Anayeshindwa uchaguzi wa ndani CCM na kulalamikia rushwa ni mnafiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anayeshindwa uchaguzi wa ndani CCM na kulalamikia rushwa ni mnafiki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwawa, Oct 8, 2012.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Kila hatua ndani ya CCM ni rushwa, kila cheo ndani ya CCM ni rushwa maisha yeyote ya cheo ndani ya CCM ni rushwa. Karibu kila kiongozi ndani ya CCM katoa rushwa na kupokea rushwa. Rushwa yamekuwa maisha ya kawaida ya viongozi wa CCM na serikali yake.

  Tulipopiga kelele za rushwa za uchaguzi CCM ilibadili jina na kuita takrima, leo walioiita takrima wanajifanya wameonewa na kudhulumiwa. Wamelea na kuvumbua rushwa sasa inawala wenyewe kwa wenyewe wanalalama.

  Mfano Sumayi akiwa waziri mkuu ndio waliokuwa wenye uwezo wa kudhibiti na kutunga sheria kali dhidi ya rushwa tumuulize kwa miaka kumi kama waziri mkuu alifanya nini hakuona rushwa hakuishi na rushwa hakutoa na kupokea rushwa hakulea na kuenzi rushwa sasa inamla analia nini??

  Nachukia pale kiongozi anaposhindwa uchaguzi ndani ya CCM na kulia lia eti kuna rushwa. Tunawaambia wote ndani ya CCM wajue vyema chama chao kimejaa rushwa mwenye nia njema aondoke kwani hakuna haki bila rushwa. Viongozi walisimamishwa au kuondolewa kwa wizi, rushwa ndio vinara kwenye chaguzi za ndani za CCM. Hakuna maadili wala weledi wa mtu kuwa kiongozi wetu wote wananuka rushwa.

  Kuna rushwa za aina nyingi ila rushwa kubwa inayotumaliza kwa sasa ni rushwa ya madaraka, wote wanojifanya vinara wa kupiga kelele kuhusu rushwa ndani ya CCM hunyamazishwa kwa rushwa ya madaraka mfano Mwakyembe, Magufuli, sita nk kila mmoja anakula na kupokea rushwa ndani ya CCM

  Wananchi wawe macho sana na viongozi hawa watoa na wapokea rushwa pale wanapozidiana nguvu kujifanya eti wao ni wema.

  Lazima serikali ya CCM na watu wake iondolewe madarakani na wote wale wanaotoa na kupokea au walioneemeka kwa rushwa wafikishwe mbele ya sheria. Ni lazima mkurugenzi wa Takukuru awajibike kwa kushindwa kukamata watoa na wala rushwa za aina yote kwani taasisi hii inatumia fedha za walipa kodi bure kabisa.

  Rushwa ni adui wa haiki, ila kwa CCM rushwa ni mhimili wa haki na haki hununuliwa.

  Say No more Rushwa

  Chief Mkwawa wa Kalenga
  Tupigane na rushwa na tuwakatae kwa vitendo wala na watoa rushwa wa aina zote
   
 2. K

  Kibagata JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 773
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Mkuu umenena. wakizidiana ndo wanaita waandishi wa habari kulalama. Kwisha habari yenu magamba
   
 3. M

  Mpwechekule JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tusubiri fisadi litakalopitishwa na chama chao na je mafisadi wengine watamuunga mkono? Au watageukana? Sitabiri lakini hatua ambayo ccm imefikia hakika watatafunana tu!, ukiangalia sura ya sumae utajua hili ninalosema, nahisi vita vya panzi vitampa kunguru sherehe kuu
   
 4. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 180
  Huko musoma wametwangana na viti baada ya kuzidiana kwa rushwa na moro pia sosi itv
   
 5. Bolizozo

  Bolizozo Member

  #5
  Oct 8, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona hata Mheshimiwa sana Sumaye alipokuwa Waziri Mkuu aliidhinisha rushwa kwa kusema hiyo ni Takrima na sawa kutolewa. Amesahau?

  Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,649
  Likes Received: 82,379
  Trophy Points: 280
  ..Si ndio maana akaishia kubwabwaja tu badala ya kuwataja waliotoa na kupokea rushwa ili apigwe mweleka katika uchaguzi ni akina nani!? Anajua fika kwamba yeye mwenyewe si safi ndio maana akaishia kujiumauma tu.

   
 7. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Na hii yote inadhihirisha wazi kwamba Takukuru wanakula pesa ya kodi yetu Watanzania bure! Mimi sioni ni kwanini wanaendelea kuwepo!
   
 8. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  They promise them freedom, but they themselves are slaves of corruption. For whatever overcomes a person, to that he is enslaved.
   
 9. m

  mhondo JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Wanaolalamikia rushwa baada ya kushindwa nao wana nafasi katika kuilea rushwa. Kwanini huwa hawatoi taarifa/kulalamika mapema kabla ya kushindwa ili hatua zichukuliwe mapema?
   
 10. m

  mokti Member

  #10
  Oct 9, 2012
  Joined: Sep 20, 2012
  Messages: 70
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi kweli kwa CCM hakuna namna nyingine isipokuwa kutoa na kupokea rushwa. Katika historia hakuna chama chochote ambacho kimedumu kwa kuweka rushwa kama sehemu ya mkakati wake wa kuendelea. Hili linafahamika na kila mmoja wa CCM, inakuwaje sasa chama kinajikuta katika janga kama hili (downward spiral). Jibu ni dhahiri, greedy, unafiki na kujisahau. Wakati umefika wa kujitafakari, kujisafisha, na kuchukua hatua za maksudi za kujenga chama upya. Swali ni kuwa Hili linawezekana tena au kansa imefikia hatua ya mwisho? Tafakari, Haki Watanzania.
   
Loading...