Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Nimekuwa nikifuatilia mambo kadha wa kadha ambayo yanajitokeza katika taifa, nimeona tuna Rais anayetumia muda mrefu sana kufanya maamuzi makubwa na ya maana.
Kwa mfano hili janga la Covid-19 tangu limeanza hadi sasa hakuna hatua za msingi zilizochukuliwa kudhibiti maambukizi ya kuenea kwake.
Watu mbalimbali wamekuwa wakitoa mapendekezo mbalimbali kuhusu kulikabili jambo hili kama vile kufunga mipaka, kuifunga (lock down) Dar es salaam kwa muda, Benki kuu kuuhami uchumi, kusambaza vifaa vya kupima ugonjwa nchi nzima, n.k.
Yeye anawaza kukusanya kodi tu ndio maana hata tamko la mkuu wa mkoa wa Mbeya la kufunga baa mapema amelifutilia mbali. Hadi sasa amepumzika tu anasubiri hadi mambo yaharibike ndio achukue hatua.
Jambo pekee analoweza kulifanya kwa haraka ni KUFUKUZA WATU KAZI isipokuwa Makonda pekee.
Mlio karibu naye hata kama mnamwogopa kwenye hili pigeni moyo konde mumwambie.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wastaafu nao kimya!!

Mitandao tu ndio kwa sasa inasaidia kukosoa na kushauri vinginevyo hata baadhi ya hatua zinazochukuliwa huenda zisingekuwepo pasipo kelele za watu mitandaoni.

Bunge kwa sasa nalo msaada wake ni mdogo sana katika kuishauri na kuisimamia serikali.
BUNGE LIMEKUWA NA KAZI YA KUSIFU TU, WAKOSOAJI NA WASHAURI WANAFANYIWA VISA VINGI, KIONGOZI WAO NI WAHOVYO KABISA HUYO SPIKA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?

Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
[/QUO
Anatupeleka kwenye nchi ya viwanda
 
Yeyote anayesimama kwenye podium siku hizi anamsifia Magufuli kwa sifa zisizo za kweli bali propaganda za kijinga. Hiyo ni dalili mbovu kuwa nchi yetu tayari imeshakuwa chini ya Authoritarian rule.

Nimesikiliza hotuba ya kiongozi wa madaktari Tanzania, anachoongea ni upuuzi mtupu kiasi kwamba amesahau taaluma yake badala yake anajipendekeza kwa Magufuli na mafedhuli wengine.

Hivi kiongozi wa madaktari anavyotoa maneno ya jumla jumla bila kutoa ufafanuzi kuwa kulikuwa na wagonjwa 509 kabla halafu sasa wamepungua bila kueleza wamepunguaje. Hayo ni mapungufu makubwa ya Professionalism.

Rais wa chama anaongea amejaa uoga, anaongea bila kujiamini na kutoa maneno ambayo hata yeye mwenyewe hayaamini. Kwenye maneno yake anaonekana akimshukuru Magufuli kila wakati kwa kuwapa confidence? Hivi huyo Magufuli amempa confidence gani?

Ameulizwa kuhusu namba ya wagonjwa waliougua, mwenzake anajibu kuwa namba wanazo lakini si lazima watoe kwa public. KWANI KUNA SIRI GANI WAKIISEMA TUNA WAGONJWA WANGAPI?

Nimemsikia msemaji wa serikali akiisifu Chemistry ya Magufuli kuwa yeye ni namba tatu baada ya Pope na Angel Merkel. Jamani hizi kufuru zitakwisha lini? Hivi kweli Magufuli amefanya nini kwenye Chemistry kiasi cha kuongelewa kuwa ni mtu wa tatu duniani baada ya hao wawili? Hivi ni wapi wanawa-rank waliosoma hiyo mi-Chemistry?

Nimemsikia leo mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam akiitaja serikali hii ya Magufuli kuwa "SERIKALI TUKUFU" Jamani mnamwabudu huyo Magufuli kama vile ndiyo Mungu wakati ni binadamu wa kawaida. Nchi hii inapelekwa kwenye misingi ya Kisukuma sasa, HIYO SIYO UTAMADUNI WETU!

Siku hizi watu wameanza kumwabudu huyo Magufuli, mara serikali tukufu, mara mtukufu rais huku mtu mzima anataja majina yote na kwa mkazo ya huyo rais ili kujipendekeza. Ni kama yale mambo ya mkuu wa mkoa wa Tabora akisema Mungu amshukuru Magufuli? Nchi hii imeshakuwa laughing stock.

ACHENI KUSIFIA UJINGA NINYI WATU NA HAYO MA-TV YENU YA PROPAGANDA. HAKUNA MAZURI ALIYOYANYA MAGUFULI PEKEE YAKE ZAIDI YA KUHAMISHIA MJI MKUU KULE JANGWANI DODOMA ndiyo maana tunaishi kimaskini. Hakuna pesa na huyo Magu anajua lakini kwa sababu anapenda sifa anahamisha mji mkuu huku akijua hakuna pesa.

Barabara zote mnazomsifia zilibuniwa enzi za Benjamin Mkapa na baadaye Kikwete, Fly-overs ni projects za Kikwete, SGR ni plan ya Kikwete, yeye Magufuli alikuwa mtekelezaji na akarithi tu hiyo miradi ila kwa sababu anapenda kujisifu kama kawaida ya Wasukuma wote akiwepo Paskali, Ndiyo maana utasikia hizo sifa zisizo za kweli.
 
Ukiwa mwanaccm hovyo kabisa,ndo maana mimi kila ikikaribia mwisho wa mwezi nawahi kununua kifurushi ili nisiangalie TBCCM ya bure sitaki mastress.
 
Sisi walutheri tunasema utukufu ni wa Mungu, ila sasa hawa wenzetu wameushusha utukufu mpaka kwenye jiwe!
 
Status
Not open for further replies.
185 Reactions
Reply
Back
Top Bottom