Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Hivi rais Magufuli anaipasua nchi au anainyoosha kutokana kuikuta imepinda sana?. Hata chuma kilichopinda kikinyoonywa kinapata moto.
Acha Magufuli ainyooshe Tanzania hadi inyooke, heri dikiteta mzalendo mwenye uchungu na umasikini wa Watanzania kuliko a smiling dhaifu huku nchi ikifanywa ni shamba la bibi!.
P
Magufuli kainyoosha nchi au ndiyo kaipindisha kabisa? Kunyoosha nchi unatoa hiki unaweka hiki. unaanzia toka kwenye conceptual, vision, objectives, mpaka plan of action. kila mtu anaelewa wajibu wake na nini afanye. Ukivuruga mfumo uliopo halafu usijenge mfumo mpya, unaleta vacuum, na tunajua kwamba NATURE ABHORS VACUUM.

Angalau wakati wa Azimio la Arusha ilijulikana tunatoka wapi tunakwenda wapi. mikakati ilikuwa wazi. maadui wetu walikuwa wanaeleweka. sasa hivi ni holela tu. HAPA KAZI TU maana yake nini? huu utaratibu wa kutumbua watu juu kwa juu, unaondoa uzembe na kuleta efficiency? ni wangapi ambao wanatendewa visivyo au kuonewa kwa sababu tu hawakupewa muda wa kusikilizwa? Hivi tunaweza kweli kusogea mbele kama nchi kama maamuzi yetu makubwa yatachukuliwa kwa kutumia hisia tu? kwamba kwa kuwa kuna watu WANATUHUMIWA kuchoma moto mahali, na kwamba wameachiwa kwa dhamana, na taratibu za dhamana zipo kisheria, basi Rais anaagiza tu kwamba WAKAMATWE MARA MOJA WAKAE NDANI!! Hapo wanarudi ndani kwa amri ya rais? au shauri linarejeshwa mahakamani? nani anajua kwamba wale ndio wahusika kweli?

Rais anafanya maamuzi mengi sana kwa hisia tu. tutaweza kweli kuwa competitive katika ulimwengu wa tekinolojia kali?
 
Lini chadema mtafanya uchaguzi wa mwenyekiti wenu na sekratarieti ya saccos yenu?
Kelele tu huku umebana pua eti katiba inavyunjwa na mpo kimya,"nonsense"

Jengeni saccos yenu
Kichwa chako kibovu kama cha kuku, soma hiyo ndiyo unijibu. I want sensible answers to that not ngonjela za lumumba. Nitakupima leo!


AMEANDIKA BABA ASKOFU BAGONZA (PHD)

Maana yangu hii:

- Wanaosema Mbowe kawa MwenyeKiti wa maisha, wanageuka na kuunga mkono kuondoa ukomo wa vipindi vya urais katika katiba?!
wamemtuma mtu alijifanya mkulima kutest zari, katesti, tusishangae majibu ya mahakama na msajili akayafanyia kazi.
kauli za juzi kwamba akiondoka atamwachia nani stigla, barabara, bomberdier na sgr imekupa jibu, usisubiri malaika.
WAtu hao hao, wanaomba Mungu wengine allah, kila uchao Mbowe asigombee uenyekiti, wanataka mtu wao, huku ni ikiwa haijulikani.


-Wanaounga mkono Mbowe apate mpinzani ndani ya chama chake katika uchaguzi, wanageuka na kupinga uwepo wa mgombea mwingine ndani ya chama chao hapo mwakani!?

Wanaopinga mgombea pekee kwenye chama cha jirani, hao hao wanapiga kura kwa mgombea pekee katika chama chao, tena wengine kwa kuwaachia wengine wawaandikie kwenye kura ili waaminike kuwa hawakuasi msimamo.

-Wanaotabiri na kutamani kuwa upinzani ufe, hao hao wanasisitiza kiongozi wa chama hicho anayeonekana mbaya, aondolewe. Si angebaki ili akiue vizuri!?

-Wanaoshabikia kuwa upinzani umeisha, wanageuka na kushangilia msajiri anapoandika barua ya kutishia kufuta usajiri wa vyama vya upinzani!? Afute nini ikiwa upinzani haupo?

Nilimaanisha contradictions hizi masikioni zikizoeleka zinaondoa radha ya maisha. Kwa shule zilifuta Debate Clubs?
 
Mkuu kwani wako Kimya au wanakalishwa Kimya

1.Azory alikaa kimya?
2.Ben saanane je alikaa kimya?
3.Ngurumo yuko Kimya?
4.Zitto Yuko Kimya?
5.Je Ukimya ndo umemuweka kabendera kizuizini?
6.Fatma Karume yupo Kimya?
7.Maria Sarungi je

Kwakweli hatuko Kimya

Britannica
Hao sio hata chembe ya tone Tanzania, wengi wetu tuko kimya na hatuwasaidi wachache wasemao ukweli, bila ya kujali itikadi, chama, dini, kabila au mkoa.

Mambo yakiendeshwa kombo waumiyao ni watanzania, sio chadema ,Act ama upinzani kwa ujumla.

Hao uliowataja hawawezi kuwa na uwezo wowote kama wayapigiayo kelele hayawadhuru watanzania wengi na hatutaunga mkono kupinga mambo yanapoendeshwa kombo.
 
Mambo yapo uvunguni, kachungulie uyaone. Ila wenzio waliochungulia wanapigwa BITI kama sio kupotezwa
Kama unashirikiana na mabeberu kuisaliti nchi kwa njia yeyote ile,unatukana viongozi,unapotosha wananchi kwa maslahi ya chama chako au binafsi,kwa nini usishuhulikiwe?Maslahi ya taifa,busara na hekima lazima vipewe kipaumbele.
 
Mitanzania mingi mijinga acha ibanwe hadi sote tuwe na akili sawa.
Mtu anakuja kwenu hamna maji anasifia kununua ndege na fly over na sgr wakati wengi wenu hamtafika Dar


Sasa ulitaka hao Watz wajinga wafanyeje wakati wao ni wajinga??, ni sawa na kumlaumu kuku kuendelea kukubali kufugwa na binadamu wakati hajitambui kwamba ipo siku atapigwa kisu.🤣
 
Penye moshi kuna moto, sasa ni dhahiri kabisa kuwa Magufuli hana mpango wa kuachia madaraka hata baada ya muda wake kuisha.

Mtu ambaye hata kipindi chake kimoja cha Urais hakijaisha tayari anatamani tena aendelee kuwa Rais huku akijiona yeye ni bora kuliko wenzake.

Kipindi kimoja tu cha Urais wake nchi ipo hoi kiuchumi huku kundi la mambumbumbu la UVCCM likishangilia Kila janga, hiyo si ajabu sana kwa sababu hata Hitler naye alikuwa na kundi la majuha lililokuwa linamshangilia.

Tunaojitambua tusikubali Magufuli aivuruge Hii nchi.

Amefanikiwa kuliweka bunge mfukoni na mahakama pia.

Hizo ni elements za udikteta, tukimwachia Magufuli afanye apendavyo hii Tanzania itakuwa Kama Burundi au Congo, ataiharibu sifa ya Tanzania kimataifa.
Amejitahidi sana kuzima nguvu za upinzani kwa uwezo wake wote.

Tusimame wote tumwambie Magufuli aheshimu katiba ya nchi

Jamani mbona hiyo hotuba wote tumeisikiliza hajamaanisha hivyo kama mnavyotaka watu waamini??? tatizo hatusikilizi maudhui ya hotuba nzima badala yake tunakata kipande tu chenye maneno tunayotaka wenyewe aidha kwa bahati mbaya au makusudi!!!
 
Sasa mbona hata hizo teuzi live na ikulu live zinafanyika muda na siku za kazi! Kwa hiyo na hao wanaofuatilia mubashara kupitia vituo vya luninga hawana kazi za kufanya!
Labda nikuulize teuzi zunafanyika kila siku?live
 
Wewe ni sehemu ya waliokuwa wanufaika wa ufisadi.Kinacho
wauma ni jinsi wafadhili
wenu walivyotumia mapesa kuhakikisha mnaingia ikulu lakini mkashin
dwa.Na wengi mlizoea kuishi Dar kwa kutumia vimemo,sasa magufulization imewaumbua.Ndicho kinachowatesa,poleni sana.


Mkuu, mwenzako ametoa hoja za ambazo unatakiwa uzijibu:-

1--- Mikataba ya ununuzi wa ndege iko wapi??

2--- Ujenzi wa Chato Airport

3--- Zilipo trillion sh 2

4--- Walipo akina Azori, Saanane, Kanguye.


Naye uumpe ajibu hoja hizi:-

1--- Ujenzi wa Bwawa la umeme stieglier

2--- Ujenzi wa SGR.

3---Ununuzi wa ndege

4--- Ujenzi wa maelfu ya zahanati.

5----Wanafunzi wa nsingi na sekondary kusoma bure na mikopo ya elimu ya juu.

6--- Uwajibikaji na nidhamu katika vyombo vya umma.

7--- vita dhidi ya ufisadi na Rushwa.

8---Kuongezeka kwa makusanyo ya kodi.

9--- Ufuatiliaji katika mikataba ya raslimali za nchi.nk.
 
Katiba inavunjwa... Tupo kimya!

Bunge halina tena makali... Tupo kimya!

Mahakama inaingiliwa... Tupo kimya!

Viongozi wanatoa kauli zinazokinzana kwenye suala linalofanana... Tupo kimya!

Watu wanauawa... Tupo kimya!

Watu wanatekwa... Tupo kimya!

Magerezani kama sokoni... Tupo kimya!

Watumishi,wafanyabiashara, wakulima, wastaafu, wahitimu na wananchi kwa ujumla wanalia... Wapo kimya!

JE, TUTAAMKA LINI??? TUTOKE NYUMA YA keyboard! MAKELELE MITANDAONI HAYATASAIDIA!

LET'S NOW WAKE UP AND TAKE ACTION!
Which action? Maneno tu? Onyesha vitenda. Mange si alijaribu wewe unashindwa nini?
 
Magufuli's efforts, heartfelt patriotism and economic maneuvers he is demonstrating for Tanzania, which we daily witness, are perfect and nice parables of the day to illustrate not only the precious future of Tanzania but the very near future of true hope for Tanzanians.

Of course he is the best leader of our time and perhaps of all time to have ever lived and ruled Tanzania.

Tumuombee!
Jinga kweli wewe, Tunamwombea Sana ili awahi kuondoka akaongoze malaika
 
Mkuu yaani wewe huoni baadhi ya watendaji wake wanaendelea kumwangusha nyakati fulani? Wanaiba pesa, na hii ni kwa kuwa haongozi peke yake. Waliiba hizo trillioni unazozisema ambapo sina uhakika hata kama una ushahidi nazo kuwa zillibwa.
Kwa hiyo CAG ni muongo?
Tuanzie hapo kwanza
 
Usikute wewe hapo akipita eneo lenu unapiga makofi.
So wee jitahidi kupiga makofi tu.kama unaweza mface ana kwa ana.
 
Nimekuelewa sana, naomba nikueleze tu kwamba usitake kupotosha umma kwa kupindisha kidogo tu, Mh Rais hakumaanisha unachojaribu kuwaaminisha watanzania, Rais hana mpango na kuendelea kuongoza kama unavyojaribu kucheza na hisia za watu, elimu uloipata usiitumie vibaya, subir miaka 10 ipite ndo uongee upuuzi huo.
Nimesema mimi au yeye ndo alisema kwa kinywa chake?
 
Hivi rais Magufuli anaipasua nchi au anainyoosha?. Hii ni kufuatia kukabidhiwa nchi aliyoikuta imepinda sana hadi kupindukia, ameikuta nchi imeoza na kunuka uvundo mzito wa rushwa na ufisadi huku ikifanywa ni shamba la bibi. Kazi ya kwanza ya Magufuli ilikuwa ni safisha safisha kwa utumbuaji majipu na kuinyoosha nchi. Hata chuma kilichopinda kikinyoonywa kinapata moto.
Acha Magufuli ainyooshe Tanzania hadi inyooke, heri dikiteta mzalendo mwenye uchungu na umasikini wa Watanzania kuliko a smiling dhaifu huku nchi ikifanywa ni shamba la bibi!.
P
Acha usenge ww
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom