Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
✓Hakupandisha Mishahara wala madaraja kwa wafanyakazi _lakini kuna wafanyakazi watampa kura

✓Hakusaidia Wakulima pembejeo wala soko la mazao, kibaya akawadhulumu pesa zao za korosho na pamba_lakini kuna wakulima watampa kura

✓Ameongeza kodi pammoja na kufanya assessment mpya ya back taxes na hivyo kuwapa mzigo mzito wafanyabiashara uliopelekea biashara nyingi kufungwa_ lakini kuna wafabiashara watampa kura

✓Hakuhangaika na ajira ya vijana, vijana wengi waliomaliza vyuo toka 2015-2020 hawajapata ajira_lakini kuna baadhi ya vijana hawa watampa kura

✓Alipandisha riba ya mikopo ya elimu ya juu kutoka 9% hadi 15%, pia hakuongeza idadi ya wanafunzi vyuo vikuu kupata mikopo_kuna wanafunzi wapo vyuo na hawana mikopo watampa kura

✓Ameweka katazo mafao ya kujitoa, Leo hii ukiacha au fukuzwa kazi na una umri wa miaka 20 utasubiri hadi ufikishe miaka 60 kupata mafao_hapa napo kuna watakaompa kura

JE TATIZO NI UJINGA? JE TATIZO USHABIKI WA KIVYAMA? JE TATIZO NI ELIMU? JE NI MASILAHI BINAFSI ?
 
Kwa miaka 60 ccm wametengeneza ujinga nchini. Wamezalisha wajinga wengi sana kiasi kwamba hata elimu wanatoa ili watu wawe wajinga zaidi kuliko wasingeenda shule. Matokeo yake wanatanzia hawafikirii kabla ya kutenda na ndiyo maana wengi bado wanapigia kura ccm wala hawajihangaishi kuwaza yote hayo uliyoandika.
 
Ni ujinga tu ndio unatusumbua kila kukicha...watu wanafungiwa biashara zao mfano maduka ya kubadilisha fedha za kigeni+kauli za kibabe kwa watumishi wa serikali na wananchi na bado masikio hayasikii,ilitakiwa kuonesha kwamba wananchi hawataki viongozi wasio na nidhamu kwa wananchi,ilikuwa kuangusha meza tu 28/oktoba.
 
Ni kweli uliyosema. Ila Magufuli anaweza haya:-
1. Ni mropokaji kwa kuwa anapoongea hajali kadamnasi imayomsikia. Matusi ya nguoni ndiyo lugha yake ya kawaida.

2. Hapendi upinzani kwa kuwa akiruhusu atashindwa asubuhi. Ndiyo maana katumia hela ya Serikali kuwanunua wabunge wa Kinondoni, Siha na Bahati.

3. Anapenda rushwa na ufisadi ndiyo maana hataki kufanya kazi na CAG aliye nyooka.

4. Ni mwizi wa mali ya umma ndiyo maana kamuweka Katibu Mkuu Hazina ambaye ni mpwa wake. Kwa miaka 4 tayari Tsh 2.4 Trillion hazijulikani zilipo

5. Ni mpenda ukabila kwa kuwa sehemu nyeti zote amejaza ndugu na watu wa Kanda ya ziwa Angalia IGP, DPP, AG, KM-KM-Hazina, RC DSM, Waziri Nishati, CAG mpya, Waziri Viwanda, Jaji Mkuu nk

6. Ni mtu wa kufuja mali ya umma. Angalia ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato na uanzishaji wa mbuga ya Burigi -Chato

7. Amezuia shughuli za vyama vya siasa wakati CCM inafanya mkutano kila mahali. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2000 na Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 zinatambua shughuli za vyama vingi.

8. Hataki watu wajieleze kwa uhuru kadri ya katiba, na amevibana vyombo vya habari. Kwa mfano Eric Kabendera ameanzishiwa shitaka la kutakatisha fedha wakati kiukweli ni maoni yake kwenye gazeti la The Economist

9. Anachukia wenye vyeti feki lakini kamuacha Bashite aendelee kuwa RC DSM wakati naye ana cheti feki. Hata PhD yake yasadikiwa amekopi kwa supervisor wake ambaye kamteua kuwa Katibu Mkuu wa Wizara mojawapo.

10. Ameruhusu kikundi cha wasiojulikana kiteke watu, kuwatesa na wengine kuwaua kama Ben Saanane, Azory Gwanda. Na majeruhi kwa Tundu Lissu

11. Analitawala Bunge kwa remote control. Bunge haiwezi kuhoji chochote kilichofanywa na Serikali.

12. Mahakama nayo iko mfukoni mwake
 
Miaka 5 Iliyopita CCM ilitukosea sana watanzania Kumsukumizia jiwe kwenye Urais.

Hakika tumeteseka sana
 
Tumeipenda wenyewe na mvimbe mpasuke🤣🤣🤣🤣🤣 Aliyetunga huu wimbo nikimuona mbinguni mi nageuza.
 
Jibu Ni elimu kaka ukitaka kumtawala bina adamu maisha mnyime elimu,na sababu atakuwa hajielewi na hajitambui sasa ndio watanzania waoivyofanywa
 
Ni ujinga tu ndio unatusumbua kila kukicha...watu wanafungiwa biashara zao mfano maduka ya kubadilisha fedha za kigeni+kauli za kibabe kwa watumishi wa serikali na wananchi na bado masikio hayasikii,ilitakiwa kuonesha kwamba wananchi hawataki viongozi wasio na nidhamu kwa wananchi,ilikuwa kuangusha meza tu 28/oktoba.
Kweli kabisa ujinga tu
 
Umesahau....amejenga barabara ..ameleta elimu bure....ameleta nidhamu serikalin...ameleta ndege....amekuza uchumi.kumbuk tupo uchum wa kat


Miaka mitano mingine kwa magufuliiii
 
Umesahau....amejenga barabara ..ameleta elimu bure....ameleta nidhamu serikalin...ameleta ndege....amekuza uchumi.kumbuk tupo uchum wa kat


Miaka mitano mingine kwa magufuliiii
Type ufanunuzi wa uchumi wa Kati huku biashara nyingi zikifugwa,masoko magumu ya mazao embu teeleweshe
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom