Anayewalipa wanaopiga kelele za Katiba Mpya atalipa hadi lini?

Sep 17, 2021
25
75
Mitandaoni hususan Twitter, kuna kelele nyingi zinazoitwa 'madai ya Katiba Mpya'

Ukitazama vizuri utagundua kwamba huo ni mradi wa watu. Yes, kuna mahali wanapata fedha kupiga hizi kelele zionekane ni madai ya walio wengi.

Nenda katazame mtindo wao wa kupost. Kuna siku wanaamka na caption moja, hasa inapokuwa ya Kingereza. Caption hiyo moja inatumiwa na account nyingi sana jambo linalooonesga hiyo movement sio 'organic', sio madai halisi ya wengi. KINA MARIA SARUNGI WANAFURAHISHA WAFADHILI WAO.

Lakini pia, unakuta mtu mmoja anatumia hiyo hashtag kwa wingi usio wa kawaida kwenye post moja. Wanalazimisha iwepo hata pasipo stahili. LENGO NI KUPIKA KWAMBA HAYO NI MADAI YA WENGI ili wakapate mtonyo huko kwa mabwenyenye wao.

Najiuliza tena, kwa kuwa hili suala la Katiba Mpya halitatimia muda wowote soon (LABA AWAMU YA PILI YA URAIS WA SAMIA KAMA ATAAMUA KUANZISHA MCHAKATO): Anayewalipa kupiga kelele hizi ambazo zimeshapoteza mvuto atawalipa hadi lini?
 
Matrix19

JF-Expert Member
Feb 24, 2020
2,871
2,000
Katiba ya sasa ilitengenezwa zama zile simu zilizokuwa zikitumika ni rotary dial. Nchi ilikuwa na watu millioni 8 . Leo hii rotary dial nani anazitumia ? Serikalini kwenyewe wamezitupilia mbali.

Katiba hii hi haiwezi kumudu mahitaji ya watu millioni 60 na kukiwa na mabadiliko makubwa tu ya sayansi na teknolojia never!

Na by the way why CCM mkisikia katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ni kama mnahisi mmeambiwa mkae kwenye viti vyenye misumari?
 
Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
15,349
2,000
Mitandaoni hususan Twitter, kuna kelele nyingi zinazoitwa 'madai ya Katiba Mpya'

Ukitazama vizuri utagundua kwamba huo ni mradi wa watu. Yes, kuna mahali wanapata fedha kupiga hizi kelele zionekane ni madai ya walio wengi...
Wewe ndiye ulielipwa kupost ujinga.

Kwani katiba mpya ya wananchi iliyo fair inakudhuru nini ?! UJINGA NI KIPAJI JIPONGEZE
 
omujubi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
4,270
2,000
Endeleeni kutumia muda huu wa thamani kuandika ujinga badala ya kuungana na wanaoitaka KATIBA MPYA.

Siku akili ikikukaa sawa walau nawe uunge mkono, huenda hata uwezo wa kuandika haya au kusoma utakuwa huna tena
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
15,933
2,000
Wakati mwingine tutakapoamua kuandika katiba mpya tume ya katiba iundwe na wataalamu tu wa katiba na sheria wenye umri kuanzia miaka 45 kutoka ndani na nchi za mbali zilizo na demokrasia ya juu.
 
akida jr

Senior Member
Jan 1, 2014
109
225
Wakati mwingine tutakapoamua kuandika katiba mpya tume ya katiba iundwe na wataalamu tu wa katiba na sheria wenye umri kuanzia miaka 45 kutoka ndani na nchi za mbali zilizo na demokrasia ya juu.
Shida iliyokuwepo ni kwamba kwa kiasi kikubwa vuguvugu la madai na wanopingana (na huenda wakakubali siku za baadae)ni wanasiasa. Na hao hao ndio hujakutawala mchakato mzima kuanzia kwenye mamlaka ya kuandaa muundo wa tume na upatikanaji wa kiongozi wa hiyo tume pamoja na wajumbe wake. Na hata ikifikia wakati wa kuwapata wabunge wa bunge la katiba; 'majority' ni wao wao. Makundi mengine yanahusishwa/kushirikishwa tu kutimiza utaratibu na kuionesha jamii tu na hatimaye washiriki wanaowakilisha makundi mengine hutumika kusongesha ajenda za wanasiasa kwenye mchakato mzima.
 
Aaronrweumbiza

Senior Member
May 16, 2013
148
250
Mitandaoni hususan Twitter, kuna kelele nyingi zinazoitwa 'madai ya Katiba Mpya'

Ukitazama vizuri utagundua kwamba huo ni mradi wa watu. Yes, kuna mahali wanapata fedha kupiga hizi kelele zionekane ni madai ya walio wengi.

Nenda katazame mtindo wao wa kupost. Kuna siku wanaamka na caption moja, hasa inapokuwa ya Kingereza. Caption hiyo moja inatumiwa na account nyingi sana jambo linalooonesga hiyo movement sio 'organic', sio madai halisi ya wengi. KINA MARIA SARUNGI WANAFURAHISHA WAFADHILI WAO.

Lakini pia, unakuta mtu mmoja anatumia hiyo hashtag kwa wingi usio wa kawaida kwenye post moja. Wanalazimisha iwepo hata pasipo stahili. LENGO NI KUPIKA KWAMBA HAYO NI MADAI YA WENGI ili wakapate mtonyo huko kwa mabwenyenye wao.

Najiuliza tena, kwa kuwa hili suala la Katiba Mpya halitatimia muda wowote soon (LABA AWAMU YA PILI YA URAIS WA SAMIA KAMA ATAAMUA KUANZISHA MCHAKATO): Anayewalipa kupiga kelele hizi ambazo zimeshapoteza mvuto atawalipa hadi lini?
Tunataka Katiba Mpya
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom