Emmanuel Tengulaga
Member
- May 17, 2020
- 17
- 4
Ni kweliNimekuwa nikifuatilia mambo kadha wa kadha ambayo yanajitokeza katika taifa, nimeona tuna Rais anayetumia muda mrefu sana kufanya maamuzi makubwa na ya maana.
Kwa mfano hili janga la Covid-19 tangu limeanza hadi sasa hakuna hatua za msingi zilizochukuliwa kudhibiti maambukizi ya kuenea kwake.
Watu mbalimbali wamekuwa wakitoa mapendekezo mbalimbali kuhusu kulikabili jambo hili kama vile kufunga mipaka, kuifunga (lock down) Dar es salaam kwa muda, Benki kuu kuuhami uchumi, kusambaza vifaa vya kupima ugonjwa nchi nzima, n.k.
Yeye anawaza kukusanya kodi tu ndio maana hata tamko la mkuu wa mkoa wa Mbeya la kufunga baa mapema amelifutilia mbali. Hadi sasa amepumzika tu anasubiri hadi mambo yaharibike ndio achukue hatua.
Jambo pekee analoweza kulifanya kwa haraka ni KUFUKUZA WATU KAZI isipokuwa Makonda pekee.
Mlio karibu naye hata kama mnamwogopa kwenye hili pigeni moyo konde mumwambie.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app