Anayekwamisha katiba ni nani? na ni kwa maslahi ya nani?

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Zilitumia billion 200 kukusanya maoni ya wananchi na Jaji Warioba.

Maoni yakawekwa kapuni

Kuna watu wanasema katiba sio kipaumbele yaani Leo ndio mnaona katiba sio kipaumbele wapuzii nyie

Billion 200 zilitengwa kwenda kuosha mataili ya gari au? Zilitengwa kutwanga maji kwenye kinu?

Wanaosema katiba sio kipaumbele ni watu wapumbavu Mimi nawaita maana hawaoni kwamba katiba ya sasa ni kiasi gani imeleta madhara katika taifa letu.

Mimi nitasimama kuhesabiwa kipindi hiki kabla ya 2025 tunataka katiba mpya kwa namna yeyote

Hatutishani Bali tuambiwe pesa zilizotumika mwaka 2013 na 2014 kukusanya maoni kama katiba hawaleti hizo pesa zinarudi vipi tujenge barabara.

Katiba ndio jambo la msingi kwa sasa kuliko mambo yote tunataka katiba mpya ya warioba yenye maoni ya Watanzania.
 
Ni CCM kwa maslahi yao, zile pesa zilizotumika haziwaumi roho coz hazikuwa za kwao, ni za walipa kodi masikini wa hii nchi.
 
Ni CCM kwa maslahi yao, zile pesa zilizotumika haziwaumi roho coz hazikuwa za kwao, ni za walipa kodi masikini wa hii nchi.
Mi nadhani kuna watu ndani ya CCM hawajiamini kutokana na udhaifu wao ndiyo wanatumia katiba iliyokuwepo kuharibu nchi.
Lakini kwa sasa naona kitu cha lazima tune huru ya uchaguzi ili wapatikane wawakilishi halali wa wananchi bungeni ili kama hiyo katiba mpya ikijadiliwa iwe ina watu sahihi na halali wa kuipitisha.
 
Ni vigumu kwani huko bungeni wamejazana wenyewe wanajadili mambo ya kitoto tu, hawana pressure wanajua next tym watarudi tena bungeni labda Samia asiwabebe wasiojiweza kama Magufuli alivyofanya, Katiba Mpya ndio mwisho wao hawawezi kuikubali.
 
Shida ilianza na maoni ya wananchi yana nafasi gani kwenye uandishi wa katiba mpya. UKAWA wakasema maoni yabebwe kama yalivyo, kama ni changes zilibadili muktadha.. CCM kwa umoja wao wakasema no, ya wananchi ni maoni tu, waandika katiba mpya tupo hapa kwenye Baraza.

Kilichofuatia ni kubadili maoni ya msingi kama muundo wa serikali tatu walioutaka wananchi etc. UKAWA wakatoka, CCM wakapata walichotaka i.e status quo. Pima mwenyewe ujue aliyevuruga ni nani
 
Back
Top Bottom