BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,087
Anayetuhumiwa ufisadi BoT aenguliwa Benki M
Shadrack Sagati
Daily News; Tuesday,February 19, 2008 @02:18
MMOJA wa watu wanaodaiwa kuhusika na ufujaji wa mabilioni ya fedha za umma kutoka Benki Kuu (BoT), Jayant Kumar Patel (Jeetu Patel) ameenguliwa kwenye umiliki na ukurugenzi wa Benki M, HabariLeo imebaini.
Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili imezipata zinasema kuwa benki hiyo imeondoa jina la ukurugenzi wa Jeetu. Patel alikuwa mmoja wa wamiliki wa benki hiyo iliyoanzishwa mwaka jana kupitia kampuni ya Noble Azania Investments Limited (NAIL) iliyokuwa na asilimia 20 ya hisa za benki hiyo wakati ikianzishwa.
Mmoja wa wamiliki wa benki hiyo, Nimrod Mkono amelithibitishia gazeti hili kuwa Patel ameondolewa ukurugenzi wa benki hiyo. Kwa sasa Jeetu hayupo nchini na kuna minongono kwamba huenda ametoroka.
Licha ya kutotaja lini wamemwondoa kwenye ukurugenzi Mkono alisema; Hilo jambo siyo siri tena kwamba siyo mkurugenzi wa benki yetu tena. Siyo mkurugenzi tena tumeona hatuwezi kuwa na mtu ambaye ana kashfa nyingi kiasi hicho, alisema Mkono ambaye pia hakutaka kueleza kama Jeetu pia ameondolewa hisa zake kweye umiliki wa benki hiyo.
Habari za hisa au mali zake mahali ziliko mimi sijui maana hazinihusu, sijui hizo hisa zake kama kampa mke wake au mtoto wake au kawapa Takukuru (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa) sijui. Waulizeni Benki Kuu ndiyo waratibu wa mambo ya benki , alisema Mkono alipozungumza na mwandishi wa habari hizi.
Tangu benki M ianzishwe zimekuwapo tuhuma mbalimbali kuwa imeanzishwa na watu wenye tuhuma mbalimbali akiwamo Jeetu Patel anayetuhumiwa kuhusika na wizi wa mabilioni ya fedha katika Benki Kuu ya Tanzania.
Kampuni zake tisa zilituhumiwa kuhusika na wizi wa takribani Sh bilioni 133 kupitia Akaunti ya Ulipaji Madeni Nje (EPA). Kwa mujibu wa sheria ya benki ya mwaka jana, leseni ya kufungua na kuendesha benki haiwezi kutolewa kwa mtu mwenye historia au rekodi ya makosa ya jinai, kufilisika, kukosa uaminifu au hujuma kwa serikali.
Kifungu cha 12 cha sheria za benki na taasisi za fedha kinasema mtu anakoma kuwa mkurugenzi na mmiliki wa benki iwapo atabainika kuwa amefilisika au atakapotiwa hatiani kwa makosa ya kughushi au ya kutokuwa mwaminifu. Katika kifungu hicho pia inaelezwa kuwa mtu anakoma kuwa mkurugenzi wa benki iwapo ataondolewa na bodi ya benki husika.
Benki M ilianzishwa Februari 21 mwaka jana ikiwa na mtaji wa Sh bilioni 6.5. Benki hiyo ambayo hufanya kazi hadi usiku siku zote saba za wiki kwa sasa ina tawi moja katika barabara ya Nyerere.
Wamiliki wa benki hiyo kwa mujibu wa usajili wake ni Jeetu Patel kupitia kampuni ya Noble Azania Investments Ltd, Vimal Mehta kupitia kampuni ya Negus Holding Ltd na Fedha Rashid ambaye anamiliki kampuni ya Africarriers Ltd. Mkono ambaye ni mwanasheria maarufu nchini alishatamka hadharani kuwa benki hiyo ni ya kwake na anamiliki hisa kupitia kampuni yake ya Equity & Allied Limited.
Pia kuna wamiliki wengine wanaotajwa ambao ni Sanjeev Kumar, mtaalamu wa mambo ya benki na Bhaskaran Nair anayetambulishwa kama mfanyabiashara. Wanahisa hao wanamiliki benki hiyo katika mchanganuo ufuatao: Negus Holdings Ltd (Sh bilioni 1.3b), Noble Azania Investments Ltd (Sh bilioni 1.3b), Africarriers Ltd (Sh bilioni 1.3), Equity and Allied Limited (Sh bilioni 1.3), Kumar (Sh milioni 650) na Nair (Sh milioni 650). Kila hisa ya benki hiyo ina thamani ya Sh 1,000.
Benki Kuu (BoT) kwa upande wake imethibitisha kupokea maombi kutoka Benki M ya kutaka kuruhusiwa kufanya mabadiliko kadhaa katika wanahisa wake. Kwa mujibu wa benki hiyo mabadiliko hayo ya wanahisa yanawahusu wanahisa mbalimbali akiwamo mwanahisa ajulikanaye kwa jina la Noble Azania Investments Limited (NAIL) anayemiliki asilimia 20 katika benki M.
Naibu Gavana wa BoT, Enos Bukuku aliliambia gazeti hili kuwa Jeetu Patel ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Noble Group inayomiliki pia kampuni ya NIL ambayo baada ya kujitoa inapendelea kuuza hisa zake zote kwa Tarek Al-Asharam raia wa Falme za Kiarabu (UAE).
Bukuku alisema kupelekwa kwa maombi hayo Benki Kuu kutokana na matakwa ya kisheria chini ya sheria za benki ya mwaka 2006 na kanuni za taasisi za fedha ya mwaka 1997. Alisema maombi ya benki hiyo kwa sasa yanafanyiwa tathmini na BoT kwa kufuata vifungu na kanuni zilizo ndani ya sheria.
Tathmini hiyo itakapokamilika Benki Kuu itatoa uamuzi wa ama kuridhia au kutoridhia mabadiliko ya wanahisa ambayo BML inakusudia kuyafanya. Patel anatajwa kumiliki kampuni tisa ambazo zilitumika kuiba mabilioni ya fedha katika BoT zikiwamo kampuni sita alizosajili kwa siku moja ambazo ni Bencom Internationa Ltd, B. V Holdings Ltd, Venus Hotels Ltd, V.B Associates Company Ltd, Bina Rosort Lt na Bora Hotels & Apartment. Kampuni zake nyingine zinazotajwa kutumika kwenye ufisadi huo ni Maltan Mining Company, Ndovu Soaps Ltd na Navy Cut Tobacco Tanzania Ltd.
Makampuni hayo yako chini ya mwavuli wa Noble Azania Group ambayo Jeetu ni mmiliki wake Anadaiwa pia kumiliki kampuni katika miji ya London, Dubai na anadhaniwa kushikilia hati nyingi za kusafiria kwa majina mbalimbali. Historia ya Jeetu Patel nchini katika nyanja za biashara inaanzia mwaka 1978 wakati huo akijulikana kama muuzaji wa vipuri vya magari Dar es Salaam.
Chini ya kampuni hiyo ya familia iliyojulikana kama Azania Investment and Management Services Ltd (AIMS) amefanikiwa kuwa mfanyabiashara mkubwa wa kimataifa anayemiliki kampuni nyingi, kati ya hizo nyingine zikidaiwa kujishughulisha na biashara tata.
AIMS ilivyozidi kupanuka, iliingia katika kilimo kwa kuanza na shamba la hekta 1,500 huko Kimamba, wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro, chini ya usimamizi wa kampuni tanzu ya Azania Agriculture akianzia na tumbaku, miwa na mahindi.
Mwaka 1980, alinunua hekta 22,000 kwa ajili ya kilimo cha mkonge kutoka Mamlaka ya Mkonge Tanzania (TSA) huko Mvomero, Kilosa na baadaye viwanda vya kusindika matunda vya Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC) wilayani Korogwe.
Mkono aliwahi kunukuliwa akisema kuwa Benki M imeanzishwa iwakomboe Watanzania. Alisisitiza kuwa lengo la kuanzishwa kwake ni kutaka kuwawezesha Watanzania kuweka fedha katika benki ambazo wamiliki wake ni Watanzania wenyewe.