barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,322
- 29,583
Chagueni mbadala. Mbona simple ila mwisho wa siku wengi watashinda.Sijui kama niko sahihi kuiweka na CCM au abaki mwenyekiti peke yake mtasahihisha wenyewe
Japo wengi hatuzijui sheria ila hatukuzoea kuona waziri anaapishwa kwenye makazi binafsi ya mtu
Japo mambo hubadilika hatukuzoea kuona Spika anapewa kiburi na Rais
Japo dunia inaenda kasi hatukuzoea kuona Rais anatoa kauli za kuchanganya wakati wa majanga
Japo kila mtu na tabia zake ila hatukuzoea kuona mtu akihamia CCM au akiwa mwana ccm anakuwa huru kufanya analolitaka
Bungeni sheria hazifuatwi,
Mahakamani mashauri ili kuamliwa yanasikiliziwa kwanza,
Watumishi wa umma hawana tena uwezo wa kunyanyua mdomo kudai haki zao
Mapolisi wanaamrishwa kufanya chochote na wakubwa zao,
Wapinzani wanajiongelesha ongelesha tu ila hawana wanachoweza kufanya,
Vyama vya wafanyakazi vinajiongelesha tu havina la kufanya,
Mawaziri wanajiongelesha tu hawana la kufanya wala la kushauri wapo kama bendera tu,
Spika wa bunge na hata Jaji nao wameshakuwa bendera
Kama sio kutuona mazwazwa ni nini?
Hebu niambieni kundi gani sasa hivi hata likifanyiwa uonevu gani linauwezo wa kujipigania na likashinda.
Sent using Jamii Forums mobile app