Anayependa Kweli na Anayeigiza Kupenda: Nini Tofauti Kati Yao?

Ila usisahau kitu kimoja. Urafiki wa kawaidia kati ya watu wa jinsi mbili huwa ni wa pekee sana. Mara nyingi hawa watu watapaswa kushea interests kadhaa au kutunziana siri, kushauriana, kusoma, kufanya kazi pamoja nk.. wengine hata hufanyiana ukuwadi. Uhusiano wenyewe usipokuwa natural enough (ktk sensi ya upekee wake) hautakawia kuporomoka na hivyo kutofikia malengo.

Ukuwadi tena?!HAYA!!!
 
Sisemi ufanye maksudi! Ila nataka ujue kuwa inatokea tena sana tu. Rafiki yangu m1 ana ndoa ya takribani miaka 6 sasa. Mkewe ndiye alikuwa msuluhishi mkubwa sana walipokuwa wanagombana na mchumba wake wa awali. Vurugu zilipozidi wakaachana na urafiki wao ukaendelea. Dada akiwa na mambo yake ambayo kwa maelezo yao hayakuwa wazi sana lakini ya mkaka (huyo rafiki yangu) yalikuwa yanajulikana sana tu. Baadaye kutembeleana kukazidi mwisho without discussion wakajikuta ni wapenzi hatimaye ni wanandoa leo. Briefly they love each other. Maigizo kama yapo sina hakika.

Ukuwadi tena?!HAYA!!!
 
Siku za mwizi arobaini, atajikanyaga tu mahali utamgundua, kwa uzoefu wangu wengi siku hizi ni wasanii tu, mpaka upate wa kweli ni kazi haswa na ndio maana ndoa nyingi za hazidumu
 
Kwa maoni yangu kuna vitu vingi sana vya kuangalia..Ingekuwa wote tupo kwenye level moja kila kitu basi ingekuwa rahisi kutambua..

Mi ninavyoona, mambo yafuatayo yanawezeka kusababisha mtu akawa na upendo fake ili atimize azma yake..

1. umaskini
2. dini/imani
3. elimu
4. umri
5. maeneo tunayoishi (asili yetu)/kabila
6. Magonjwa

Hivi vitu visiposhughulikiwa mapema vinaweza kupelekea mapenzi ya uongo..Mtu anaweza 'kukupenda' kwa sababu ya kipato chako. au mwingine atadanganya kwamba anaishi 'Dar' ili muwe wapenzi..

Kwa hiyo kumjua mtu kama anaupendo wa kweli basi ni vyema
1.Uandae vigezo vyako ili kumpima mwenzio
2.Kujenga tabia ya kuwa wazi kusema umri, elimu, n,k kama nilivyoorodhesha hapo juu
3.Kuwa na uvumilivu/kusubiri ili kuujua undani wa mwenzio
4.kujiatahidi kupata ushauri kama kuna utata
5.Kumshirikisha Mungu sana.

Ni hayo
The Following User Says Thank You to Eiyer For This Useful Post: Safina.

Mi ninavyoona, mambo yafuatayo yanawezeka kusababisha mtu akawa na upendo fake ili atimize azma yake..

1. umaskini
2. dini/imani
3. elimu
4. umri
5. maeneo tunayoishi (asili yetu)/kabila
6. Magonjwa

Naomba kuongezea namba 7:
7. Kuolewa.
 
Watu wengi tunapenda kusema yule mtoto au jamaa ananipenda sana a.k.a kanizimia ile mbaya nk. Naomba wanajamvi tujadili jambo hili kwa kina. Maadam kuna wasanii wengi sana ktk maisha ya siku hizi unaweza vipi kumtofautisha mtu anayekupenda kwa dhati na anayekusudia hasa (kwa dhati) kuonekana anakupenda kwa dhati japo siyo kweli?

Hadi kufikia muda huu naamini kwamba kama mtu ana lake jambo na amekusudia kwa nia moja anaweza kuigiza vizuri kiasi cha kuaminika kama anayependa kwa dhati wakati kumbe ana nia yake tofauti, na kupenda ni njia tu kufikia malengo. Mfano mzuri ni kijana anayempenda binti na kufanya mengi tu kama kubadili dini nk akidai anapenda lakini akishafaidi anachotaka huyoooo! anatimua. Hamjawasikia watu kama hao? Baadhi yao wanasema waziwazi kwamba iliwalazimu kujifanya wamependa ile mbaya ili wapate. Madada pia wapo wanaodai walijifanya wamependa ili kupata utajiri nk.
Halafu wadada wengi huwa tunadondokea mikononi mwa wanaoigiza tunaacha wale halisia sijui huwa inatokana na nini
 
Nadhani hawa watu (Players) huwavutia zaidi kwa jinsi walivyo na wanavyokusudia kuonaekana. Mashuleni, vyuoni na maeneo kama hayo, kwa mfano, vijana wengi wanaopenda kwa dhati hata kujiexpress mbele ya wasichana huwa hawawezi au hawajui na hivyo wanabore. Wavulana wengi wenye uwezo wa kujipresent na kujielezea vizuri kwa madada kiasi cha kuwaridhisha huwa ni wale wenye uzoefu wa kushawishi na ambao kwa nguvu zao huweza kunasa wasichana wengi na hivyo kukosa utulivu maana hata kama atapenda pua yako tu atataka zaidi na kwa kuwa ana uwezo huo utamkubalia tu.
Wakati mwingine raha tunazohitaji (wake kwa waume) kwenye mahusiano haziwezi kutolewa na watu wanaotupenda sana kwa kuwa wao hudhania si ustaarabu kwa mtu wanayempenda na hivyo tunajikuta tunafuata raha badala ya mtazamo/hisia za wahusika juu yetu. Hali hii inapotokea mtu anashindwa kutofautisha kupendwa kwake halisi na tamaa/uchu wake na matumaini ya kupendwa ktk akili yake. Unampenda jamaa na unatamani akupende pia lakini unajidanganya katika nafsi anakupenda.

Halafu wadada wengi huwa tunadondokea mikononi mwa wanaoigiza tunaacha wale halisia sijui huwa inatokana na nini
 
Anayependa kweli anajitoa kwa moyo wake wote, ila yule anayeigiza utamjua tu, hata kwa kuwangalia, na hata siku moja hawezi kusucrifice kitu chochote juu yako, na wala hajali akikuumiza kwa lolote
 
Hii swali halina jibu, yote ni kumshirikisha Mungu ili ukutane na right candidate siyo MSANII. Ninachojua mimi wote tumekuwa wasanii, tunasema uongo ambao baadae ni ni mfarakano, bugudha na aibu. Kuwa mkweli toka mwanzo, kama una watoto wataje kwa majina, uliwahi kuolewa au kuoa ukaacha basi sema ukweli imi mtuachague bega mapema.

Uthubutu wa kusema uongo kabla hujaolewa, ujue wewe utakuwa muongo mpaka siku unaingia kaburini. Tuwe waaminifu na wawazi.
 
Imagine: Najitoa kila unapohitaji msaada wangu, sisiti kutumia chochote ili kukufurahisha, najitahidi kwa kila njia nisikuudhi, nakuletea zawadi kila mara, usipoonekana nalalamika kuona wivu, nakusifu kupendeza kila wakati, nakuomba mara kwa mara usiniache kwa kuwa nakupenda sana, nawajali wazazi wako na ndugu zako wote wananipenda na muda wote nawafaa ninapohitajika. Ninafanya yale unayosema wewe na si mwingine. Unaposema tusubiri nakubali na unaposema ok basi nahakikisha hujutii kuwa na mimi, bado unapougua nahangaika na kupozi kwa majonzi na unapopona nakufanyia pati na mazuri mengine yote yanayoweza kufanywa na mtu anayekupenda. Je hii inamaanisha ninakupenda kweli? Hakuna uwezekano wa mtu mwenye agenda yake kufanya vitu hivi tena kwa umakini mkubwa kiasi cha kuwaaminisha watu kuwa ni chaguo bora na la pekee?

[/QUOTE=Gaga;2080410]Anayependa kweli anajitoa kwa moyo wake wote, ila yule anayeigiza utamjua tu, hata kwa kuwangalia, na hata siku moja hawezi kusucrifice kitu chochote juu yako, na wala hajali akikuumiza kwa lolote[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom