Anayetuhumiwa kutoa rushwa ya Milioni 90 kwa Lukuvi afikishwa Mahakamani

View attachment 825236
Leo August 2,2018 mchana Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imempandisha kizimbani Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Steal Group. Co.ltd na Kiluwa Free Processing Zone, Mohamed Kiluwa (50) kwa tuhuma za kutoa rushwa ya Shilingi Milioni 90 kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi.

Mshtakiwa huyo amepandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi na kusomewa shtaka moja la kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Akisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Shaidi, Wakili wa Serikali Mkuu kutoka TAKUKURU, Maghela Ndimbo amedai July 16,2018 kati ya saa 6 na 8 mchana mshtakiwa huyo akiwa Mkurugenzi wa kampuni hizo mbili alitoa rushwa ya Dola za kimarekani 40,000 sawa na Sh. Milioni 90 kwa Waziri Lukuvi.

Wakili Ndimbo amedai mshtakiwa huyo alitoa fedha hizo kwa lengo la kutowasilisha hati ya umiliki wa kiwanja namba 57 ‘Block B’ Kikongo na ‘Block D’ Disunyura kilichopo eneo la viwanda Kibaha mkoani Pwani.

Baada ya kusoma shtaka hilo, Wakili Ndimbo ameiomba mahakama kuwapangia tarehe ya kutajwa kwa shauri hiyo na kuongeza kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na hawana pingamizi kuhusiana na mshtakiwa huyo kupewa dhamana.

Naye Wakili Upande wa Utetezi Imani Madega amedai kuwa kwa kuwa upande wa mashtaka hauna pingamizi na dhamana dhidi ya mshtakiwa wanaiomba mahakama itoe dhamana kwa kuzingatia masharti.

Hakimu Shaidi amesema ili mshtakiwa huyo apate dhamana anatakiwa kuwa na wadhamini 2 na mmoja atoe fedha taslimu mahakamani hapo kiasi cha Sh. Milioni 45 na kama hana awasilishe hati ya mali isiyo amishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Masharti ambayo upande wa utetezi uliyatekeleza na mshtakiwa akaachiwa kwa dhamana. Kesi hiyo imeahirishwa hadi August 15,2018.
Takukuru hawana mawakili wa serikali kwasababu hawapo chini ya Attorney General, kwa uelewa wangu huyo atakuwa ni mwendesha mashitaka mkuu wa takukuru. they don't represent the attorney General ndio maana sio mawakili wa serikali. tafuteni definition ya wakili wa serikali ni nani.
 
Jamaa amekosea timing kweli kweli. Rushwa?, Serikali hii?..Sali sala zote usikutwe na yaliyomkuta huyu ukiamua kupenyeza rupia penye udhia

Najaribu pia kutafakari kiasi cha fedha za Aina hii zilizowahi kutolewa na kupokelewa na wenye nyadhifa kama za Mh. William huko nyuma.
Nyie watu kila siku acheni porojo! Eti serikali hii... serikali ipi?! Si ndo serikali hii ambayo hata JPM siku moja alitamka hadharani kwamba mmoja wa ma-RC ni mwizi aliyekusudia kuiibia serikali kwa kukwepa kodi?! Leo hii tena tunaona kumbe waziri mwandamizi wa serikali hiyo hiyo alimpiga mtu roba ili amwibie madolari raia!!!

Juzi juzi tu hapa tumeona mkuu wa serikali hii akinywa juice na mtuhumiwa namba moja ya maufisadi makubwa nchini na wiki kadhaa baadae, tunaona kaka wa mtuhumiwa huyo wa maufisadi akihukumiwa kutoa faini kwa kesi ya uhujumu wa uchumi, ujangiri, na utakatishaji fedha!!!

Yaani mhujumu uchumi anapigwa faini?

Yaani mpiga risasi tembo anapigwa faini?

Yaani mtakatishaji fedha anapigwa faini?!

Halafu bado mnapiga simulizi za "serikali hii!"
 
Back
Top Bottom