Anayetuhumiwa kumteka DR. Ulimboka azungumza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anayetuhumiwa kumteka DR. Ulimboka azungumza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Muke Ya Muzungu, Jul 4, 2012.

 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Askari anayetuhumiwa kumteka Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka, Kamishna wa Polisi Msaidizi (ACP), Ahmed Msangi, amehojiwa na kuzungumzia kilichotokea kuhusiana na tuhuma kwamba aliambiwa arejeshe simu ya mkononi na pochi ya Dk. Ulimboka.


  Akizungumza na Gazeti la JAMHURI, ACP Msangi alikiri kwenda katika wodi ya wagonjwa mahututi katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa nia ya kumhoji Dk. Ulimboka, ila akaeleza mshangao wake kutokana na habari zilizochapishwa mwishoni mwa wiki, kuwa aliambiwa arejeshe pochi na simu ya Dk Ulimboka kwa maana kuwa alivipora walipomteka.


  Vyombo vya habari mwishoni mwa wiki vilichapisha taarifa bila kutaja jina la askari anayetuhumiwa, lakini pia ukawa unasambazwa ujumbe mfupi kupitia simu za mkononi ambao ulisema hivi:


  "Kamanda Msangi aliyemkamata na kumtesa Dr. Ulimboka, yuko katika jopo la kuchunguza nini kilimtokea Dk. Ulimboka. Alipofika kumhoji Dk. Ulimboka alimwambia ‘Nirudishie simu na wallet yangu'. Kamanda Msangi taratibu akaondoka wodini kichwa chini. Kama wewe ni mpenda haki na unapinga ujinga na dhuluma, watumie ujumbe huu watu wengi kadri uwezavyo ili wamjue dhalimu aliyeongoza unyama huu," ulisema ujumbe huo unaosambazwa kupitia simu za mkononi.


  Tume ya Jeshi la Polisi iliyoundwa kuchunguza tukio la Dk. Ulimboka kutekwa nyara, kwa mujibu wa Kamanda Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, inaongozwa na Kamanda Msangi.

  Kamanda Msangi azungumza

  Jamhuri: Afande umetangazwa kuongoza hii Tume ya Polisi kuchunguza suala la Dk. Ulimboka, lakini taarifa zilisosambaa zinaonyesha Ulimboka alikwambia umerejeshee simu na wallet yake. Unalizungumziaje hili?

  Kamanda Msangi: Hata mimi nimesikia hizi taarifa, na zimenisikitisha mno. Naamini taarifa hizi zina malengo ya ziada. Si kweli kwamba nilishiriki kumteka Dk. Ulimboka na wala sijawahi kuwa na wazo hilo.

  Jamhuri: Ikiwa hukushiriki kumteka iweje wodini akwambie nirudishie simu yangu?


  Msangi: Kwanza ifahamike mimi huyu Dk. Ulimboka na mwenzake Dk. Deo nimewafahamu siku nyingi sana. Kwa maana hiyo ni mtu anayenifahamu vizuri tu. Kuna upotoshaji wa makusudi umefanywa ambao mimi nadhani una msukumo wa kisiasa.


  Alichosema Dk. Ulimboka nilipozungumza naye, ni kwamba simu moja ilidondoka, nyingine wale watu waliomteka wameichukua pamoja na wallet yake. Hivyo alikuwa ananitajia vitu vilivyopotea. Nilipomuuliza iwapo anakumbuka namba ya simu, aliniambia nikamuulize Dk. Deo. Sasa nashangaa mtu aliyepenyeza uongo huu kwamba alisema mimi ndiye niliyempora hivyo vitu… sielewi ni nani na ana malengo gani.

  Jamhuri: Haya unayasema wewe, hivi unadhani jamii itakuamini kwa kauli hizi, haitaonekana unajitetea tu?

  Msangi: Wakati anazungumza maneno haya, alikuwapo Profesa Museru ambaye ni Mkurugenzi wa MOI. Sina cha kuficha kamuulize tu, atakwambia alichosema Dk. Ulimboka. Yupo pia Dk. Deo, huyu ananifahamu na Dk. Ulimboka anasema walikuwa wote wakati anatekwa. Dk. Deo ananifahamu, akaulizwe iwapo mimi ndiye niliyemteka Dk. Ulimboka.

  Jamhuri: Tuhuma hizi zilianza kusambaa mapema tu Ijumaa. Je, wewe hukuwa na hofu kwenda pale MOI kumhoji Dk. Ulimboka?


  Msangi: Ndugu yangu, nchi hii ina askari wengi mno. Hivi mimi kwa akili ya kawaida naweza kushiriki kumteka Dk. Ulimboka kisha nikaenda wodini kumhoji? Hata katika akili ya kawaida ya binadamu hilo haliwezekani.


  Jamhuri: Hizi tuhuma zilizoelekezwa kwako ni nzito. Wewe ndiye uliyeteuliwa kuongoza Tume ya Uchunguzi wa tatizo hili. Je, unadhani uchunguzi utakaofanya utaaminiwa na wananchi ukitoa ripoti?

  Msangi:
  Mimi ninachokuhakikishia sikushiriki kumteka na si kweli kwa kila hali. Mambo kama haya yanakatisha tamaa. Kama tunaanza kuzushiana uongo kwa kiwango hiki, nchi hii sijui inaelekea wapi! Kimsingi imenikatisha tamaa mno. Wapo wanaosema nijiuzulu katika Tume hii lakini mimi nasema wakubwa wangu wamenipa kazi hii na watakaloamua nitalipokea.

  Hivi wewe gazeti lako likituhumiwa unaacha kuendelea kutafuta habari? Nitaendelea kufanya kazi hii kama nilivyoapa siku nilipohitimu mafunzo kwamba nitalitumikia taifa kwa uadilifu na uaminifu wa hali ya juu katika kiapo changu cha utii. Na hilo ndilo nitakaloendelea kufanya. Watu wanapenda kuharibiana maisha tu.

  Profesa Museru asema alichokisikia


  Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru, akizungumza na JAMHURI kuhusiana na sakata kwamba Dk. Ulimboka, alimweleza Kamanda Msangi arejeshe simu na wallet yake.

  Jamhuri: Profesa nimezungumza na Kamanda Msangi juu ya tuhuma zinazomkabili kuwa aliambiwa na Dk. Ulimboka amrejeshee simu na wallet yake, na akakutaja wewe kuwa ulikuwapo wakati wa mazungumzo hayo. Wewe nini ulichokisikia kuhusiana na tuhuma hizi.

  Profesa Museru: Mimi ndiye niliyempeleka pale wodini. Ni bwana mzuri tu. Nilimu-introduce (nilimtambulisha), akaanza mahojiano. Mimi hilo sikulisikia kwamba ameambiwa arejeshe simu na wallet, hilo sikulisikia.

  Jamhuri: Kuna habari kuwa Kamanda Msangi baada ya kuambiwa kauli hiyo alitoweka wodini bila kuaga akikwepa kipigo kama ilivyomtokea askari mwenzake siku mbili kabla. Je, unalizungumziaje hilo profesa?

  Profesa Museru: Nini? Kwamba alikimbia? Jamani nchi hii inakwenda pabaya. Mimi nilimsindikiza hadi nje ya wodi akapanda gari lake na kurejea ofisini kwake, sasa hilo la kukimbia limetokea wapi? Jamani ehee, mimi niseme katika hali kama hii sintofahamu zipo nyingi. Ni vyema kuchuja taarifa tunazozipata.

  Daktari asisitiza polisi wanahusika

  Gazeti la JAMHURI lilichukua jukumu la kumtafuta mmoja wa viongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, ambaye kwa sababu za kiusalama alikataa jina lake lisitajwe gazetini, lakini yeye alisisitiza kuwa polisi wanahusika na utekaji huo kwa asilimia 100.


  "Hivi unategemea leo Kamanda Msangi kwa akili ya kawaida ya binadamu anaweza akakiri kuwa alishiriki kumteka? Taarifa tulizonazo ni kwamba polisi ndiyo waliomteka Dk. Ulimboka na kumfanyia unyama huu.

  "Ndiyo maana tunasema polisi tayari wanatuhumiwa hivyo hawana haki ya kuchunguza suala hili. Tunataka ateuliwe Jaji, na Tume iwe na wajumbe huru wasiofungamana na chama, taasisi au siasa za nchi hii, wachunguze kwa kina na kutoa taarifa huru," alisema Daktari huyo.


  Alisema mbinu iliyotumika kumtesa Dk. Ulimboka hutumiwa na majasusi wenye mafunzo ya hali ya juu, ambayo hata majambazi wa kawaida hawawezi kuzifahamu.


  "Unapomg'oa mtu kucha au jino bila kumpiga ganzi, unashtua mishipa ya fahamu kumfanya anayeteswa afahamu kuwa kinachofuatia dhahiri ni kifo, na hivyo kulazimika kusema ukweli wote anaojua juu ya suala analohojiwa. Mtu akishang'olewa jino au kucha na asiseme chochote, basi unajua fika kuwa hakuna anachokifahamu zaidi ya alichokisema.


  "Hii inatokana na nini? Hicho kinatokana na ukweli kwamba baada ya kung'olewa kimojawapo kati ya hivyo, kinachofuata ni kupoteza fahamu. Sekundi chache kabla ya kupoteza fahamu nati za mishipa ya fahamu huwa zinafunguka na kusema kila kilicho cha kweli bila wewe unayeteswa kujua. Ndiyo maana nasema vyombo vya dola ndivyo vilivyohusika. Haya ni mateso ya kitaalamu," alisema daktari huyo.


  Rais wa Chama cha Madaktri Tanzania, Dk. Namala Mkopi, alipopigiwa simu na JAMHURI kueleza chochote anachokifahamu katika sakata hili, alipokea simu akasikiliza kisha akakata bila kujibu na hata alipopigiwa simu tena hakutaka kuipokea tena.

  Dk. Ulimboka apelekwa nje kwa matibabu

  Madaktari inaelezwa kuwa wameamua kumpeleka Dk. Ulimboka katika matibabu nchini India, ingawa kwa sababu walizosema ni za kiusalama hawakutaka kutaja ni hospitali gani aliyopelekwa.


  Jumanne wiki iliyopita, Dk. Ulimboka alitekwa na watu wasiofahamika hadi sasa na kupigwa, akang'olewa meno mawili na kucha mbili, kisha akatupwa katika msikiti wa Mabwepande baada ya kuwa ameteswa kupita kiasi.


  Dk. Ulimboka baada ya kuokotwa na wasamaria wema, alikaririwa na Radio Clouds akisema kuwa walipokuwa Kinondoni ndipo alipotekwa usiku wa saa 5:30.


  "Mara, katikati ya maongezi tukaona mtu anaongea na simu. Ghafla tukiwa tunasema tuagane, wakaja watu kama watano hivi na bunduki, wakasema wewe na yule bwana mko free (huru), tunakuchukua wewe (Dk. Ulimboka)," alieleza na kuongeza.


  "Sijakaa sawa, nikaona nimeshaburutwa nikaanguka kwenye lami, wakaniinua na kuniingiza kwenye gari nyeusi, lakini ilikuwa haina namba."

  Wananchi wataka uchunguzi huru

  Baadhi ya wananchi waliozungumza na JAMHURI huku wakionyesha hofu ya kutaja majina yao, walilituhumu Jeshi la Polisi kuwa linahusika moja kwa moja na tukio hili hivyo wakuu wa jeshi hilo wawajibike kuhakikisha ukweli unapatikana.


  "Ndugu yangu nawahurumia nyie wenye kutafuta habari hizi. Mnafanya kazi ya hatari. Tutazidi kuwaombea tu, muishi milele na Mungu awalinde. Hivi leo kwa mfano unaweza kwenda kumhoji Msangi kuwa unatuhumiwa kumteka Dk. Ulimboka? Ukitoka hapo anatuma vijana wake nao wanakuteka na wewe pia.

  "Naamini polisi walihusika kwa kiwango kikubwa na hivyo hawapaswi kushiriki uchunguzi huu. Hawa wanapaswa kupanda kizimbani kujitetea hivyo ni makosa kushiriki uchunguzi wao," alisema Mkazi wa Dar es Salaam.


  Mwananchi mwingine alisema chimbuko la mgogoro wa madaktari liko wazi. "Hawa wanadai mishahara mizuri na marupurupu sawa na wanavyopata wabunge wasiofanya kazi yoyote. Leo unadhani serikali inaona imeshikwa pabaya itawaacha waendelee kutamba tu? Thubutu. Kimsingi polisi wametumiwa. Hao waliowatumia ndiyo tunaotaka uchunguzi huru utueleze ni kina nani na kwa nia ipi," alisema Mkazi wa Arusha kwa njia ya simu.


  Hadi sasa madaktari katika hospitali za umma wamegoma kuendelea na kazi kutokana na mgogoro wa malipo kati yao na serikali, na hivi karibuni mgogoro huo umeshika kasi baada ya Dk. Ulimboka kutekwa na kuumizwa vibaya.

  Chanzo: Gazeti la Jamhuri Jumanne, Julai 03, 2012
   
 2. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hana jipya atatundanganya kwa lipi tunajua na kufahamu nini alichokifanya
   
 3. Gwangambo

  Gwangambo JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 3,655
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Naenda zangu Love Connect, ntapigwa ban buree!!
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Jul 4, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Natamani nimpige hadi afe.
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ban ya nini wakati hii ni published news?
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Siku hizi digital itatuumbua wengi, sijui picha hii waliipataje na anayeonekana pichani ndiye mtuhumiwa au?
   
 7. Red Giant

  Red Giant JF-Expert Member

  #7
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 9,497
  Likes Received: 5,977
  Trophy Points: 280
  mbona analikicheko la kinafiki hata ni kikaa mbali na PC naliona kuwa ni cheko la mamba
   
 8. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  hiyo gazeti lazima ipigwe stop kusambazwa asubuhi,watasema bado uchunguzi unaendelea na siyo kutoa taarifa nusu nusu
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wamechelewa kwani gazeti hilo nakaza zilishasambaa mitaani. Wao walikazia macho magazeti yenu kufumua mazito kama Mwananchi, Tanzania Daima, kumbe wenzao wamewazunguka mbuyu kushtukia nakala zimejaa mitaaani.
   
 10. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #10
  Jul 4, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Tupeni taarifa wakuu. Mbona mnatubania, wengine tuko mbali. Nini kimeandikwa katika hilo gazeti?
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hii inaingia akilini kidogo..........

  Msangi hana jeuri ya kumteka mtu hadharani kwa mkono wake mwenyewe kisha akenda kumhoji.
   
 12. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #12
  Jul 4, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Kizungumkuti!!!
   
 13. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  Ngoja arudi afrika kusini aje awatambue wote
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Jul 4, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Anaweza asiwe yeye kama yeye lakini anaweza akawa mastermind. Na hata kama alikuwa ndiyo mastermind bado sidhani kama ataweza kukiri.

  Kwa vyovyote vile jeshi la polisi na serikali nzima ya CCM hawana credibility kwenye hili suala la Ulimboka.
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mbona alichozungumza "0"?

  Huyo kama kweli kazungumza basi si mtendaji. Mtendaji anazungumza?

  "if you have to shoot, shoot, don't talk" - The Good, The Bad and The Ugly.
   
 16. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Serikali ya CCM haiwezi kujitoa hata kidogo. Kama iliamuru, kama vikundi vilifanya kwa utashi wao wenyewe, kama ni vikundi nje ya serikali, bado serikali inatakiwa kujibu kwa sababu ndio yenye dhamana na maisha ya Mtanzania.

  Na hii kuwa hadi sasa wiki inakatika hakuna aliyekamatwa wakati tukio lilitokea kukiwa na mashahidi wa wazi kunatupa hisia kuwa wajumbe wa tume wanahusika kwa njia moja au nyengine


  Lakini bado haiondoi ukweli kuwa siku hizi imekuwa rahisi kwa watu kusambaza habari ambazo hazijathibitishwa. Kwa hali inavyokwenda, kuna siku raia asiye na hatia anaweza kuadhibiwa kwa makosa asiyoyatenda kwa sababu tu ya habari zisizothibitishwa. Hala hala mti na macho
   
 17. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #17
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  .....Kabla mwaka kuisha atazawadiwa alichoahidiwa...RPC!stay tuned!!
   
 18. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #18
  Jul 4, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  wamepata gazeti la kujisafishia.
   
 19. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #19
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Tutasubiri hadi hapo Dr. Ulimboka atakapotoa ukweli kwa kuwataja aliowatambua na hata kama huyo Msangi ikikana. Tutamwamini Ulimboka zaidi kuliko huyo Msangi. Let us pray ili kijana wetu arudi salama.
   
 20. Chizi Fureshi

  Chizi Fureshi JF-Expert Member

  #20
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,710
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Deo na Ulimboka watajakosana tu. Subirini.
   
Loading...