Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kwa wenye macho yanayoona mbali (Kama mleta uzi) tuliliona hili. Sasa nadhani wengine wameanza kuona tunakoelekea(kama bado hatujafika).
 
Fanya maendeleo yote ya vitu lakini maendeleo ya watu na maisha yao ni lazima yaendelee, miradi mikubwa ya ujenzi w reli na umeme viendelee lakini pia bila kuathiri maisha ya watu huo ndiyo uongozi wenye uweledi, sasa leo wafanyakazi wapo taabani maisha yao yameathirika vilivyo wewe unaongelea miradi ya miaka kumi ijayo, so maisha ya watu yasimame?? Kisa wewe na familia yako upo vizuri. Hiyo ni roho ya chuki iliyo mbaya kabisa. Tumia elimu kubalance mambo yote haya yaende mbele. Unaacha kula ili ununue shati! Au unaacha kujitibu maradhi ili uende disko,
 
Wanandugu,
Nashangaa sana yanayotokea kwenye nchi yangu sasa hivyi...Viongozi wamekuwa sio wale tena wanaoshauriana kabla jambo halijafanyika.

Sasa hivyi unaweza kuona katibu wa wizara flani anafanya jambo baadae anakuja waziri analipinga...Sasa inakuwaje au kuna mtu yuko sehemu ananyanyua waya moja kwa moja kwa watendaji bila kupitia kwa waziri???

Nimwtafakari sana...Hata hii nchi ya viwanda tutaisikia kwenye Bomba.
 
Tulijionea Jana wakati Waziri Mkuu akisema kuwa mishahara inaongezwa lakini kisiri siri na si kwa matangazo. Lakini tulimsikia Bosi wake akisema mishahara haongezi hadi amalize miradi mikubwa, ambayo ni reli ya SGR na mradi mkubwa wa umeme wa Stieglers gauge! Full Drama
 
Mimi ni mmoja wa wanachama wa chama ambacho mwenyekiti wetu ni Jiwe, jiwe anatuumiza sana mioyo yetu. Msione kila mahali tunamsifu Jiwe lakini kiukweli mngejua mioyo yetu inavyoumia msingesema kitu, mioyo yetu inaumia kuliko mwanachama wa chama chochote kile hapa nchini lakini tunamsifu ili tupate hata sh. elfu saba siku isogee.

Jiwe anaumiza kuanzia viongozi wenzie mpaka wanachama wa kawaida, Jiwe amezungukwa na wanafiki wanaomsifia hata akifanya maamuzi yasiyo na faida kwa chama. Jiwe ametuondolea waliokijenga chama na kubaki na wasiojua chochote kuhusu chama ila kwakuwa wanamsifu.

Jiwe ukimkosoa wapambe wanampelekea taarifa, akizipata bila kufikiri anakuadhibu kwa namna yoyote ile. Wakati mwingine hata kama hujamkosoa ila mpambe akikuchonganisha nae basi imekula kwako, anapenda sana kusikiliza story za vijiweni.

Jiwe tuonee huruma wanachama wenzio, Jiwe umewamaliza wao sasa umeanza na sisi wenzio tuliokuwa pamoja kipindi chote cha kampeni. Tulikwenda porini pamoja, tulikwenda shinyanga pamoja, tukaenda bagamoyo pamoja lakini tulienda mpaka Tanga pamoja leo hii Jiwe umenitenda.

Asanteni sana Jiwe
 
FB_IMG_1530425217452.jpg
 
Back
Top Bottom