Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Mbona kawaida sana na ndio utamaduni wetu sisi waafrika baada ya Mungu salam za shukrani zinaenda kwa mkuu nchi kisha ruksa kuzungumza unachotaka kusema.
 
Sumve 2015,

Kwahiyo yale maombi ya siku tatu kushukuu kuisha kwa Corona yalikuwa kwa Shetani?

Kele KKKT alikwenda kuhutubia Mkuu wa nchi kulikuwa binafsi, kama ndiyo kwanini zile kauli zimefanyiwa kazi, mfano kufungua vyuo, kutovaa barakoa maana aliziita "matambara" etc?
 
Kuna Uzi humu unauliza "Nani amemuumba Mungu?" Nenda kausome. Mungu wa mtu anatengenezwa na mtu. Wacha watu waendelee kusifu na kuabudu.
 
Sumve 2015,

Kwahiyo yale maombi ya siku tatu kushukuu kuisha kwa Corona yalikuwa kwa Shetani?

Kele KKKT alikwenda kuhutubia Mkuu wa nchi kulikuwa binafsi, kama ndiyo kwanini zile kauli zimefanyiwa kazi, mfano kufungua vyuo, kutovaa barakoa maana aliziita "matambara" etc?
Maombi yalifanyikia wapi? kama ni kanisani, makanisa hayo yanaabudu shetani? au unataka kutuambia kwamba maombi yalifanyikia Ikulu?
 
Wewe unajua kesho utaenda wapi?
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?

Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
 
Huu uzi utolewe! Umeisha mda wake! anatupereka wapi hajui tulipo saivi?
1. Standard guage
2. Bwawa la nyerere
3.fly overs
4.Bandari
5. Mafisadi/ majambazi/vibaka ( hawa wte kipindi cha jk walitisha. Saivi hawapo
6.mashamba ya bangi hayapo tena
7.ajari kupungua
8.umeme kila kijiji
9. Barick kakuukubari mziki
10.Tundu lisu msaliti kakimbia
11.corona imesalim Amri
12. Serikari iko dodoma
13. Tausi wameongezeka
14.ndege zimenunuliea
15.meli zimerudi
16. Wapinzani wameunga hoja

Kiujumla cwezi kumaliza hivyo magufuri anatupereka KAANANI.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom