Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Umesahau....amejenga barabara ..ameleta elimu bure....ameleta nidhamu serikalin...ameleta ndege....amekuza uchumi.kumbuk tupo uchum wa kat


Miaka mitano mingine kwa magufuliiii
Mkuu angalia upya hii comment yako kisha uandike upya
 
Type ufanunuzi wa uchumi wa Kati huku biashara nyingi zikifugwa,masoko magumu ya mazao embu teeleweshe
Sababu mimi Ni mmoja wapo wa hao wakulima nimevuna maindi na mpunga mwingi tu lkn hivi nachokwambia gunia la maindi bei 30,000 bei ambayo nikiuza hata nusu ya hasara sipati
 
Tuna Rais wa ajabu haijawahi kutokea "in TL voice"....huyu bwana katufanya wasomi wote tuonekane hatuna maana mtaani
 
Umesahau....amejenga barabara ..ameleta elimu bure....ameleta nidhamu serikalin...ameleta ndege....amekuza uchumi.kumbuk tupo uchum wa kat


Miaka mitano mingine kwa magufuliiii
Biashara hazitoki kabisa mtaani mkuu mitaji inaanguka tu
 
Sawa nimeelewa point yako,ila kaa ukijua shida anazopambana nazo ni nyingi mno.

Jamani Magufuli nae ni mtu kama sisi hivyo tutambue kua ye uwezo wake ni mkubwa kutuongoza miaka mitano.

Na kufanya mabadiliko haya ni uwezo wa ajabu,hivyo hata akija hapa naamini kwa tabia ya binadamu hakuna atakae amini pia
 
aisee inahitaji ujasiri wa hali ya juu sana

unapataje ujasiri wa kumtetea mtu ambaye katurudisha nyuma hivi?

kwa kipi hasa?

maisha magumu,

ajira hakuna,

biashara ngumu

saivi kila kitu kinasajiliwa ili kitoe kodi hadi pool table!

vikodi uchwara vimeongezeka hadi kumiliki youtube channel unalipia kodi kama vile serikali ndio inamiliki Youtube!

mishahara haipandi,

demokrasia imekandamizwa

hivi kweli mtu unapata kabisa ujasiri wa kumuombea kura mtu wa hivi?

tuweni serious bana tuache utani, miaka mitano imemtosha atupishe
 
Hatakama mmechelewa au hamkuwa na mpango wa kurekebisha mambo yafuatayo jirekebisheni sasa hivi vinginevyo hamtoamini kitakachotokea 28.10.2020.Watu wanasema wanajambo lao

1.Makato ya 18% bodi ya mikopo elimu ya juu badala ya makoto ya 8% iliyozoeleka
2.Malimbikizo ya mshahara
3.Vitambulisho vya 20000 kwa wafanya biashara
4.Utekaji watu,kupotea kwa watu na wengine kupigwa risasi
5.Nyongeza ya mshahara kwa mujibu wa sheria
6.Milioni 50 kila kijiji
7.Maisha yamekuwa magumu na kazi tunafanya
 
Mfumo wa vyama vingi upo kwa muujibu wa katiba. Hivyo basi wananchi wao ndio huchagua mgombea yupi wa chama kipi atuongoze.

Sasa matamshi ya mgombea urais kupitia CCM yanaonyesha wazi hapendi uwepo wa mfumo wa vyama vingi. Kwanza alipiga marufuku shughuli zozote halali za kisiasa . saizi anazunguka huko kwenye kampeni akitishia wananchi wasichague upinzani.

Je, huyu mwenyekiti ndio kwamba haoni uhalali wa mfumo wa vyama vingi? Nini kinamfanya achukie hivi uwepo wa vyama kinzani vya siasa?
 
Kuzuri! Tulimuhitaji huyu mtu siku nyingi, tumechelewa lakini potelea mbali

Tunamuhitaji tena kwa tano nyingine.
 
Pole sana, tumpe tano tena. Tano inayokuja utaona mabadliko makubwa.

Mambo mazuri yanahitaki uvumilivu.
 
Je anavuruga au anapalilia vyama vingi ulitaka afanye nini kwenye siasa za ushindani humsemi vizuri mshindani wako. Hiyo hakuna.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom