo...
3.nitumie namba yake pm ila utamuambia wewe unitambulishe!

pole sana aisee!
ndio shida za vijana siku hizi, wakati mwingine labda hawahitaji misaada halisi wanataka michango labda
 
Pole sana jamaa yetu,, mnapitia magumu kwakweli, ila nnacho kuomba ujaribu tu kubariki haya maisha kwamaneno yako mwenyewe... Ukiwa unalaumu maisha nakusema maisha ni ovyo yanakua ovyo hivohivo... Lakini ukisemea mazuri mazuri yatakuja hata Kama sio leo...
Mungu akutie nguvu akupe furaha na maisha bora ili usaidie na ndugu zako na wote wenye shida maana unajua shida ninini naamini ukitoboa hutosahau kusaidia waitaji... Mungu atulinde..
 
Ni mdogo wangu wa kike, anayoyapitia yananiumiza mimi kama kaka yake. Najiona mwenye hatia ndani ya nafsi.

Wazazi wetu walifariki na kutuacha tukiwa wawili, tukiwa wadogo.

Mimi kama kaka niliingia mtaani na nikaishi mtaani kama chokolaa, nilishuhudia na kujionea ni namna gani wanadamu walivyo watu wa hovyo.

Kunyanyaswa, kuonekana mbwa mbele za watu ilikuwa kawaida kwangu mpaka nikaizoea hiyo hali.

Nimeishi kama mtoto wa mtaani mpaka nimekuwa kijana. Nimeyaona mengi huko.

Nikirudi kwa mdogo wangu wa pekee, alipewa mimba akiwa na miaka chini ya 16, mimi binafsi simlaumu kwa kupewa mimba, angejuaje hayo mambo kuwa yana madhara mbeleni? Alikuwa bado mdogo.

Kwakuwa mdogo wangu alikua hasomi, kupewa kwake mimba haikuwa jambo la kushangaza wala kushtua watu, ukizingatia hakuna mzazi wala mlezi aliyepo.

Alilea mimba na akajifungua katoto, kasichana, nikapewa nafasi ya kumchagulia jina, nikasema aitwe 'Furaha' .

Akapewa tena mimba, naamini ni katika kujaribu kujitafutia nahitaji yake na mwanae, alipewa mimba tena.

Afanyeje sasa? Msaada ninaoutoa kwake ni kama tone ndani ya bahari, si chochote, haisaidii. Na sasa naona magumu zaidi yamemfika.

Mara kadhaa hunipigia simu huku akilia na kusema maneno ambayo binafsi yananiumiza sana, ananiambia mpaka mambo ambayo kwakweli naamini hakupaswa kuniambia, lakini amwambie nani sasa? Mimi ndiye ndugu yake.

Anayopitia siyo sawa na umri wake, hii hali inaniumiza sana mimi kama kaka yake. Nazikumbuka sana nyakati nzuri tukiwa na wazazi wetu.

Mimi binafsi nimejifunza mengi katika kuishi, nimepata changamoto nyingi hata sasa nazikabili.

Ila changamoto anazopata mdogo wangu ni kubwa Mara dufu, ana watoto, hana mzazi wala mlezi, anawatunza vipi watoto?

Haya maisha ni hovyo.
Pole sana Kaka binafsi nimeguswa mno maana nayajua maisha ya kuishi Kama chokoraa huna wazaz Wala walezi ukiwa binti mdogo kwakweli simlaumu kupata mimba hizo ni matatizo mazito mno

Nilianza maisha ya kujitegemea kila kitu nikiwa na miaka 18 Ila msoto wake sitamani kukumbuka kuishi bila kula hata siku tatu ilikua kawaida kwangu, kufukuzwa Kodi etc all in all bado napumua

Pambana Kaka msaidie mdogo wako kwa namna yoyote
 
Wengi tumepitia maisha hayo machozi yamejaa kwenye vifua vyetu na hatukua na pa kuegemea dah nakumbuka mbali Sana nilipoanza kujitegemea nikiwa na miaka 12 ndani ya jiji la dar lakini mpka sasa nimesonga ni maisha ambayo watoto wengi wa kimasikini tunapitia kwa sababu unabeba majukumu ukiwa na umri mdogo kikubwa ni kupambana tu Mungu atakusimamia
 
12?oh no!...dah...aise
 
Anayopitia siyo sawa na umri wake, hii hali inaniumiza sana mimi kama kaka yake. Nazikumbuka sana nyakati nzuri tukiwa na wazazi wetu.

Siku njema zijapopita usihuzunike bali ufurahi kwakuwa zilikuwako!
Mungu atampigania
Siku njema zijapopita usihuzunike bali ufurahi kwa kuwa zilikuwako.
 
Wengi tumepitia maisha hayo machozi yamejaa kwenye vifua vyetu na hatukua na pa kuegemea dah nakumbuka mbali Sana nilipoanza kujitegemea nikiwa na miaka 12 ndani ya jiji la dar lakini mpka sasa nimesonga ni maisha ambayo watoto wengi wa kimasikini tunapitia kwa sababu unabeba majukumu ukiwa na umri mdogo kikubwa ni kupambana tu Mungu atakusimamia
Maisha ni safari. Tutafika tu.
 
Back
Top Bottom