Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Magufuli kauliza katenda dhambi gani asipewe tena miaka 5, sasa majibu yake haya hapa:

1. Hajatoa ajira miaka 5
2. Hajaongeza mishahara kwa miaka 5
3. Ameongeza makato HESLB toka 8% to 15%
4. Amefukuza wafanyakazi na hajawapa hata senti tano kisa vyeti feki
5. Kaondoa fao la kujitoa NSSF
6. Kaondoa wanunuzi binafsi wa kahawa waliokuwa wanatoa bei nzuri
7. Karudisha gharama za matibabu kwa watoto na wajawazito
8. Anatoza maiti kodi kuzitoa mochwari
9. Kavunja katiba ya nchi kuzuia wapinzani kufanya mikutano halali ya siasa
10. Katunga sheria kandamizi kukomoa watu
11. Kabambikia kesi watu kwa visasi na chuki
12. Kafilisi wafanyabiashara kwa chuki binafsi
13. Kathibiti mashirika ya kutetea haki za binadamu
14. Kadhibiti na kutisha vyombo vya habari na kuviamrisha vimtangaze yeye tu na chama chake
15. Kavuruga sana mahusiano ya kimataifa
16. Kavuruga demokrasia na anataka wananchi waishi kama mifugo yake kufuata analotaka
17. Kazima bunge live na kulitumia bunge kama muhuri kufanya mambo yake
18. Mahakama imebinywa na imekuwa siyo huru tena
19. Kawadhibiti viongozi wa dini wanaomkosoa na kumwambia ukweli
20. Kanunua ndege bila kufuata sheria ya PPRA
21. Watu wengi wameuwawa na kupotea na kutekwa
22. Amelea na kulinda kikosi kazi cha "watu wasiojulikana"
23. Amepandikiza hofu, ukatili na dhuluma kama nyenzoza siasa mpya za Tanzania na utu umetoweka
24. Ameasisi ufisadi mkubwa sana Yeye na ndugu zake aliowachomeka serikalini na kuiba fedha kwenye miradi ya serikali kama Mayanga Contractors na Mbutu Contractors
25. Kakivuruga chama chake na kukimega vipande vipande
26. Kajenga uwanja wa ndege kwao bila ya ruhusa ya bunge wala Baraza la mawaziri.
27. Amebomoa nyumba za maelfu ya watu kwa kisingizio cha sheria ya barabara na hajalopa fidia hata mia
28. Ameikataa katiba mpya kupitishwa kwa hila tu
Ongeza Sababu zako kwanini Magufuli Hastaili Kuwa Raisi wa TANZANIA..

Nimeikuta mahali nikaona kama ina ukweli kwa asilimia 80.
 
Watanzania wengi tutamchagua Rais Magufuli Mafisadi na wauza madawa ya kulevya na wanaoutumika na Mabeberu ndio hawatamchagua.

Kwa kuwa Watanzania 98% wanampenda Rais Magufuli hata asipopiga kampeni ushindi ni uhakika.
 
Kwa kuongezea hapo kapora rambirambi za wahanga wa tetemeko la Kagera .
IMG_20200911_013530.jpg
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom