Anayetuhumiwa kuua watu wawili katika nyumba ya wageni Tanga anaswa

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
.
23031537_10155877133874339_6504411881303844193_n.jpg

Mtuhumiwa huyo alikamatwa Tunduma wakati akifanya jaribio la kutoroka


Tanga.Mkazi wa Kijiji cha Bulwa Tarafa ya Amani Wilayani Muheza, Ismail Yahaya (41) aliyekamatwa Tunduma wiki iliyopita akifanya jaribio la kutaka kutoroka nchini, hatimaye amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi jijini Tanga na kusomewa mashtaka mawili ya mauaji.

Ismail ambaye ni mganga wa jadi alifikishwa mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi Tanga, Crisencia Kisongo akituhumiwa kuwaua Ibrahim Ali na Benedictor John katika nyumba ya kulala wageni.

Ilidaiwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali Rebeca Msalangi mbele ya hakimu huyo kuwa mshtakiwa huyo alifanya mauaji hayo Septemba 25 mwaka huu katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo Bomai Inn iliyopo barabara ya 20 jijini hapa.

Wakili huyo wa Serikali aliendelea kudai shtaka la kwanza linalomkabili mshtakiwa huyo ni kuwa Septemba 25 alimuua Ibrahim Ali na kisha kumfunga kamba. Shitaka la pili kwa mujibu wa mwendesha mashtaka huyo ni kwamba Septemba 25 mwaka huu mshtakiwa huyo alimuua Benedictor John na kasha kumfunga kamba.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, hakimu Cresencia alisema kutokana na kesi hiyo kuwa ya mauaji, mshtakiwa hakustahili kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kisheria hadi itakapofikishwa ngazi ya mahakama kuu.

"Kwa sababu hiyo huwezi pia kupewa dhamana kwa hiyo utakwenda Rumande," alisema hakimu huyo wakati akiahirisha kesi hiyo hiyo hadi itakapotajwa tena Novemba 14 mwaka huu

Chanzo: Mwananchi
 
Huyu mganga naye ovyo kabisa kama kweli aliwaua hao watu kwanini asingekodi kirikuu na kuwatupa baharini ili wazee wa "matamko" wapate point za kuilaumu serikali"
 
Wahusika wa matukio mengine yote wananaswa. Inakuwaje wale wa lisu mpk sasa hawajajulikana? Au alikuwa akitaka kujiua mwenyewe?
 
Wahusika wa matukio mengine yote wananaswa. Inakuwaje wale wa lisu mpk sasa hawajajulikana? Au alikuwa akitaka kujiua mwenyewe?


Tatizo dereva hajakwenda kuripoti Polisi. Hebu mshawishi Dereva akatoe ripoti Polisi - ili mambo kama haya yaendelee. Kama hapo unaona watu wa ile Guest House wametoa ushirikiano - jamaa amekamatwa. Nina hakika Dereva akitoa ushirikiano - Polisi wataweza pia kuwakamata na hao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom