Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
I agree. If it looks like a duck and walks like a duck, even if it talks like chicken, it is a duck either way. Many have objected to the notion that he will want to vie for presidency again and again. It is just mere chicken talk, but we know a duck is a duck.

Thank God for TL, at least now CCM is facing stiff competition. Let us hope this interferes with any secretive plans they have been plotting. God bless Tz, but politics in this country stinks indeed. Thanks for a great post.

Kutokana na muonekano wa mienendo ya raisi Magufuli toka aingie madarakani , mioyo ya baadhi yetu inasita kukubali kwamba hili haliwezi kutokea Tanzania.

Lakini leo nilivyoona wanajeshi wanapiga saluti chato huko kijijini kwake,tena airport aliyoijenga yeye kitu kama kimeclick.
Tujitayarishe kuingia kwenye wakati mgumu sana tangia Tanzania ipate uhuru.

Tunaingia kwenye uraisi wa maisha.



Sent from my SM-A505FN using JamiiForums mobile app
 
Watetezi wake mlivyowajinga mtatetea uhuni wake wa kubadili katiba.
CCM hamjawahi kuwa na uchungu na nchi zaidi ya majimbo yenu tu.
Nadhani umekosea kuniqoute mkuu. Comment nimeandika mimi mwenyewe.

Kwa lugha rahisi nipo mwenyewe hapa kwa keyboard.
 
Nadhani umekosea kuniqoute mkuu. Comment nimeandika mimi mwenyewe.

Kwa lugha rahisi nipo mwenyewe hapa kwa keyboard.
Nimemaanisha nilichokiandika.

Ili kuzuia hilo hakikisheni mnapigia kura wabunge wengi wa upinzani nje na hapo wale ccm wakienda bungeni kazi yao kubwa ni kupigia makofi serikali hata kwenye mambo yenye madhara kwa wananchi.

Hatuna namna nyingine ya kuzuia Magufuli asiongeze muda madarakani zaidi ya kumuondoa nafasi hiyo kupitia bunge.


Kule Zanzibar wanafanya kila linalowezekana ili apate 2/3 majority kwa upande wa Zanzibar ajipe urais wa maisha.
 
Atamaliza miaka yake mitano aondoke aje mwingine. Hatuhitaji nchi kufanywa ya familia kama baadhi ya nchi zilizotuzunguka.

Anafanya kazi nzuri saana ila hilo la kubaki milele asahau.
Wewe hujui unachokiongea. Na hata auhitaji kueleweshwa, kwa sababu una u much know mwingi
 
Nimemaanisha nilichokiandika.

Ili kuzuia hilo hakikisheni mnapigia kura wabunge wengi wa upinzani nje na hapo wale ccm wakienda bungeni kazi yao kubwa ni kupigia makofi serikali hata kwenye mambo yenye madhara kwa wananchi.

Hatuna namna nyingine ya kuzuia Magufuli asiongeze muda madarakani zaidi ya kumuondoa nafasi hiyo kupitia bunge.


Kule Zanzibar wanafanya kila linalowezekana ili apate 2/3 majority kwa upande wa Zanzibar ajipe urais wa maisha.

Ukiamua kuniqoute tumia umoja maana sisaidiani na mtu kuandika unachokisoma.

Hapa hakuna fact iliyomezani zaidi ya hisi tu. Na nimeshamsikia akijibu tuhuma za kujiongezea muda.

Sasa kama hadi kufikieni sasa Magufuli hajasema wala kuonyesha kwa vitendo kuwa atajiongezea muda, suala la kutokuwachagua au kuwachagua wabunge wa upinzani linabaki mikononi mwa mpiga kura mwenyewe.
 
Wasalaam,

Kwa nini tuifute CCM Oktoba 28?

1. Usiri katika mikataba ya madini na gesi.
2. Kunajisi katiba ya JMT
3. Kufuta bunge live
4. Kudharau na kuwadhulumu wafanyakazi wa umma na wakulima.
5. Ufisadi umetamalaki
6. Utekaji na mauaji ya wapinzani/ kubambikiwa kesi
7. Maisha magumu kwa kila Mtanzania.
8. Kutoweka uhuru wa kujieleza na Uhuru vya vyombo vya habari
9. Ubaguzi katika mikopo elimu ya juu

Miaka mitano ya magufuli imetosha na miaka 60 ya utawala wa CCM imetosha pia tunahitaji fikra mpya kuchagua CCM ni sawa kuchagua miaka mingine 5 ya mateso maana kupanga ni kuchagua.

Maendeleo yana vyama.
 
CCM ni ileile wakipewa mitano mingine watazuia mpaka mitandao ya jamii tukose madini ya Lissu.
 
Huu ni uongo mkubwa . Sisi wakazi wenyewe wa Morogoro hatuoni hilo. Barabara zinatengenezwa kwa usawa.
Zimechongwa Mji mzima bila kujali Diwani ni Chama gani.
Hata hivyo barabara hazitengenezwi na Halmashauri ambayo inaundwa na Madiwani Bali zinasimamiwa na TARURA , Chombo huru cha Serikali.
Kama ni uongo waulize wakazi wa Nangurukuru-Kilwa, walijibiwa hadharani kuwa hawapati standi kwa kumchagua mbunge toka upinzani.
 
Ndugu yangu huna haja ya kusumbua kichwa kujua tunaelekea wapi, wewe fanyakazi kwa bidii ulipe kodi kwa uaminifu na ustawishe familia yako. Hiyo kodi Magufuli tunaona anaitumia vizuri kujenga nchi. Kodi yako hailiwi na "Mchwa" kama ilivyokuwa inatafunwa hadharani hapo zamani.

Mheshimiwa Rais Magufuli anajua kuendesha nchi na kuiletea maendeleo, pia anajaua kuwafanya watu wajue kutafuta na kutumia fedha halali kujiletea maendeleo. Kwa kifupi MAGUFULI ANATUPELEKA KWENYE NCHI YENYE NIDHAMU! Huko nyuma tulikuwa hatuna discipline, tuliona kwenye mgao wa escrow, walipata mgao na wakazipokea ni kada zote, sheria, imani (dini), bunge nk! Leo hata ndoto ya kutokea harufu tu kama ile - HAKUNA! MAGIFULI HOYEE! Ila Sisiemu wanatabia za Wajumbe!
 
Kusema kweli Rais Magufuli akiingia jamii forum kusikiliza shida zetu itapendeza sana,maana kipengele cha maoni kina jumbe nyingi sana na sina hakika kama zinashughulikiwa,ni vyema angetangaza siku akatoa na mda ili tutoe shida zetu,
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom