Anayemlipa Mpiga Zumari Ndiye Huchagua Wimbo-Sikia Hii

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,136
2,000
MWENYEKITI wa Friends Of Simba (F.O.S.), Zacharia Hans Poppe amewaambia wanachama wa Simba SC wahakikishe wanachagua viongozi wazuri katika uchaguzi wa klabu hiyo Juni 29, mwaka huu, vinginevyo hatakuwa tayari kushirikia na viongozi wasiofaa.
“Na siyo mimi tu, kuna wafadhili wengine sita nimewapata ambao wamekubali kuisaidia Simba SC, iwapo tu uchaguzi wa mwezi ujao utazalisha viongozi bora wenye kuaminika,” amesema Hans Poppe akizungumza na BIN ZUBEIRY leo.
Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) amesema kwamba baada ya miaka minne ya kuvumilia kufanya chini ya uongozi wa Alhaj Ismail Aden Rage, hatakuwa tayari kupoteza muda na fedha zake kwa mara nyingine kwa kuwasaidia viongozi wengine bomu iwapo watachaguliwa.
 
muhomakilo jr

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
11,185
2,000
Viongozi watakaochaguliwa ndiyo ambao wanachama wamewaona wanafaa,na siyo ambao Hans Poppe anawaona wanafaa,yeye anataka viongozi anawataka yeye ambao pengine si chaguo la wanachama,hapa ndiyo umuhimu wa virabu vyetu kujitegemea yaani kuwa na vyanzo vyao vya fedha/mapato....
 
MKALIKENYA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,196
1,170
Hivi kama katiba inasema mtu aliyewahi kufungwa haruhusiwi kugombea na kuwa kiongozi wa kuchaguliwa na wanachama inakuaje wale wanaochaguliwa wamchague mtu huyo kuwa kiongozi wa kamati fulani, uharari uko wapi hapo? na moral authority je? au katiba ni viini macho?

My take

Hakuna haja ya kumzuia mtu kugombea eti sababu alishawahi kutumikia kifungo hili suala nalipinga kabisa na kama katiba inazuia kuchaguliwa basi hata sifa za kuteuliwa hana.
 
anapigia upatu Friends
 
Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,136
2,000
inabidi tuichungulie Kat8ba ya JMT
Hivi kama katiba inasema mtu aliyewahi kufungwa haruhusiwi kugombea na kuwa kiongozi wa kuchaguliwa na wanachama inakuaje wale wanaochaguliwa wamchague mtu huyo kuwa kiongozi wa kamati fulani, uharari uko wapi hapo? na moral authority je? au katiba ni viini macho?

My take

Hakuna haja ya kumzuia mtu kugombea eti sababu alishawahi kutumikia kifungo hili suala nalipinga kabisa na kama katiba inazuia kuchaguliwa basi hata sifa za kuteuliwa hana.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom