Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kiukweli kwa takwimu hizi ulizoleta mleta Uzi zinathibitisha Pasi na shaka kwamba Tshs. Inafanya vizuri kwa kipindi hiki cha miaka minne ya mh. JPM kuliko miaka minne ya kwanza ya watangulizi wake. Hebu jaribu kupitia kwa makini utagundua hilo. Kipindi kasi ya kuporomoka kwa tshs ni ndogo kulinganisha na kipindi kilichopita.
huna data,ongea kwa twakwimu.
no research no right to speak
 
Ndo hapo sasa, Kikwete ndo aliporomosha, kama JPM Kwa miaka 4 imeporomoka Kwa sh100 , hata akmaliza 2025 atakuwa ameporomoka Kwa 200 or 300 in total, Kikwete 1000 + in total
Lakini watu walikuwa na hela mfukoni, vice versa is true
 
Kikwete alikuwa mtu wa watu, mpenda Amani, Ila kwenye utendaji ni zero kabisa ukweli lazma tuseme tuu, na asingekuwa na wazir wa ujenzi mbishi kama JPM sjui hata angejivunia kwa lipi labda kuinua mashirika ya upigaji kama NHC, na mifuko ya jamii n.k, na ni katika kipind cha Kikwete elimu iligeuka kuwa ya kuunga unga Sana na isiyo na thaman, nchi ilikuwa kama haina kiongozi Kwa kweli
.....kuna kpind alimpa Sjui chenge kuwa wazir wa Ujenzi jamaa alipiga karibia hela zote za miradi , na iliyotekelezeka ilikuwa substandard...af mwambafy Kikwete anacheka Cheka tuu

Kwa upande wa JPM kwenye social activities ni zero kabisa, complicator af mbabe Sana mixer na Dharau, exposure ndogo ila kwenye utendaji kazi jamaa hakunaga, miaka michache hii amepiga parefu sana, still Kura yangu nampa 2020 ,
Waziri mbishi? Sema ktk wizara zilizokuwa zinapewa pesa za kutosha ili kuwa wizara yake!! Wengine wanapewa 20% yeye anapata 95%!!!wangempa wizara ya elimu tukaona!! Alipokuwa wizara ya ardhi, ilikuwaje, wizara ya uvuvi?!! Kama wizara yako inapewa robo ya bajeti uliyoomba hata uwe mbishi vipi, huwezi fanya kitu
 
Kusema ukweli nchi ilihitaji mtu kama magufuli ili isonge mbele si unaona yupo madarakani na ukali wake bado watu wanapiga sasa asingekuwepo si ingekua balaa. Ishu inayomgalimu kwa sasa na kupelekea viongozi wengi kupiga hela ni uncertanity mtu hajui kesho yake yani kama hamna job security vile so mtu anaamua apige mapema hata akiwa kijiweni anakua anagalafu ana visenti vya kumuweka mjini ushauri wangu mzee awe anashaurika kidogo apunguze ukali viongozi wafanyekazi kwa kujiamini
 
huna data,ongea kwa twakwimu.
no research no right to speak
Mkuu nimetumia data ulizoweka hapa wala sikutumia data nyingine na ni just simple mathematics, labda utwambie data zako ulizoshusha hapa jamvini ni za kubumbabumba tu.
 
Mkuu nimetumia data ulizoweka hapa wala sikutumia data nyingine na ni just simple mathematics, labda utwambie data zako ulizoshusha hapa jamvini ni za kubumbabumba tu.
nimepitia data za BOT,wewe hapo LUMUMBA UTAZIPATA WAPI ZAIDI YA KUSUBIRI "SLOW SLOW " aje na chaki hapo ubaoni
 
huna data,ongea kwa twakwimu.
no research no right to speak
We jamaa inawezekana ukawa ni mjinga ila hujijui! Hapo kwenye post yako inaonyesha hadi 2015 dola iilikuwa 2200, so kwa maana yake ni jk kaiacha dola 2200, ila sasa ivi ni 2300 , so miaka minne ya magu imepanda kwa shilingi 100 tu!
 
JMK
2005 - 1 USD = 1050 TZS
2006 - 1 USD = 1100 TZS
2009 - 1 USD = 1250 TZS
-----------
200 TZS
JPM

2015 - 1USD = 2210TZS
2016 - 1 USD = 2200TZS
2019 - 1 USD = 2300TZS
-----------
90 TZS
Takwimu zako zinamjega usiyempenda, inabidi nikupe pole.
 
Kusema ukweli nchi ilihitaji mtu kama magufuli ili isonge mbele si unaona yupo madarakani na ukali wake bado watu wanapiga sasa asingekuwepo si ingekua balaa. Ishu inayomgalimu kwa sasa na kupelekea viongozi wengi kupiga hela ni uncertanity mtu hajui kesho yake yani kama hamna job security vile so mtu anaamua apige mapema hata akiwa kijiweni anakua anagalafu ana visenti vya kumuweka mjini ushauri wangu mzee awe anashaurika kidogo apunguze ukali viongozi wafanyekazi kwa kujiamini
Hashauriki Sasa.
 
Raisi wetu ndio kinara na alama ya taifa hivyo sisi raia wema ni wajibu wetu kukusaidia, kukuunga mkono unapo tenda sawa na kukukosoa ukienda tofauti iwe kwa bahati mbaya au makusudi.
Ni kwa bahati mbaya sana kipindi hiki cha miaka takribani minne umeonyesha kutenda na kuruhusu mambo mengi ya tofauti yanayoonyesha kushindwa. Sina maana kuwa hayapo yenye mafanikio, yapo. Ila huo ni wajibu wako tena sio kwa kulazimishwa bali uliuomba kwa kuzunguka nchi kujinadi unaweza na Watanzania eakakupa nafasi na wanakulipa na kukutunza kwa hilo.
Baada ya wananchi kugoma kujiandikisha na kuwa tukio la kwanza la aina yake hapa nchini, nimejiuliza sana UNAKWAMA WAPI?
Mbona umekuwa kiongozi wa kukwama mambo mengi unayoanzisha kwa mbwembwe? Hao wasaidizi hawakusaidii kukuepusha na aibu hizi za kitaasisi?
1. Hili linatokana na kauli zako za kuchagua upinzani hutaki kusikia.
2. Uliagiza korosho zinunuliwe na serikali wakati serikali haiwezi Fanya biashara, matokeo ni mateso kwa wakulima, umehujumu uchumi na kulitia aibu jeshi letu ulilolishi rikisha biashara hiyo ya korosho.
3. Makinikia na malipo ya kodi zetu kubaki story.
4. Pamoja na hao ulio ita watumishi hewa kuondoka umeshindwa kutoa nyongeza za mshahara za kisheria au kupandisha mishahara wakati bei za kila kitu zimepanda 50-100%.
5. Ajira hakuna kwa kiwango kikubwa ingawa unajinasibu kuongoza kwa kukusanya katika historia ya nchi. Zinakwenda wapi?
6. Matukio ya utekaji na mauaji ya kimafia yametamalaki katika kipindi hiki huku hatua za makusudi za kuweka wazi hazionekani.
MAONI;
Jee umefahamu unakwama wapi ili wenye mapenzi mema na nchi yao wakusaidie? Kwa nini usitambue uwepo wa vyama vya kisiasa kikatiba kisha kukaa roundtable na viongozi wake (bila kuhusisha TV na redio) na kujadiliana nini kifanyike kuirudisha nchi katika mstari kwa upendo na kuheshimiana? Hujui kuwa hizi kauli za viongozi kuwaita wengine "wadudu" zinachangiwa na tabia zako unazoonyesha hadharani?
Kuchaguliwa wewe kuwa Rais miongoni mwa RAIA 50m sio kwa ni bora kuliko wengine wote bali ni utaratibu lazima awe mmoja na bahati hiyo inaanguka kwa mmoja tuu.
Chuki nyingi zidi yako zinazalishwa na wewe mwenyewe Mheshimiwa Rais wangu! Ukimchukia binadamu naye atakuchukia. Na sio vizuri hali hiyo. Hebu fikiria tukio la 1979 kule Kagera ndio lingetokea wakati huo, jee morali ile ya kupigana vita tungekuwa nayo sasa hivi? Hapana.
TUAMBIE UNAKWAMA WAPI!
 
Write your reply...HAPA KAZI TU. Ndiyo inayowatesa nyote mnaompinga JPM,maana mlizoea kujipigia na kupata pesa za dhambi kwa kudhurumu jasho la wanyonge.Sasa ni wakati wenu wa kukinywea kikombe, wote mnaompinga JPM Mungu anawaona.
 
Mitanzania mingi mijinga acha ibanwe hadi sote tuwe na akili sawa.
Mtu anakuja kwenu hamna maji anasifia kununua ndege na fly over na sgr wakati wengi wenu hamtafika Dar
Ni kweli kabisa. Watu wanazugwa na bombardier, SGR, stigler goggle ilhali kijijini kwetu bara bara as am speaking hazipitiki kabisa.
 
Man! Magufuli is the best to you wewe uliyepo mjini; na si kwetu sie tuliopo huku vijijini Buzige. Huwezi kunishawishi uzuri wa Magufuli kwa lolote ilhali kijijini kwetu miundombinu ya bara bara ni mibovu kupindukia, sekta ya kilimo kavulunda ambayo ndiyo uti wa mgongo wetu sie wakulima.
Jipongezeni wewe na Magufuli kama wanufaika wa keki ya taifa, na si wanainchi wa huku kijijini kwetu.
Kama unaona kuna shida ni wewe,sisi tunaona Magufuli is the best President ever.Infact he is our dream President.Kama wewe hupendi Magufulization it's simple,hama nchi.Magufulization is here to stay.Mbona nchi ilipokuwa inafujwa kwenye awamu ya tatu na nne hamkusema?Sasa tumepata Rais anayejali taifa lake na kufanya mambo ya msingi,mnapiga makelele,viumbe wa ajabu sana ninyi.
 
Man! Magufuli is the best to you wewe uliyepo mjini; na si kwetu sie tuliopo huku vijijini Buzige. Huwezi kunishawishi uzuri wa Magufuli kwa lolote ilhali kijijini kwetu miundombinu ya bara bara ni mibovu kupindukia, sekta ya kilimo kavulunda ambayo ndiyo uti wa mgongo wetu sie wakulima.
Jipongezeni wewe na Magufuli kama wanufaika wa keki ya taifa, na si wanainchi wa huku kijijini kwetu.
Mkuu nakubali kwamba miundombini ya barabara nk.sio mizuri nchi nzima.Lakini kumbuka kwamba maendeleo ni hatua.Najua pia kwamba kuna kazi kubwa ya kufanya kwenye Kilimo.

Naomba nikutonye kwamba Kilimo kilianza kuharibiwa kwenye awamu ya kwanza.Nadhani unakumbuka utaifishwaji wa mashamba kwenye awamu ya kwanza.Ule ulikuwa mkakati wa kuharibu Kilimo.Kwa ujumla upo mkakati mkubwa wa kuharibu Kilimo,sio Tanzania tu,bali ni mkakati wa dunia nzima.Katika mkakati huu zinatumika mbinu nyingi,tena zingine za siri sana,ambazo Tanzania peke yake haiwezi kuzimudu.

Yapo kwa mfano mabadiliko ya hali ya hewa.Leo mkulima hajui lini apande mahindi,kwa sababu ya mabadiliko haya ya hali ya hewa. Maeneo mengi ambayo vuli kwa kawaida haikuwepo,msimu huu wa mazao vuli imerudi!!Huu ni mkakati wa kumchanganya mkulima kwa makusudi,ili asijue la kufanya,kwa hiyo asifanikiwe katika Kilimo.Kwa mtizamo finyu watu wanaweza kusema mabadiliko haya ni heri,lakini yana nia mbaya sana kwa wakulima.

Wapo wadudu wanaozalishwa kitaalamu ili wawe waharibifu zaidi au wasiweze kuuliwa na dawa kirahisi.Upo uzalishaji wa mazao ambayo yanaharibiwa na wadudu kirahisi.Utakumbuka kwamba mahindi ya zamani yalikuwa yanastahimili wadudu,kwa maana kwamba mbegu zake zilikuwa ngumu na kwa hiyo si rahisi kuharibiwa na wadudu.

Upo mkakati mkubwa wa kuhakikisha kwamba mbegu zetu za asili zinapotea,na tunaingiziwa mbegu za hovyo ambazo kama nilivyosema, zinashambuliwa na wadudu kirahisi.Upo mkakati wa mashirika makubwa kama IMF na World Bank kutupa ushauri mbovu,wakitushari tu-adopt miradi ambayo wao wanajua fika kwamba haina tija kwenye kuboresha Kilimo chetu, lakini sisi kwa ujinga wetu tunaikubali.Ndio maana pamoja na miaka mingi ya kuwa na miradi hiyo ya IMF na World Bank,kilimo chetu kinazidi kurudi nyuma.Jambo hili lilifanyika sana kwenye awamu za tatu na nne.

Mikakati ni mingi mkuu.Inawezekana wataalamu wetu hawajui mikakati hii au wanajua lakini wanashirikiana na wabaya wetu.Kwa hiyo usidhani mambo ni rahisi kama unavyodhani,mambo ni magumu sana.

Nimalizie kwa kusema,kwa kuwa mikakati ya kuharibu Kilimo ni ya kidunia, tunahitaji mikakati ya kidunia ili kuweza kukabiliana nayo.Niseme pia kwamba kwa sababu nilizotangulia kusema, tatizo sio Nyerere,Mzee Ruksa,Mkapa, Kikwete au Magufuli per se.,tatizo ni mchanganyiko wa mambo mengi,ukiwepo mfumo mbovu wa kidunia imposed on us.
 
Write your reply...HAPA KAZI TU. Ndiyo inayowatesa nyote mnaompinga JPM,maana mlizoea kujipigia na kupata pesa za dhambi kwa kudhurumu jasho la wanyonge.Sasa ni wakati wenu wa kukinywea kikombe, wote mnaompinga JPM Mungu anawaona.
kazi tu wakati uchumi unakufa? sasa hiyo kazi tu ni ya nini au ni kazi tu for nothing
 
Mkuu nakubali kwamba miundombini ya barabara nk.sio mizuri nchi nzima.Lakini kumbuka kwamba maendeleo ni hatua.Najua pia kwamba kuna kazi kubwa ya kufanya kwenye Kilimo.

Naomba nikutonye kwamba Kilimo kilianza kuharibiwa kwenye awamu ya kwanza.Nadhani unakumbuka utaifishwaji wa mashamba kwenye awamu ya kwanza.Ule ulikuwa mkakati wa kuharibu Kilimo.Kwa ujumla upo mkakati mkubwa wa kuharibu Kilimo,sio Tanzania tu,bali ni mkakati wa dunia nzima.Katika mkakati huu zinatumika mbinu nyingi,tena zingine za siri sana,ambazo Tanzania peke yake haiwezi kuzimudu.

Yapo kwa mfano mabadiliko ya hali ya hewa.Leo mkulima hajui lini apande mahindi,kwa sababu ya mabadiliko haya ya hali ya hewa. Maeneo mengi ambayo vuli kwa kawaida haikuwepo,msimu huu wa mazao vuli imerudi!!Huu ni mkakati wa kumchanganya mkulima kwa makusudi,ili asijue la kufanya,kwa hiyo asifanikiwe katika Kilimo.Kwa mtizamo finyu watu wanaweza kusema mabadiliko haya ni heri,lakini yana nia mbaya sana kwa wakulima.

Wapo wadudu wanaozalishwa kitaalamu ili wawe waharibifu zaidi au wasiweze kuuliwa na dawa kirahisi.Upo uzalishaji wa mazao ambayo yanaharibiwa na wadudu kirahisi.Utakumbuka kwamba mahindi ya zamani yalikuwa yanastahimili wadudu,kwa maana kwamba mbegu zake zilikuwa ngumu na kwa hiyo si rahisi kuharibiwa na wadudu.

Upo mkakati mkubwa wa kuhakikisha kwamba mbegu zetu za asili zinapotea,na tunaingiziwa mbegu za hovyo ambazo kama nilivyosema, zinashambuliwa na wadudu kirahisi.Upo mkakati wa mashirika makubwa kama IMF na World Bank kutupa ushauri mbovu,wakitushari tu-adopt miradi ambayo wao wanajua fika kwamba haina tija kwenye kuboresha Kilimo chetu, lakini sisi kwa ujinga wetu tunaikubali.Ndio maana pamoja na miaka mingi ya kuwa na miradi hiyo ya IMF na World Bank,kilimo chetu kinazidi kurudi nyuma.Jambo hili lilifanyika sana kwenye awamu za tatu na nne.

Mikakati ni mingi mkuu.Inawezekana wataalamu wetu hawajui mikakati hii au wanajua lakini wanashirikiana na wabaya wetu.Kwa hiyo usidhani mambo ni rahisi kama unavyodhani,mambo ni magumu sana.

Nimalizie kwa kusema,kwa kuwa mikakati ya kuharibu Kilimo ni ya kidunia, tunahitaji mikakati ya kidunia ili kuweza kukabiliana nayo.Niseme pia kwamba kwa sababu nilizotangulia kusema, tatizo sio Nyerere,Mzee Ruksa,Mkapa, Kikwete au Magufuli per se.,tatizo ni mchanganyiko wa mambo mengi,ukiwepo mfumo muovu wa kidunia imposed on us.
Kama mpango wa kuangamiza kilimo ni wa dunia nzima, swali;
1. je tuendelee kumwamini Magufuli kwa anayoyafanya kwa kuwa tu kilimo ni mkakati wa dunia?
2. Na kama mkakati wa kuvuruga kilimo ni wa dunia nzima, mbona sisi hatujawahi mskia (Magufuli) akiongea hivyo kwamba ameshindwa kuinua kilimo sababu ya mabeberu?
Habari za mvurugo wa kilimo ndo kwanza nazisikia kwako. Sasa ungekuwa wewe utawashawishi vipi wanakijiji wa buzige kwa hoja zako zilizo mafichoni? Maana wakulima wanajua kazi ya serikali ni kuratibu masuala ya pembejeo, mbolea, madawa, masoko n.k
 
Mkuu haya niliyoandika si rahisi kuyajua kama wewe sio mtafiti,mdadisi au msomaji mzuri.Ni personal initiative.B.Sc,MSc. au hata PhD haisaidii kuyajua haya,so inawezekana hata Rais wetu hayajui.Najua kwamba wataalamu wetu wengi hawayajui na ndio maana wanaingizwa mkenge kirahisi na mashirika kama IMF na World Bank.Ni muhimu viongozi wetu wakajua mikakati ya siri ya The World Shadow Government,The Elite au The New World Order(NWO),ili tusiingizwe mkenge kirahisi,ingawa consequences sake ni mbaya in the long run.Hawa jamaa wakiona wamebanwa sana wanaweza kufanya lolote,hata ku-initiate vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Hata hivyo naishukuru sana serikali ya awamu ya tano,kwa ujumla it is doing a good job.Kama viongozi wa serikali ya awamu ya tano wanafahamu mikakati ya The NWO au wanayafanya wanayoyafanya by coincidence sijui.
 
Nothing special in Tz ,poor roads ,heath care , mtu akioongea English sio mzalendo ni ushamba tu bora Africa kusini its a free county with great opportunities
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom