Anayejua Tiba Mbadala ya Amoeba Tafadhali Anijuze

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Wadau,

Nina mwezi wa nne mfululizo naumwa amoeba na nimetumia kila aina ya madawa lakini wapi haitoki. Mara kadhaa nikienda maabara naambiwa nina amoeba na minyoo ya ascaris. Nimetumia sana dawa za kisasa lakini natesekea tu bila kupata nafuu. Hivi jamani hakuna tiba mbadala ya amoeba na ascaris? Tafadhali naomba msaada.
 
Pole sana mkuu! Unapima wapi na unapewa dawa gani??? Tuanzie hapo

Kwa mara ya mwisho nilipima Mikocheni Hospital na nilipewa dawa nadhani inaitwa CONAZ pamoja na Albendazol. Nimemaliza dozi lakini bado najisikia hali ile ile.
 
Jaribu ku2mia flagile,trinidason ikishindikana waone wamasai wakupe za kienyeji!
 
Pole sana mkuu! Unapima wapi na unapewa dawa gani??? Tuanzie hapo

Good start mkuu, ...ni vizuri kujua alipataje hao minyoo na Amoeba..maana hata kama atapata dawa sahihi, katika dozi na muda sahihi kisha akarudi katika mazingira/hali ile ile iliyomsababisha kupata tatizo haitasaidia na kudhani kuwa dawa hazifanyi kazi.
 
Mimi nimewahi kusumbuliwa sana na amoeba mpaka kujisaidia damu nilikunywa dozi na dozi,kila nikipima hospitali zetu hizi za kata naambiwa ni minyoo napewa albendazol.nilipokwenda private hospital nikatibiwa vizuri sana mpaka sasa ni miaka mitatu sijaugua tena huo ugonjwa lakini dawa siikumbuki,halafu kingine nilijitahidi sana kurekebisha mazingira nyumbani kwangu,

cha kwanza nilihama nyumba niliyokuwa naishi kwa sababu mwenye nyumba na ndugu zake walikuwa ni wachafu sana.halafu epuka kupigia mswaki chombo cha kuogea kwa sababu kuna watu wakitoka haja kubwa wanajitawazia kwenye vyombo hivyo,hivyo ndivyo alivyokuwa mwenye nyumba wangu.
 
Wadau,

Nina mwezi wa nne mfululizo naumwa amoeba na nimetumia kila aina ya madawa lakini wapi haitoki. Mara kadhaa nikienda maabara naambiwa nina amoeba na minyoo ya ascaris. Nimetumia sana dawa za kisasa lakini natesekea tu bila kupata nafuu. Hivi jamani hakuna tiba mbadala ya amoeba na ascaris? Tafadhali naomba msaada.

Tafuta uzi, wa jamaa anaitwa BAOSITA,alipost kuhusiana na kitunguu swaumu,kinavyoweza kumaliza fungus,amoeba na hao minyoo.
 
Unachukua kitunguu swaumu kizima unakimenya,unakitwanga chote alafu unachanganya na Maji ya vugu vugu kama nusu lita unakunywa yote,lakini usitumie kama unapresha ya kupanda.

Nayakumbuka haya Maelezo
 
kutibu amoeba kunaendana pia na vitu kadhaa vya kufuata,epuka,maji yasiyochemshwa,juisi ambazo kwa hakika hufahamu zimetengenezwa na maji gani,kachumbali,wakati wa kuoga watu wengi wanajisahau maji yanaingia kwenye mdomo,wanameza, sahani ya chakula na glasi ya maji viwe vimekaushwa vizuri nakitambaa.matunda uoshe na maji salama ambayo hayatakuwa navimelea vya amoeba,dawa nzuri ukiizingatia vizuri kwa muda bila kuruka ni flagyl(metronidazole).
 
Msaada anaotaka mleta uzi ni tiba mbadala. Inawezekana hiyo dawa uliyomtajia ameshatumia tayari kama ilivyo kwangu. Nami nasumbuliwa sana na amoeba. Huwa napona baada ya muda naanza kujisikia vibaya yena nikipima naambiwa ni amoeba.
 
Mkuu, it is very unlikely kupata "Amoeba isiyopona" dawa hufanya kazi...naomba niseme tena hili, Dawa hufanya kazi , ila wengi hudhani ikishatumia dawa unapata na kinga(prophylaxis) na wakitoka hapo wanarudi kule kule!!

Mf. mzuri amesema mkuu Isaac Chikoma, tumia dawa lakini USIRUDIE mazingira ya zamani yaliyosababisha tatizo hilo...Only that.
 
Last edited by a moderator:
Msaada anaotaka mleta uzi ni tiba mbadala. Inawezekana hiyo dawa uliyomtajia ameshatumia tayari kama ilivyo kwangu. Nami nasumbuliwa sana na amoeba. Huwa napona baada ya muda naanza kujisikia vibaya yena nikipima naambiwa ni amoeba.

mkuu hata mimi nimekuwa nikisumbuliwa na amoeba,moja ya vitu ninavyofuata ili nilipate maambukizo mapya nimeandika hapo juu,kama,nimetumia dawa nyingi,za kihindi,tinidazole,conaz,metronidazole, nikawa narudi pale pale,the most effective drug kwa amoeba nimetaja hapo juu,nilichogundua ni kwamba sikuwa nafuata dose kama inavyotakiwa,kuruka ,kupitisha masaa.kwa sasa hainisumbui tena. Dawa ninayoyumia ni hiyo hiyo,ila nimebadili mwenendo wa vitu ninavyotumia kama nilivyoeleza hapo juu.
 
Isack nashukuru kwa ushauri wako. Masharti ya kimazingira unayoeleza ninayazingatia sana. Kwa ujumla, nimekuwa nikijitahidi kuepuka kadri ninavyoweza kupata contamination. Na nafanya hivyo kwa sababu madhara yake nimeya-experience sana. Pamoja na kufuata masharti hayo, naweza kupumzika wiki mbili then hali inarudia. Nimetumia dawa zote ulizoeleza hapo juu pamoja na dawa moja inaitwa furazol ambayo dozi yake kwa weight yangu ina vidonge 60. Niliambiwa dawa hiyo ni nzuri sana lakini wapi. Jambo la ajabu ni kwamba katika mazingira hayohayo ninayoishi wenzangu wawili sioni kama wanasumbuliwa na amoeba tena wapo loose zaidi katika kuzingatia kanuni za usafi.

Baada ya mateso ya muda mrefu ndiyo maana nimeamua kuuliza kama kuna tiba mbadala ili nijaribu.
 
Unachukua kitunguu swaumu kizima unakimenya,unakitwanga chote alafu unachanganya na Maji ya vugu vugu kama nusu lita unakunywa yote,lakini usitumie kama unapresha ya kupanda.

Nayakumbuka haya Maelezo
Fanya hii ni ukwi kabisa ! mdogo wangu tumesumbuka mpaka rufaa nikasoma ile uzi akafanya hivyo ss mzima kabisa like a miracle na alikunywa once!
 
cha kwanza nilihama nyumba niliyokuwa naishi kwa sababu mwenye nyumba na ndugu zake walikuwa ni wachafu sana.halafu epuka kupigia mswaki chombo cha kuogea kwa sababu kuna watu wakitoka haja kubwa wanajitawazia kwenye vyombo hivyo,hivyo ndivyo alivyokuwa mwenye nyumba wangu.

haahahaaaaaaaaaaaaaa! at your level unashare vyombo vya kuogea na mwenye nyumba? unagongea na sabuni? teeeeeeeeeeeeeeeeeeeeh! kweli uswahilini kuna mambo..!
 
Pole sana ndugu yangu. Mimi najua dawa mbadala ya AMOEBA ni mbegu za papai lililoiva. Unachukua mbegu za papai unaweka maji safi na salama kidogo kiasi cha nusu kikombe cha chai halafu unablend kwenye blender. Unatumia kijiko kikubwa cha chakula kikubwa viwili kutwa mara tatu kwamuda wa siku saba. Kama huna blender basi unaweza kutafuna mbegu zenyewe kiasi cha kijiko kimoja kikubwa cha chakula kutwa mara tatu. Utapona kabisa mpendwa. Kuna ndugu yangu alisumbuliwa sana na tatizo hilo akashauriwa kutumia dawa hiyo na sista mmoja wa kanisa katoliki parokia ya Kristo Mfalme Moshi. Alipona kabisa mpaka leo hajawahi kuumwa Amoeba. Pia zingatia ushauri wa wadau wengine, mfano usinywe maji yasiyochemshwa, usile kachumbari ambazo huna hakika na utayarishwaji wake mfano kula kabichi mbichi n.k. Tumia then utoe feedback!! GET WELL SOON!!
 
Mungu akubariki mpendwa. Nitajaribu na kukupatia feedback.
 
Mimi nimewahi kusumbuliwa sana na amoeba mpaka kujisaidia damu nilikunywa dozi na dozi,kila nikipima hospitali zetu hizi za kata naambiwa ni minyoo napewa albendazol.nilipokwenda private hospital nikatibiwa vizuri sana mpaka sasa ni miaka mitatu sijaugua tena huo ugonjwa lakini dawa siikumbuki,halafu kingine nilijitahidi sana kurekebisha mazingira nyumbani kwangu,

cha kwanza nilihama nyumba niliyokuwa naishi kwa sababu mwenye nyumba na ndugu zake walikuwa ni wachafu sana.halafu epuka kupigia mswaki chombo cha kuogea kwa sababu kuna watu wakitoka haja kubwa wanajitawazia kwenye vyombo hivyo,hivyo ndivyo alivyokuwa mwenye nyumba wangu.

mkuu ulienda hospitali gani????? ni vyema ukatusaidia na sisi japo hospitali uloenda kama dawa huikumbuki.
 
Back
Top Bottom