Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
kaikuta nchi imetulia? wakati nchi ilikuwa inanuka rushwa na hongo tena nje nje kila mwenye nacho alijiona na yeye ni rais anafanya anachotaka na hakuna wa kumgusa, leo unasema aliikuta nchi imetulia? au kutulia huko unakosema wewe ni kupi? sio kama nakubaliana na kila anachofanya hakuna mkamilifu kwenye utawala but dnt tell us kwamba hii nchi eti aliikuta vizuri now way
Tatizo mnasumbuliwa na mahaba ya kumpenda mtu badala ya kuutambua ukweli, Tanzania unasema imetulia?
Kwa hiyo unataka kusema hakuna rushwa Tanzania sasa hivi?
Mikononi mwa Magufuli Tanzania inanuka shida kuliko wakati wowote ule
 
YAANI ILI UPATE CHA KUMKOSOA MAGUFULI NI LAZIMA KWANZA UMSINGIZIE JAMBO HALAFU HICHO ULICHOMSINGIZIA NDIO KIWE MSINGI WA KUMKOSOA NA WENGINE HATA KUMKASHIFU NA KUMTUKANA. KWELIN MAGUFULI ANAFANYA KAZI ILIYOTUKUKA ISIYOKUWA NA LAWAMA HALISI
Wewe ni chizi nenda Mirembe haraka
 
Hivi rais Magufuli anaipasua nchi au anainyoosha?. Hii ni kufuatia kukabidhiwa nchi aliyoikuta imepinda sana hadi kupindukia, ameikuta nchi imeoza na kunuka uvundo mzito wa rushwa na ufisadi huku ikifanywa ni shamba la bibi. Kazi ya kwanza ya Magufuli ilikuwa ni safisha safisha kwa utumbuaji majipu na kuinyoosha nchi. Hata chuma kilichopinda kikinyoonywa kinapata moto.
Acha Magufuli ainyooshe Tanzania hadi inyooke, heri dikiteta mzalendo mwenye uchungu na umasikini wa Watanzania kuliko a smiling dhaifu huku nchi ikifanywa ni shamba la bibi!.
P
Hivi mkuu , je uvundo wa rushwa umeisha , umepungua , umeongezeka ama upo palepale?
Ufisadi haupo?

Nafikiri tusisifie saana pasipo kuangalia uhalisia wa mambo
 
hebu waonee huruma watanzania wanavyoteswa na shetani mkuu wa Tanzania.
Mkuu Chief Kabikula, sio haki, sio utu, sio heshima kumuita binaadamu wa Mungu kuwa ni shetani!. Hata Osama licha ya yote aliyowafanyia Wamarekani, hawakuwahi kumuita shetani, na kwa taarifa tuu, alifanyiwa ibada ya maziko kwa heshima zote za dini yake ikiwemo kuoshwa, kuvishwa sanda, kuswaliwa na sheikh wa Kiislamu na kuzikwa baharini kwa kutizamishwa kibla!. Mtu utamuitaje shetani?.
P
 
Mkuu kwani wako Kimya au wanakalishwa Kimya

1.Azory alikaa kimya?
2.Ben saanane je alikaa kimya?
3.Ngurumo yuko Kimya?
4.Zitto Yuko Kimya?
5.Je Ukimya ndo umemuweka kabendera kizuizini?
6.Fatma Karume yupo Kimya?
7.Maria Sarungi je

Kwakweli hatuko Kimya

Britannica
Samahani, nilidhani umeungana na namba tano hapo juu.

Anyways, mbona rangi inazidi kukorea? More assertive than I have ever read from you! No ambiguity or mipindisho!
 
Hivi mkuu , je uvundo wa rushwa umeisha , umepungua , umeongezeka ama upo palepale?
Ufisadi haupo?

Nafikiri tusisifie saana pasipo kuangalia uhalisia wa mambo
Kumbe wewe hauna elimu ya mambo ya vyuma. Kazi ya kunyoosha vyuma vilivyopinda sana na kukaa muda mrefu, hufanywa taratibu kwa kunyooshwa kidogo kidogo. Ukivinyoosha kwa nguvu, vitakatika.
Hivyo tunakwenda mdogo mdogo, sasa rushwa imepungua, ufisadi umepungua, maendeleo yanakuja kwa kasi, midege ile angani, madaraja ya juu kwa juu, viwanda vinajazana, reli ya SGR inakamilika, umeme wa Stigila unakuja, Tanzania ya viwanda inakuja, Tanzania ya uchumi wa kati inakuja, Tanzania donor country inakuja. Sasa kila nyumba itakuwa na mabomba matatu matatu, mabomba nchi nzima yatatoa maji, maziwa na asali.
P
 
YAANI ILI UPATE CHA KUMKOSOA MAGUFULI NI LAZIMA KWANZA UMSINGIZIE JAMBO HALAFU HICHO ULICHOMSINGIZIA NDIO KIWE MSINGI WA KUMKOSOA NA WENGINE HATA KUMKASHIFU NA KUMTUKANA. KWELIN MAGUFULI ANAFANYA KAZI ILIYOTUKUKA ISIYOKUWA NA LAWAMA HALISI
Wenye mawazo M-badala wanasikilizwa? Embu anzia hapo KUMSIFIA MAGUFURI nisije nikaambiwa namsingizia kitu kwenye kona hiyo
 
Kumbe wewe hauna elimu ya mambo ya vyuma. Kazi ya kunyoosha vyuma vilivyopinda sana na kukaa muda mrefu, hufanywa taratibu kwa kunyooshwa kidogo kidogo. Ukivinyoosha kwa nguvu, vitakatika.
Hivyo tunakwenda mdogo mdogo, sasa rushwa imepungua, ufisadi umepungua, maendeleo yanakuja kwa kasi, midege ile angani, madaraja ya juu kwa juu, viwanda vinajazana, reli ya SGR inakamilika. Tanzania ya viwanda inakuja, Tanzania ya uchumi wa kati inakuja, Tanzania donor country inakuja. Sasa kila nyumba itakuwa na mabomba matatu matatu, mabomba nchi nzima yatatoa maji, maziwa na asali.
P
Na polisi wakihakikisha uwepo wa u(hasa)ma/usalama wa raia katika ukamuaji /utumiaji wa maziwa na asali.
 
Mkuu, mwenzako ametoa hoja za ambazo unatakiwa uzijibu:-

1--- Mikataba ya ununuzi wa ndege iko wapi??

2--- Ujenzi wa Chato Airport

3--- Zilipo trillion sh 2

4--- Walipo akina Azori, Saanane, Kanguye.

Naye uumpe ajibu hoja hizi:-

1--- Ujenzi wa Bwawa la umeme stieglier

2--- Ujenzi wa SGR.

3---Ununuzi wa ndege

4--- Ujenzi wa maelfu ya zahanati.

5----Wanafunzi wa nsingi na sekondary kusoma bure na mikopo ya elimu ya juu.

6--- Uwajibikaji na nidhamu katika vyombo vya umma.

7--- vita dhidi ya ufisadi na Rushwa.

8---Kuongezeka kwa makusanyo ya kodi.

9--- Ufuatiliaji katika mikataba ya raslimali za nchi.nk.
Wewe unajisumbua bure,hivi unafikiri aliyofanya Magufuli hawayajui,wanayajua, ila wanajifanya hamnazo na hawayaoni.Tumesha ainisha sana yote aliyofanya Magufuli hapa JF.,lakini kila siku ni back to square one.Ni chuki binafsi na husda tu zinazowasumbua mkuu,hamna lolote.
 
Hii nchi bila Magufuli hatuwezi kwenda mbele. Kura yangu nitampa tu na hata kama ni miaka mingine aendelee kama Kagame aweze kuinyoosha hii nchi maana ni kweli ilikuwa imeoza. Wananchi mpeni tu kura, anapokesea ni mapungufu ya mwanadamu tu lakini kwa ujumla anajitahdi.
AENDELEE KUMALIZA muda (10yrs) wake, ila nitamuelewa akimalizia na katiba mpya. "End justify the means"
 
Kati ya wandishi niliokua ninawapa uzito na kuamini wana ujasili mkubwa wa kuhoji ni pamoja na ww, lkn kwa Bahati mbaya sana umekua mtu wa hovyo sana kuliko wale waliokua hovyo kabla yako. tafadhali njaa sisikupeleke pabaya, Usiwe Kijana wa "ndiyo bwana mkubwa".
Huyu Mayalla ashalegezwa na bahasha

Ova
 
Tunapo anzisha uzi tuwe na fact za kuwapa wanazengo attention ya kuusoma uzi na kuchangia kwa marefu na mapana
Kujenga ni kazi sana hasa ukiwa na wasaidizi walio kua wakiishi kimazoea magufuri kaingia madarakani alikua anajua kabisa kwenye uozo TRA makamishina waliweka hela adi kwenye vyombo vya maji TPA kulijaa uozo mtupu akajitaidi kurekebisha saizi yupo anapambana kurekebisha na kufufua shilika la reli tusisahau kua ATCL ilikua na hali mbaya sana nayo kaifufua binadamu wote tunamapungufu ila uyu mzee anamaumivu makubwa sana kwa nnchi kwani anajua viongozi wengi walivyo wapo ki maslahi sana wanao ishi dar es salaam nadhani wanaona jinsi jiji la dar es salaam linavyo rekebishwa kwa sasa dodoma napo kumenoga mikoa ni mingi Tanzania nazani wengi ni mashahidi uko mliko kunamaendeleo mengi sana yanayo fanyika ikiwemo ujenzi wa barabara vituo vya afya usambazwaji wa maji safi ni mengi mnoo yaliyo fanyika kwenye awamu ya tano

Ningumu kukidhi mahitaji na matakwa ya watanzania wote ata marekani nako Kuna watu awana kazi wanamaisha magumu na hawana ata makazi maalumu ko nnchi Kama Tanzania kwa kipindi hiki tunacho pitia ni kigumu Sana ambapo mambo yanayo fanyika kwa Sasa yalitakiwa yawe yashafanyika mda Sana
 
Kinacho onyesha mwelekeo wa nchi ni itikadi ya chama sasa bas ccm haina itikadi inayo onesha landa serikali hii inafwata mfumo wa kijamaa au kibepari(kineberu)hivyo tupo njia panda hata Magufuli mwenyewe ukimuuliza hii nchi ni ya kijamaa au kibepari(kibeberu) atashindwa Kukujibu kwa uhakika ndio maana tulitaka kwenye katiba mpya hilo liwekwe wazi.
 
Tunapo anzisha uzi tuwe na fact za kuwapa wanazengo attention ya kuusoma uzi na kuchangia kwa marefu na mapana
Kujenga ni kazi sana hasa ukiwa na wasaidizi walio kua wakiishi kimazoea magufuri kaingia madarakani alikua anajua kabisa kwenye uozo TRA makamishina waliweka hela adi kwenye vyombo vya maji TPA kulijaa uozo mtupu akajitaidi kurekebisha saizi yupo anapambana kurekebisha na kufufua shilika la reli tusisahau kua ATCL ilikua na hali mbaya sana nayo kaifufua binadamu wote tunamapungufu ila uyu mzee anamaumivu makubwa sana kwa nnchi kwani anajua viongozi wengi walivyo wapo ki maslahi sana wanao ishi dar es salaam nadhani wanaona jinsi jiji la dar es salaam linavyo rekebishwa kwa sasa dodoma napo kumenoga mikoa ni mingi Tanzania nazani wengi ni mashahidi uko mliko kunamaendeleo mengi sana yanayo fanyika ikiwemo ujenzi wa barabara vituo vya afya usambazwaji wa maji safi ni mengi mnoo yaliyo fanyika kwenye awamu ya tano

Ningumu kukidhi mahitaji na matakwa ya watanzania wote ata marekani nako Kuna watu awana kazi wanamaisha magumu na hawana ata makazi maalumu ko nnchi Kama Tanzania kwa kipindi hiki tunacho pitia ni kigumu Sana ambapo mambo yanayo fanyika kwa Sasa yalitakiwa yawe yashafanyika mda Sana
Well said Mkuu..
Nashangaa mleta Uzi hadi Leo hajui Magu anatupeleka wapi..!
Weka likizo itikadi ya siasa kwa muda utaona Magu anatupeleka wapi..!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom