Anayepaswa kupigwa mawe siyo Freeman Mbowe Bali ni CCM

Elice Elly

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
1,268
1,593
Nchi hii tangu tupate Uhuru IPO chini ya CCM na siyo Mbowe.

Umaskini wa nchi hii umeletwa na CCM siyo Mbowe.

Ufisadi Mkubwa tangu tupate Uhuru umefanywa na CCM.

Ukosefu wa elimu bora katika Taifa tangu tupate Uhuru umefanywa na CCM.

Uvunjwaji Mkubwa wa Sheria za nchi tangu tupate Uhuru unaongozwa na CCM.

Wizi wa rasilimali za Taifa hili tangu Uhuru unafanywa na CCM.

Mikataba mibovu ya kuliibia Taifa hili inafanywa na CCM.

Hao mnaowaita Leo mabeberu ni CCM inafanya nao mikataba mbali mbali huku wakileta hela ikiwaita wadau wa maendeleo, wakikemea mabaya ya CCM wanaitwa mabeberu.

Ni CCM inayo ligawa Taifa kwa hitikadi mbali mbali zinazo bomoa umoja wa kitaifa.

Ni CCM ndiyo walioua viwanda mbali mbali katika Taifa letu.

Mambo mengi mabaya yamefanywa na CCM ikiwa ni pamoja na kuliingizia taifa hasara nyingi.

Sasa huyo Mbowe mnaye msurubu kwa mabaya mliyofanya nyinyi mnataka kumfanya kuwa kafara kwa maovu yenu?
Acheni kufanya mambo yatakayo mchukiza Mungu.Kwa mabaya mliyolitendea Taifa hili mlipaswa kukaa kimya,msidhani kwamba watanzania ni wajinga kiasi hicho.IPO Siku Mungu Atawaumbua.
 
Mbowe asipoomba radhi kwa Watanzania kuna hati hati ya kuozea jela
Mbowe ndiye alichota pesa za EPA...

Mbowe ndiye alibaba hela za ESCROW...

Mbowe ndiyo aliuza nyumba za serikali kwa hawala zake kwa bei ya kutupwa....

Mbowe ndiye aliingia mkataba na ACASIA hotelini.....

Mbowe ndiye aliye iba Meremeta.....

Mbowe ndiye alikuwa akitorosha TANZANITE na Dhahabu bandarini.....

Mbowe ndiye aliyefisadi mashirika ya umma.......

Mbowe ndiye alisababisha kutoonekana matumizi ya 1.5T zilizooneshwa na CAG...

Mbowe ndiye aliua viwanda, kilimo, elimu, na sekta ya afya.....

Mbowe ni mfanyakazi hewa, mikopo hewa, mwanafunzi hewa.....

Mbowe ndiyo kaleta Corona, HIV na maralia.......




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ohh tumeibiwa sana,Mara nchi hii ilikuwa inaliwa sana,Mara gas imepigwa na wajanja.Tulipata Uhuru Mwaka 1961 ambapo TANU&ASP=CCM wamekuwa madarakani na hiyo wao ndiyo waliotufikisha hapa,wanayosema Mbowe na wapinzani wameyafanya kumbe tatizo ni wao.

Propaganda za kutugawa kwa vihoja vya uchwara wakidhani Watanzania ni wajinga.Eti wanataka kushinda kwa kishindo,huku wanaandaa refa,uwanja wao na washabiki wote wanaoruhusiwa kushangilia pia wawe wao Sisi wengine tunyamaze.Unyonge basi,nami sitaki kujumuishwa kwa wanyonge kwa Sababu Mimi siyo mnyonge ndani ya nchi yangu.Ni Marufuku.
 
ccm wamemshindwa mwamba mbowe, wanaongea na lusifa awape mbinu za giza
 
Back
Top Bottom