Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Sijui kama niko sahihi kuiweka na CCM au abaki mwenyekiti peke yake mtasahihisha wenyewe

Japo wengi hatuzijui sheria ila hatukuzoea kuona waziri anaapishwa kwenye makazi binafsi ya mtu

Japo mambo hubadilika hatukuzoea kuona Spika anapewa kiburi na Rais

Japo dunia inaenda kasi hatukuzoea kuona Rais anatoa kauli za kuchanganya wakati wa majanga

Japo kila mtu na tabia zake ila hatukuzoea kuona mtu akihamia CCM au akiwa mwana ccm anakuwa huru kufanya analolitaka

Bungeni sheria hazifuatwi,

Mahakamani mashauri ili kuamliwa yanasikiliziwa kwanza,

Watumishi wa umma hawana tena uwezo wa kunyanyua mdomo kudai haki zao

Mapolisi wanaamrishwa kufanya chochote na wakubwa zao,

Wapinzani wanajiongelesha ongelesha tu ila hawana wanachoweza kufanya,

Vyama vya wafanyakazi vinajiongelesha tu havina la kufanya,

Mawaziri wanajiongelesha tu hawana la kufanya wala la kushauri wapo kama bendera tu,

Spika wa bunge na hata Jaji nao wameshakuwa bendera

Kama sio kutuona mazwazwa ni nini?

Hebu niambieni kundi gani sasa hivi hata likifanyiwa uonevu gani linauwezo wa kujipigania na likashinda.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ni zaidi ya zwazwa!
 
Hapa ndo tunapokwama na wao ndio wanapotuona hatuwezi kuwafanya chochote!

Kwamba watuache tupige kura kihalali, kura zihesabiwe kihalali, na mshindi atangazwe kihalali! Kuwaza hivi ndo kunatufelisha

Nchi nyingi zilizofanikiwa kubadili uongozi zilijipanga kwa kuweka plan B. Wabongo plan B yetu iko wapi?

Wanajua hatuna plan B ndiomaana wanafanya wanavyotaka wao wala sio sisi

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndiyo maana nayaita maajabu hayo ninayoendelea kuyasubiri yatokee safari hii.

Nitayaona kuwa maajabu kwa sababu hata hao CCM hawajapata kutuvuruga kiasi cha walipotufikisha safari hii.

Mara nyingi wamekuwa wakitumia ujanja ujanja wa akina Kikwete, Makamba na wenzao...

Hawajawahi kutulazimisha kwa nguvu kama wanavyotuendesha sasa hivi.

Kwa hiyo nasubiri kuyaona maajabu haya ya Tanzania safari hii. Baada ya hapo, nitajua kwa hakika Tanzania yetu ni nchi ya kipekee sana.
 
Sasa hivi nadhani hata Mungu mwenyewe atakuwa anatushangaa!! Mimi naamini Mungu kachoka tunavyonyanyasika na ufedhuli wa "hugu gumchama", anatupitisha katika hii hali makusudi tuchukue hatua, lakini waaapi! Sasa atakuwa anafanya ulinganisho na kujiuliza "hivi ni taifa gani nililowahi kulipitisha kwenye utawala wa maudhi" wa kipimo cha WaTz na bado hawakuchukua hatua!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom