Anayetuhumiwa kumchoma kwa Pasi Msichana wa kazi aachiwa kwa dhamana

kamonga

Senior Member
Feb 13, 2008
170
195
Yaani nimeshangaa sana na haya yafuatayo
1. Hivi watu wana roho gani kwenda kumdhamini Amina Maige? yule aliyemla nyama mfanyakazi/ ndugu yake mwenyewe. Inawezekana vipi ukamdhamini mtu mwehu kama Amina?
2. Eti utetezi wa mahakama ni walikataa kumtoa kwa kuhofia maisha yake kwa kuwa kesi hio imegusa watu wengi' siriazly?? Kweli kabisa mimi nilidhani wangekataa kumtoa kwa sababu ni hatari kwa jamii nzima. Wanajuaje hata kula watu wengine'?? hata kumpima akili hakimu kashindwa kusema? mimi si mwanasheria ila kuna muda sheria zinavyo pinda pinda mie nachoka kabisa.
3. Such a case dhamana ni 3 million tu? basically ninaweza kukukula nyama hapa nikiwa ni 3m tu aka najitokea jela fresh'?' very disappointing.
4. Kwanza kuna haraka gani? na dhama hii wakati hata miezi mi3 haijafika mtoto watu akapimwe ukimwi nk nk
Hebu wanasheria mtujuze hapa sheria ilivyoenda?
5. Mi sio mdini ila mie hijabu na baibui zinanikera sana pale mtu akitumia kuficha maovu yake. leo Amina kavaa baibui na hijabu kajifunika gubigubi kuficha aibu yake....picha tulizoona kabl hata scarf alikua havai.... pretender in mkandamizaji voice.
Ameniharibia siku yangu yote huyu mla watu.:angry::angry:
============================== ==================

Anayetuhumiwa kumchoma kwa pasi msichana wa kazi aachiwa kwa dhamana.

Mahakama ya wilaya ya Kinondoni imemwachia kwa dhamana Bi. Amina Maige wa miaka 42 mkazi wa Mwananyamala anayetuhumiwa kwa kosa la kumng'ata na kumchoma kwa pasi binti yake wa kazi Yuster Kashinde kwa kipindi cha miaka miwili baada ya kutimiza masharti ya dhamana hiyo.

Dhamana hiyo imetolewa na hakimu mkazi Yohana Yongolo baada ya upande wa mashtaka kutimiza Masharti ya dhamana ambapo mshtakiwa alitakiwa kulipa milioni tatu ama kudhaminiwa na watu wawili wenye kazi inayotambuliwa na kuweza kuhakikisha usalama wa mtuhumiwa masharti ambayo waliweza kutimiza.

Wakili upande wa utetezi Emmanueli Agustino baada ya kutoa vielelezo vya kuishawishi mahakama kwa mtuhumiwa kupewa dhamana ametakiwa kuhakikisha kuwa mtuhumiwa atakuwa salama baada ya pingamizi la upande wa utetezi wa serikali kuhofia usalama wa mtuhumiwa kutokana na kesi hiyo kugusa watu wengi.

Mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani Juni mwaka huu akikabiliwa na shtaka la kumng'ata na kumchoma kwa pasi binti Yusta Kashinde mwenye umri wa miaka 20 na kumsababishia majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake .

Kesi hiyo inatarajia kuja tena mahakamani hapo Julai 22 kwaajili ya kusikilizwa.


Chanzo;ITV Tanzania
 
Last edited by a moderator:

Galadudu

JF-Expert Member
Jun 23, 2014
2,305
1,225
Mbona yule wa mwanza alomwagia maji ya moto mtoto wake akalazwa ICU pale bugando na baadae akampelekea sumu kwny juice,yule binti akafariki...jamaa hadi leo anadunda uswahilini tu bila hofu
 

Jamaa_Mbishi

JF-Expert Member
Jun 15, 2013
8,070
2,000
Mbona Luis Suarez yuko huru pamoja na meno yake makubwa vile yupo huru japo anafyonza watu damu? Ila kwa Bongo mi sishangai.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom