TANZIA Anayesadikiwa kuwa MwanaJF afariki dunia

Ifikie hatua MTU kama hupendi tabia za mume urudi tu kwenu,kuliko unajua mume ni mlevi umekomalia kwenye Nyumba yake na mlango unamfungia.

Nao ni watoto wa wanawake wenzenu walipata uchungu kama muupatao. Pumzika Mkuu,pumzika Kamanda!
 
Kila nafsi itaonja umauti leo kwake kesho kwetu, mwenyezimungu ampunguzie adhabu za kaburini
 
Ukiona anakugomea kukufungulia mlango.
Tafuta housegirl muweke humo ndani
Na Moja ya majukumu yake ni kumfungulia baba mwenye Nyumba.

Wawe wanawasiliana pindi baba akikaribia kurudi
Kwa mwendo huo yeye atalala kwa amani na baba mwenye Nyumba hatolala nje.

Vifo vya namna hii umevikomesha
 
Hapo changamoto.. ila wanaume wasiokunywa kabisa wapo.


Me zamani nilikuwa nakunywa kiasi, nikaja date mtu hanywi pombe kabisa.
Akanirudisha kwenye mstari, nikaacha na mpk leo sijawahi hata kumiss
Usimuache mtalea watoto wasio walevi.
 
Duh, uyo mke wake atakua kwenye majuto Sana,kitendo Cha kufungua geti asingechukua ata dakika moja, Sasa ameshapoteza mume
Unaweza kuta amefurahi sana na hana hata chembe ya huzuni...anaona Mungu amemuondolea usumbufu.

Watu hawafanani.
 
Tumetoka kuongea jana
Tukatae waume walevi 😢

Tinsley Lenie
Temea chini mama mshukuru Mungu kwa kukuepusha!

Katika hali ya kuchumbiwa na kijana anayeishi mbali na wewe, waweza kumjua hobi zake kindaki ndaki, wakati wewe una muhu ya kuolewa uwatambie "wachawi" wako?

Na pia saazingine ulevi huanzwa ndani ya ndoa, hapo "Tukatae wanaume walevi" yako itasadifu namna gani, utavunja ndoa?
Lina hela? Kama lina hela usijemtibulia mazako mdogo
Mh!
 
Yani mm jamani Mume wangu akiwa nje siwezi kupata usingizi silalii mpk nihakikishe nimefungua mlango huwa nawaza mengi kweli. Wacha niufungue halafu ninune tuu. But kuliko kupigwa na majambazi aisee. Na kama mume sio mlevi na hajazoea kuja late siku ikiwa hivyo huwezi pata usingizi. So maybe huyo alizidi lakini huruma lazima ikuingie ukiwaza panya road na usiku una mambo mengi.
Ila hatuwezi hukumu hatujui kilichotokea
R.I.P
 
Mimi baba yangu alikua anakunywa sana na alikua anarudi usiku na mimi ndo alikua anapenda nimfungulie akifika mlangoni ataniita mimi japo nilikua nakwazika sana napata hasiraa sana nikawa nawaza why baba hawaamshi wengine.. na huwezi amini japo nilikua sipendi but nilikua silali usingizi hauji hadi nihakikishe namfungulia nilikua naogopa asije dhuriwa. Hivyo hyo ni tabia yangu mpk leo kwa husband japo yy si mnywaji ni mara moja moja akichelewa yupo huko siwezi lala mpk nifungue mimi naogopa ssna usiku na kama kuna mpendwa wangu nje hajaingia ndani au labda anasafiri usiku huwa napata shida.
 
Memba mwenzetu ametangulia mbele ya haki. Pengine nisingejisumbua kuripoti huu msiba lakini mazingira ya kifo chake ni ya kuhuzunisha na yenye mafunzo. Sijui username yake ya JF kwani tulikutana ''casually'' kwenye kilevi mwezi wa tatu mwaka huu tena siku moja tu. Katika maongezi alinijulisha kuwa yeye ni ''active member'' wa JF na anapenda sana kuchangia. Baada ya kilevi (maeneo ya Boko) tulipokuwa tunaondoka akanionyesha nyumbani kwake na mimi nikaondoka kurudi kwetu Msasani ninakoishi.

Fast forward, wiki kama mbili zilizopita nilirudi tena maeneo tuliyokutana kwenye mishe zangu. Nikaona msiba kwenye boma aliloniambia ni nyumba yake. Kuulizia kulikoni nikaambiwa ni yeye, mwenye nyumba amefariki. ''Eti'' alitoka kwenye kilevi usiku, akagonga geti, mke akagoma katukatu kumfungulia. Akachukua uamuzi wa kuruka ukuta. Kwa bahati mbaya akachomwa na moja ya nondo zilizoko kwenye geti la nyumba (nadhani wengi mnafahamu nondo zinazochongwa kama mkuki na kuwekwa juu ya kuta au geti ili kuzuia vibaka). Kwa bahati mbaya akavuja damu nyingi mpaka akapoteza maisha. RIP member.
du!!! wanawake watupa shida sana wanaume!!! R.I.P
 
Back
Top Bottom