Anayetuhumiwa kutoboa macho Buguruni DSM apandishwa Kizimbani

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,077
17,208
14523301_1243167415747250_7543419503409346308_n.png

Mkazi wa Buguruni kwa Mnyamani anayetuhumiwa kuwachoma watu visu na kisha kuwatoboa macho, Salum Henjewele maarufu kama Scorpion amepandishwa kizimbani na katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala na kusomewa tena shtaka la unyang'anyi wa kutumia silaha.

Scorpion ambaye alikamatwa baada ya kumchoma visu na kisha kumtoboa macho, Ally, mkazi wa Mabibo Hostel, alipandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Septemba 23, mwaka huu.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Adolf Sachore leo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na upande wa mashtaka umeieleza Mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.


Chanzo: Mwananchi

----------
MKAZI wa Machimbo Yombo jijini Dar es Salaam, Salum Njwele (34) maarufu kama Scorpion, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashitaka ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kumtoboa macho yote mawili Said Mrisho.

Scorpion alifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Adelf Sachore na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serikali, Munde Kalombola.

Akisoma mashitaka hayo, Kalombola alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Septemba 6, mwaka huu eneo la Buguruni Sheli wilaya ya Ilala.

Munde alidai, Njwele aliiba mkufu rangi ya fedha wenye uzito wa gramu 34 ikiwa na thamani ya Sh 60,000, bangili na fedha taslimu Sh 331,000 vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya Sh 476,000 mali ya Mrisho.

Kalombola alidai kuwa mshitakiwa kabla na baada ya wizi huo, alimchoma kisu machoni, tumboni na mabegani mlalamikaji ili ajipatie mali hizo.

Hata hivyo, upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na upande wa mashitaka uliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutaja.

Hakimu Sachore aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 19, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena. Mshitakiwa alirudishwa rumande kutokana na mashitaka yanayomkabili kutokuwa na dhamana.


Chanzo: HabariLeo
 
Issue huyu ametoka kwenye vyombo vya habari
Lakini wapo ambao hawatoi macho ila ni wahalifu wanaofahamika.
Na kila siku limekuwa likielezwa,sasa mpaka mtu atolewe macho ndio watu tena iwe habari kwenye mitandao kila hatua inayochukuliwana Polisi.

Huyu alianza kidogo kidogo mpaka akawa sugu,sasa wajue kuna underground nao wanakomaa huko na wao watakuwa masugu.Muhim ni kuanza chini sio kusubiria mpaka mtu akubuhu kwa uhalifu.

Yule ndio kaishampa ulemavu mwenzie,hata wakimhukumu kifo kwa mhusika haimsaidii chochote.
Vijana wenye mchezo wa kihalifu wapo wengi na maeneo yao yanajulikana
 
Nilitaka kuona picha yake,yupoje?,yaani alimjeruhi jamaa visu mwili nzima na kumpofua macho?,na jamaa alishindwa kujilinda na watu kumgwaya?,...wazee tupunguze bia tufanye mazoezi kujilinda...
 
Huwa anayafanyia nini hayo macho, au ni kishirikina zaidi mana sioni faida ya kumtoboa mwenzio macho...ili iweje kwa mfano.
 
Back
Top Bottom