Anayetuhumiwa ufisadi BoT aenguliwa Benki M

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Anayetuhumiwa ufisadi BoT aenguliwa Benki M
Shadrack Sagati
Daily News; Tuesday,February 19, 2008 @02:18

MMOJA wa watu wanaodaiwa kuhusika na ufujaji wa mabilioni ya fedha za umma kutoka Benki Kuu (BoT), Jayant Kumar Patel (Jeetu Patel) ameenguliwa kwenye umiliki na ukurugenzi wa Benki M, HabariLeo imebaini.

Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili imezipata zinasema kuwa benki hiyo imeondoa jina la ukurugenzi wa Jeetu. Patel alikuwa mmoja wa wamiliki wa benki hiyo iliyoanzishwa mwaka jana kupitia kampuni ya Noble Azania Investments Limited (NAIL) iliyokuwa na asilimia 20 ya hisa za benki hiyo wakati ikianzishwa.

Mmoja wa wamiliki wa benki hiyo, Nimrod Mkono amelithibitishia gazeti hili kuwa Patel ameondolewa ukurugenzi wa benki hiyo. Kwa sasa Jeetu hayupo nchini na kuna minong’ono kwamba huenda ametoroka.

Licha ya kutotaja lini wamemwondoa kwenye ukurugenzi Mkono alisema; “Hilo jambo siyo siri tena kwamba siyo mkurugenzi wa benki yetu tena.” “Siyo mkurugenzi tena…tumeona hatuwezi kuwa na mtu ambaye ana kashfa nyingi kiasi hicho,” alisema Mkono ambaye pia hakutaka kueleza kama Jeetu pia ameondolewa hisa zake kweye umiliki wa benki hiyo.

“Habari za hisa au mali zake mahali ziliko mimi sijui maana hazinihusu, sijui hizo hisa zake kama kampa mke wake au mtoto wake au kawapa Takukuru (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa) sijui. Waulizeni Benki Kuu ndiyo waratibu wa mambo ya benki…,” alisema Mkono alipozungumza na mwandishi wa habari hizi.

Tangu benki M ianzishwe zimekuwapo tuhuma mbalimbali kuwa imeanzishwa na watu wenye tuhuma mbalimbali akiwamo Jeetu Patel anayetuhumiwa kuhusika na wizi wa mabilioni ya fedha katika Benki Kuu ya Tanzania.

Kampuni zake tisa zilituhumiwa kuhusika na wizi wa takribani Sh bilioni 133 kupitia Akaunti ya Ulipaji Madeni Nje (EPA). Kwa mujibu wa sheria ya benki ya mwaka jana, leseni ya kufungua na kuendesha benki haiwezi kutolewa kwa mtu mwenye historia au rekodi ya makosa ya jinai, kufilisika, kukosa uaminifu au hujuma kwa serikali.

Kifungu cha 12 cha sheria za benki na taasisi za fedha kinasema mtu anakoma kuwa mkurugenzi na mmiliki wa benki iwapo atabainika kuwa amefilisika au atakapotiwa hatiani kwa makosa ya kughushi au ya kutokuwa mwaminifu. Katika kifungu hicho pia inaelezwa kuwa mtu anakoma kuwa mkurugenzi wa benki iwapo ataondolewa na bodi ya benki husika.

Benki M ilianzishwa Februari 21 mwaka jana ikiwa na mtaji wa Sh bilioni 6.5. Benki hiyo ambayo hufanya kazi hadi usiku siku zote saba za wiki kwa sasa ina tawi moja katika barabara ya Nyerere.

Wamiliki wa benki hiyo kwa mujibu wa usajili wake ni Jeetu Patel kupitia kampuni ya Noble Azania Investments Ltd, Vimal Mehta kupitia kampuni ya Negus Holding Ltd na Fedha Rashid ambaye anamiliki kampuni ya Africarriers Ltd. Mkono ambaye ni mwanasheria maarufu nchini alishatamka hadharani kuwa benki hiyo ni ya kwake na anamiliki hisa kupitia kampuni yake ya Equity & Allied Limited.

Pia kuna wamiliki wengine wanaotajwa ambao ni Sanjeev Kumar, mtaalamu wa mambo ya benki na Bhaskaran Nair anayetambulishwa kama mfanyabiashara. Wanahisa hao wanamiliki benki hiyo katika mchanganuo ufuatao: Negus Holdings Ltd (Sh bilioni 1.3b), Noble Azania Investments Ltd (Sh bilioni 1.3b), Africarriers Ltd (Sh bilioni 1.3), Equity and Allied Limited (Sh bilioni 1.3), Kumar (Sh milioni 650) na Nair (Sh milioni 650). Kila hisa ya benki hiyo ina thamani ya Sh 1,000.

Benki Kuu (BoT) kwa upande wake imethibitisha kupokea maombi kutoka Benki M ya kutaka kuruhusiwa kufanya mabadiliko kadhaa katika wanahisa wake. Kwa mujibu wa benki hiyo mabadiliko hayo ya wanahisa yanawahusu wanahisa mbalimbali akiwamo mwanahisa ajulikanaye kwa jina la Noble Azania Investments Limited (NAIL) anayemiliki asilimia 20 katika benki M.

Naibu Gavana wa BoT, Enos Bukuku aliliambia gazeti hili kuwa Jeetu Patel ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Noble Group inayomiliki pia kampuni ya NIL ambayo baada ya kujitoa inapendelea kuuza hisa zake zote kwa Tarek Al-Asharam raia wa Falme za Kiarabu (UAE).

Bukuku alisema kupelekwa kwa maombi hayo Benki Kuu kutokana na matakwa ya kisheria chini ya sheria za benki ya mwaka 2006 na kanuni za taasisi za fedha ya mwaka 1997. Alisema maombi ya benki hiyo kwa sasa yanafanyiwa tathmini na BoT kwa kufuata vifungu na kanuni zilizo ndani ya sheria.

“Tathmini hiyo itakapokamilika Benki Kuu itatoa uamuzi wa ama kuridhia au kutoridhia mabadiliko ya wanahisa ambayo BML inakusudia kuyafanya. Patel anatajwa kumiliki kampuni tisa ambazo zilitumika kuiba mabilioni ya fedha katika BoT zikiwamo kampuni sita alizosajili kwa siku moja ambazo ni Bencom Internationa Ltd, B. V Holdings Ltd, Venus Hotels Ltd, V.B Associates Company Ltd, Bina Rosort Lt na Bora Hotels & Apartment. Kampuni zake nyingine zinazotajwa kutumika kwenye ufisadi huo ni Maltan Mining Company, Ndovu Soaps Ltd na Navy Cut Tobacco Tanzania Ltd.

Makampuni hayo yako chini ya mwavuli wa Noble Azania Group ambayo Jeetu ni mmiliki wake Anadaiwa pia kumiliki kampuni katika miji ya London, Dubai na anadhaniwa kushikilia hati nyingi za kusafiria kwa majina mbalimbali. Historia ya Jeetu Patel nchini katika nyanja za biashara inaanzia mwaka 1978 wakati huo akijulikana kama muuzaji wa vipuri vya magari Dar es Salaam.

Chini ya kampuni hiyo ya familia iliyojulikana kama Azania Investment and Management Services Ltd (AIMS) amefanikiwa kuwa mfanyabiashara mkubwa wa kimataifa anayemiliki kampuni nyingi, kati ya hizo nyingine zikidaiwa kujishughulisha na biashara tata.

AIMS ilivyozidi kupanuka, iliingia katika kilimo kwa kuanza na shamba la hekta 1,500 huko Kimamba, wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro, chini ya usimamizi wa kampuni tanzu ya Azania Agriculture akianzia na tumbaku, miwa na mahindi.

Mwaka 1980, alinunua hekta 22,000 kwa ajili ya kilimo cha mkonge kutoka Mamlaka ya Mkonge Tanzania (TSA) huko Mvomero, Kilosa na baadaye viwanda vya kusindika matunda vya Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC) wilayani Korogwe.

Mkono aliwahi kunukuliwa akisema kuwa Benki M imeanzishwa iwakomboe Watanzania. Alisisitiza kuwa lengo la kuanzishwa kwake ni kutaka kuwawezesha Watanzania kuweka fedha katika benki ambazo wamiliki wake ni Watanzania wenyewe.
 
Hivi ile fee anayolipwa Mkono BoT ndio ukombozi kwa Mtanzania? Unawaibia 10,000 unawarejeshea 100.
 
Mkono yeye mwenyewe fisadi na pia ana kashfa nyingi tu. Inatakiwa bank nzima ifutwe na mali zake kurudishwa kwa wananchi.

Bank M ni ufisadi kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Nashangaa Mkono hata anaendelea kuwa mbunge.

Ikibidi ifike mahala wananchi wasusie makampuni yote ambayo yamehusika katika kutuibia, hii bank ni moja ya hayo makampuni.
 
Wameanza kutoana kafara.
Wamemtoa kafara Muhindi zamu yao ikifika watagoma kuwa kafara hapo ndipo Genge zima la Benki M itabidi liangamie.
Mkapa na Mkono wote wako kwenye list ya Kikosi cha kwanza cha Mafisadi, Pamoja na mkono kufichama nyuma ya kampuni yake ya sheria na Mkapa kufichama nyuma ya katiba, siku inakuja siku ambayo watatambua kwamba Ufisadi haulipi.

Hawasomi Dalili Za Nyakati
 
Benki ile imejaa mafisadi na hakuna aliyeko salama .Kuanzia Mukono hadi Mkapa na kusema Mhindi ana kashfa nyingi nasema ni twist na wamesha mdhulumu maana kakimbia na hawezi kurudi Tanzania tena .
 
Mimi nadhani ipo haja kubwa sana ya kuirudisha ile taarifa nzima ya Mafia.. Hawa kina Jeetu na wamiliki wote wa Benki M wasije fikiria sisi tumesha sahau na tumelala.

Haiwezekani benki hii kuendelea kufanya kazi ikiwa imeshiriki sana ktk uhujumu wa Uchumi wetu, taarifa kama ile ni muhimu na kama nakumbuka vizuri nafikiri Mzee 6 aliikataa Bungeni kwa madai kuwa ni habari za mtandaoni, sasa baada ya kudhihirisha mengi mazito na yenye ukweli nadhani nitamwomba Dr. Slaa aiwakilishe tena bungeni ama kwa waziri mkuu wetu - FBI.
 
The whole working of our government organs on National security are questionable. This nation has got no proper governance; how can you announce the culprits even before zeroing them? Huu ni ushuhuda mkubwa hawa mafisadi wanalindwa na serikali yetu hii hii ambayo inatuambia ati hawa ni wezi! Hivi kweli mkubwa wa nchi anaenda ku-anounce kuwa hawa watu ni wezi, inatakiwa washikwe, ana hata baada ya siku 20 ya kutangazwa, hata watu hao bado wako huru; are we sure we are safe in this country?
 
Interested Observer,
how can you announce the culprits even before zeroing them?
ONLY IN TANZANIA..
A Prime minister resign with full honor after the fact!..

Unajua tena tunatumia kifungu cha sheria ya IKULU kisemacho:- Yaliyopita sii ndwele tugange yajayo!
 
Naibu Gavana wa BoT, Enos Bukuku aliliambia gazeti hili kuwa Jeetu Patel ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Noble Group inayomiliki pia kampuni ya NIL ambayo baada ya kujitoa inapendelea kuuza hisa zake zote kwa Tarek Al-Asharam raia wa Falme za Kiarabu (UAE).

Nadhani iwapo benki kuu wanataka kurejesha heshima, hawana budi kutoruhusu uhamishwaji wa hisa hizo kwenda kwa kampuni ya UAE. Yawezekana hii ni money laundering ya Jeetu kwa kutumia udhaifu uliopo katika sheria zetu unaohusu kulinda mali binafsi. Kwa sasa ni vema wakasimamisha 'any financial transactions' zihusuzo watuhumiwa wa EPA
 
Interested Observer,

ONLY IN TANZANIA..
A Prime minister resign with full honor after the fact!..

Unajua tena tunatumia kifungu cha sheria ya IKULU kisemacho:- Yaliyopita sii ndwele tugange yajayo!
Awamu hii yaliyopita ni ndwele...!
 
Mimi nadhani ipo haja kubwa sana ya kuirudisha ile taarifa nzima ya Mafia.. Hawa kina Jeetu na wamiliki wote wa Benki M wasije fikiria sisi tumesha sahau na tumelala.

Haiwezekani benki hii kuendelea kufanya kazi ikiwa imeshiriki sana ktk uhujumu wa Uchumi wetu, taarifa kama ile ni muhimu na kama nakumbuka vizuri nafikiri Mzee 6 aliikataa Bungeni kwa madai kuwa ni habari za mtandaoni, sasa baada ya kudhihirisha mengi mazito na yenye ukweli nadhani nitamwomba Dr. Slaa aiwakilishe tena bungeni ama kwa waziri mkuu wetu - FBI.
Sioni wapinzani wanaosimama kwenye hoja nyeti za kitaifa kama hizi...wao wanasubiri kauli za Rais wazitolee matamko tweeter.
VIVA JPM VIVA JPM...THIS IS BUSINESS UNUSUAL!!
 
And 10yrs later the House of Cards collapsed. Naikumbuka na kuikosa sana JF ya kitambo. Wakati wadau/members tulikuwa tunachambua mada kwa kina kutumia Hoja.
 
Anayetuhumiwa ufisadi BoT aenguliwa Benki M
Shadrack Sagati
Daily News; Tuesday,February 19, 2008 @02:18

MMOJA wa watu wanaodaiwa kuhusika na ufujaji wa mabilioni ya fedha za umma kutoka Benki Kuu (BoT), Jayant Kumar Patel (Jeetu Patel) ameenguliwa kwenye umiliki na ukurugenzi wa Benki M, HabariLeo imebaini.

Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili imezipata zinasema kuwa benki hiyo imeondoa jina la ukurugenzi wa Jeetu. Patel alikuwa mmoja wa wamiliki wa benki hiyo iliyoanzishwa mwaka jana kupitia kampuni ya Noble Azania Investments Limited (NAIL) iliyokuwa na asilimia 20 ya hisa za benki hiyo wakati ikianzishwa.

Mmoja wa wamiliki wa benki hiyo, Nimrod Mkono amelithibitishia gazeti hili kuwa Patel ameondolewa ukurugenzi wa benki hiyo. Kwa sasa Jeetu hayupo nchini na kuna minongono kwamba huenda ametoroka.

Licha ya kutotaja lini wamemwondoa kwenye ukurugenzi Mkono alisema; Hilo jambo siyo siri tena kwamba siyo mkurugenzi wa benki yetu tena. Siyo mkurugenzi tenatumeona hatuwezi kuwa na mtu ambaye ana kashfa nyingi kiasi hicho, alisema Mkono ambaye pia hakutaka kueleza kama Jeetu pia ameondolewa hisa zake kweye umiliki wa benki hiyo.

Habari za hisa au mali zake mahali ziliko mimi sijui maana hazinihusu, sijui hizo hisa zake kama kampa mke wake au mtoto wake au kawapa Takukuru (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa) sijui. Waulizeni Benki Kuu ndiyo waratibu wa mambo ya benki, alisema Mkono alipozungumza na mwandishi wa habari hizi.

Tangu benki M ianzishwe zimekuwapo tuhuma mbalimbali kuwa imeanzishwa na watu wenye tuhuma mbalimbali akiwamo Jeetu Patel anayetuhumiwa kuhusika na wizi wa mabilioni ya fedha katika Benki Kuu ya Tanzania.

Kampuni zake tisa zilituhumiwa kuhusika na wizi wa takribani Sh bilioni 133 kupitia Akaunti ya Ulipaji Madeni Nje (EPA). Kwa mujibu wa sheria ya benki ya mwaka jana, leseni ya kufungua na kuendesha benki haiwezi kutolewa kwa mtu mwenye historia au rekodi ya makosa ya jinai, kufilisika, kukosa uaminifu au hujuma kwa serikali.

Kifungu cha 12 cha sheria za benki na taasisi za fedha kinasema mtu anakoma kuwa mkurugenzi na mmiliki wa benki iwapo atabainika kuwa amefilisika au atakapotiwa hatiani kwa makosa ya kughushi au ya kutokuwa mwaminifu. Katika kifungu hicho pia inaelezwa kuwa mtu anakoma kuwa mkurugenzi wa benki iwapo ataondolewa na bodi ya benki husika.

Benki M ilianzishwa Februari 21 mwaka jana ikiwa na mtaji wa Sh bilioni 6.5. Benki hiyo ambayo hufanya kazi hadi usiku siku zote saba za wiki kwa sasa ina tawi moja katika barabara ya Nyerere.

Wamiliki wa benki hiyo kwa mujibu wa usajili wake ni Jeetu Patel kupitia kampuni ya Noble Azania Investments Ltd, Vimal Mehta kupitia kampuni ya Negus Holding Ltd na Fedha Rashid ambaye anamiliki kampuni ya Africarriers Ltd. Mkono ambaye ni mwanasheria maarufu nchini alishatamka hadharani kuwa benki hiyo ni ya kwake na anamiliki hisa kupitia kampuni yake ya Equity & Allied Limited.

Pia kuna wamiliki wengine wanaotajwa ambao ni Sanjeev Kumar, mtaalamu wa mambo ya benki na Bhaskaran Nair anayetambulishwa kama mfanyabiashara. Wanahisa hao wanamiliki benki hiyo katika mchanganuo ufuatao: Negus Holdings Ltd (Sh bilioni 1.3b), Noble Azania Investments Ltd (Sh bilioni 1.3b), Africarriers Ltd (Sh bilioni 1.3), Equity and Allied Limited (Sh bilioni 1.3), Kumar (Sh milioni 650) na Nair (Sh milioni 650). Kila hisa ya benki hiyo ina thamani ya Sh 1,000.

Benki Kuu (BoT) kwa upande wake imethibitisha kupokea maombi kutoka Benki M ya kutaka kuruhusiwa kufanya mabadiliko kadhaa katika wanahisa wake. Kwa mujibu wa benki hiyo mabadiliko hayo ya wanahisa yanawahusu wanahisa mbalimbali akiwamo mwanahisa ajulikanaye kwa jina la Noble Azania Investments Limited (NAIL) anayemiliki asilimia 20 katika benki M.

Naibu Gavana wa BoT, Enos Bukuku aliliambia gazeti hili kuwa Jeetu Patel ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Noble Group inayomiliki pia kampuni ya NIL ambayo baada ya kujitoa inapendelea kuuza hisa zake zote kwa Tarek Al-Asharam raia wa Falme za Kiarabu (UAE).

Bukuku alisema kupelekwa kwa maombi hayo Benki Kuu kutokana na matakwa ya kisheria chini ya sheria za benki ya mwaka 2006 na kanuni za taasisi za fedha ya mwaka 1997. Alisema maombi ya benki hiyo kwa sasa yanafanyiwa tathmini na BoT kwa kufuata vifungu na kanuni zilizo ndani ya sheria.

Tathmini hiyo itakapokamilika Benki Kuu itatoa uamuzi wa ama kuridhia au kutoridhia mabadiliko ya wanahisa ambayo BML inakusudia kuyafanya. Patel anatajwa kumiliki kampuni tisa ambazo zilitumika kuiba mabilioni ya fedha katika BoT zikiwamo kampuni sita alizosajili kwa siku moja ambazo ni Bencom Internationa Ltd, B. V Holdings Ltd, Venus Hotels Ltd, V.B Associates Company Ltd, Bina Rosort Lt na Bora Hotels & Apartment. Kampuni zake nyingine zinazotajwa kutumika kwenye ufisadi huo ni Maltan Mining Company, Ndovu Soaps Ltd na Navy Cut Tobacco Tanzania Ltd.

Makampuni hayo yako chini ya mwavuli wa Noble Azania Group ambayo Jeetu ni mmiliki wake Anadaiwa pia kumiliki kampuni katika miji ya London, Dubai na anadhaniwa kushikilia hati nyingi za kusafiria kwa majina mbalimbali. Historia ya Jeetu Patel nchini katika nyanja za biashara inaanzia mwaka 1978 wakati huo akijulikana kama muuzaji wa vipuri vya magari Dar es Salaam.

Chini ya kampuni hiyo ya familia iliyojulikana kama Azania Investment and Management Services Ltd (AIMS) amefanikiwa kuwa mfanyabiashara mkubwa wa kimataifa anayemiliki kampuni nyingi, kati ya hizo nyingine zikidaiwa kujishughulisha na biashara tata.

AIMS ilivyozidi kupanuka, iliingia katika kilimo kwa kuanza na shamba la hekta 1,500 huko Kimamba, wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro, chini ya usimamizi wa kampuni tanzu ya Azania Agriculture akianzia na tumbaku, miwa na mahindi.

Mwaka 1980, alinunua hekta 22,000 kwa ajili ya kilimo cha mkonge kutoka Mamlaka ya Mkonge Tanzania (TSA) huko Mvomero, Kilosa na baadaye viwanda vya kusindika matunda vya Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC) wilayani Korogwe.

Mkono aliwahi kunukuliwa akisema kuwa Benki M imeanzishwa iwakomboe Watanzania. Alisisitiza kuwa lengo la kuanzishwa kwake ni kutaka kuwawezesha Watanzania kuweka fedha katika benki ambazo wamiliki wake ni Watanzania wenyewe.
Rudi nyumbani pamenoga
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom